NGUVU ILIYOMO KWENYE MAOMBI (..MWISHO)
BWANA ANAKUJA |
- Kujinyenyekeza
- Kuomba (somo letu)
- kutafuta uso wa BWANA (imeongelewa kwenye Muungano wako na huo ulimwengu kwa kilasiku.)
- kuziacha njia zao mbaya (imeongelewa lwenye Ushikaji wako wa maagizo ya huo ulimwengu.)
basi tuitazame pia kujinyenyekeza
inamaana ya kujishusha au kuiacha thamani yako na kuiona si kitu mbele za bwana
muumba wako. Ambayo inakuwa imejengwa na mambo matatu nayo ni:-
- kukubali kufundishika
- kutii
- kuwa na kicho(hofu)
hivi vitu vitatu mbele za bwana ni
muhimu sana na vyote huanzia rohoni na kufikia kuviona nje kwa mtu ni baada ya
moyo wake kuwa umejaa hivyo vitu nakuwa mmoja na vitu hivyoo ndio huyo mtu hata
matunda ya roho unaweza kuyaona kwa wepesi kwake. Nje ya hapo utajijua wewe tu
ukiwa unamtukia mungu bali watu wa nje hawawezi hata kulijua hilo. Hapa sizungumzii
walokole nazungumzia mtu mwenye safari ya kwenda mbinguni kwamaana YESU alileta
uzima wa milele ambao hakusema kuwa ni kuokoka bali ni kumjua MUNGU wa pekee na
yesu kristo mwanaye aliyemtuma yohana 17:3.
Na pia haiishi hapo inatakiwa
kujivika nila yake ili tuwe naye kweli lakini ili MUNGU asikuache inabidi kufanya
yale yampendezayo kwamaana nyingine ili udumu katika uso wa bwana mungu wetu
inabidi ufanye mda wote yampendezayo yeye. Ukisoma yohana 8:28-29 utakutana na
neno wakati wa kufundisha yesu anasema neno siyo la kwake bali la kufundishwa
na baba na akilisema au kulitenda naye baba anakuwepo mda wote naye ili
kulilinda neno aliloagiza lisemwe au litendwe kwa jina lake. Unaweza usielewe kwa
haraka lakini namaanisha mtazame YESU aliposema lolote muombalo kwa jina langu
hilo nitalifanya. Lakini siyo kila mtu akitumia jina la yesu, yesu atatenda
bali lazima uwe umeitwa kwa jina lake au umefanyika kuwa mwanafunzi wake . na
ili akuhesabu hivyoo ataangalia ushikaji wako wa maaagizo yake
. Hapo ndipo njia mbaya nazo
hutazamwa YESU aliweka kila kitu kiendacho kwa baba kipitie kwake yeye na
hakuna njia nyingine na kama ukitumia jina jingine kuomba kitu utakuwa unaomba kutoka kwa mungu
wa ulimwemgu huu wala siyo mungu wa mbinguni aliyeumba mbingu na nchi 2wakorintho
4:4. Basi ndugu na rafiki yangu achana na njia zako mbaya naye MUNGU atakusikia
na atakusamehe dhambi zako. Na ndipo macho yake yatafumbuka, na masikio yake yatasikiliza maombi yako
2nyakati 7:15&17.
Kingine ni hofu ya kutenda dhambi inatakiwa itawale ndani
yako maana utakuwa unaogopa kumkosea MUNGU na ndipo utaenenda vizuri. Na wala
siyo kuogopa waumini wenzio maana hukumu nao ipo juu yao. Kwamaana kwa sheria
wote tulihukumiwa kifo na mwanzo tulikuwa hapo wote. Bali ROHO alibatilisha kwa
kutuhuisha kutoka uharibifu mpaka kutoharibika ambako ndiko kuwa na uzima wa
milele. Basi pia tafuta kujazwa na ROHO WA MUNGU ndipo dhambi utaishinda na
wala siyo kwa kushika sheria. Maana ashikaye sheria huyo ni mtumwa wa hiyo
sheria bali sisi kwasasa ni watumwa wa YESU na malipo ni ROHO MTAKATIFU aletaye
uzima wa milele ndani yetu.
MWISHO
MWANDISHI: MICHAEL BASA 0765279698 au+255 789 799 199
Hakuna maoni
Chapisha Maoni