Header Ads

MAMBO YA MKE MWEMA KWA MUMEWE

Leo tujifunze namna ya mke mwema anapaswa kuwa kwa mume wake! (kuwa mwanamke wa kiroho,) hii inabeba mambo yafuatayo:

1. kuwa mnyenyekevu ( usimjibu vibaya au kumpandishia sauti mme wako ni

isahara ya kukosa heshima kwa mmeo MITHALI 15:1

2. usitoe siri za ndani za udhaifu wa mme wako kwa watu wengi (marafiki,

family) WAEFESO 5:12

3. kamwe usimfananishe mme wako na wanaume wengine ( mbona mme wa

fulan yuko hivi au anafanya vile )

4. Hata kama huwapendi marafiki wa mme wako usigombane nao acha mme

wako amalizane nao MITHALI 15:13

5. usijisahau majukum yako kwa mme wako hata kama una house girl ( mme

wako amekuoa wewe sio mfanyakazi) MWANZO 2:24

6. kamwe usigawe majukum ya maangalizi ya mme wako kwa MTU yeyote

....mfanya kazi afanye kazi nyingine zote Ila mme wako ni majukum yako

WAEFESO 5:33

7. kamwe usimlaumu mme wako kwann amekuja nyumbani mikono mitupu

mtie moyo kesho atapata TORATI 3:28

8. Jua kutumia pesa vizuri usiwe mharibifu na kutumia pesa ovyo za mme

wako jasho LA mme wako ni LA thamani kupotea hovyo

9. usijifanye unaumwa kwaku mnyima kufanya tendo LA ndoa na mme wako

(mke na ampe mme haki yake....mke hana amri juu ya mwili

wake.....msinyimane) 1korintho 7:3-5

10.Usimjibu vibaya mme wako mbele ya watoto, wageni, au umati wa

watu.....subiri mfike nyumbani mtatue matatizo yenu

11.Hakikisha unaandaa mavazi ya mme wako kila siku....na kabla hajatoka

hakikisha smartness yake kabla hajatoka

12.usiwaache marafiki zako wa kike kua karibu zaid na mme wako usiamin

13.usiharakishe kutoka bafuni wala kwa dressing table hakikisha uko vizuri

siku zote maana huko njee mme wako anakutana na wanawake waliotumia

muda wao bafuni na kwa dressing table ( usijipambe jitunze)

14.Wazazi, marafiki, ndugu, hawana usemi was mwisho kwa ndoa yako

Wamuzi ni wewe na mmeo

15. Usioneshe upendo kwa mme wako kwa wakati akiwa na kitu mheshim na

umtii, kuwa mnyenyekevu na umpende hata kama unamzidi kipato LUKA 21:16

16. Usiwe busy kwa mme wako kumbuka anahitaji umsikilize uwe na mda kwa

jili yake usiwe na ubize anapoongea na wewe acha unachofanya na umjib

usimjib huku unaendelea na mambo mengine

17.Kama umetowa wazo na likaleta mafanikio usijifanye unaakili kumzidi nyie

ni kitu kimoja.

18. Mwanamke mvivu hawezi kujali mme hawezi kujua kama mme wangu

anahitaji kuoga kula n.k

19. Wanaume hawapendi uchafu hata kidogo.....kuwa msafi kuanzia

mwonekano mpaka chumba cha kulala

20.kuwa mbunifu kwa mme wako.......Fanya zaidi vile vitu anapenda

asivyopenda viache Mara moja

21.Usilazimishe mme wako afanye vile unataka hata kama ni

vibaya......usimuombe vitu vya gharama kuzidi uwezo wake....

22.Jua lugha ya kuzungumza na mmeo akiwa anahasira nyamaza au tumia

polite language , ( Tafadhali, naomba, nisamehe, nakupena, Asante)

23.: kuwa mkarimu kwa wageni wote, usibague upande wako!

24.MPE glass ya maji mme wako baada ya kufika nyumbani kama

ukaribisho.....Fanya hivyo hata kwa wageni waingiao na kutoka malongoni

25.Usiwe na marafiki wenye mawazo hasi na mitazamo mibaya na Tania

mbaya zisizo faa kuigwa

26.Ndoa yako ni yathamani kwakadri unavyoithamin, iheshiim na kuilinda

27.Uzao wa tumbo lako ni baraka kutoka kwa Bwana ....wapende watoto wako

na uwafundishe njia iwapasayo MITHALI 22:6

28.Hata kama umri umeenda na mmezeeka usipunguze na usiache majukum

yako kwa mme wako

29.Mwanamke mwenye maombi ni ngao tosha ndani ya nyumba....Omba siku

zote kwajili ya family yako, mme wako na watoto wako....na watu wengine!

Pia angalia kwenye katabu cha mithali 31:10-31. Bwana akubariki

unapoendelea kujifunza. Amina.
pakua pdf hapa

Mwandish; Michael Basa(0765 279 698, +255 789 799 789)

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.