KUUSHINDA ULIMWENGU
Yesu kristo aliwahi kusemajuu ya
kujipa moyo kwa mtazamo wa kuwa kila kitu cha ulimwengu ni wale wa ufuatao
ulimwengu na tamaa zake nao huwapenda na kuwafurahia bali kwa wale wasioupenda
au wanaoenda kinyume nao huwachukia na kutamani wasiwepo bali yesu anasema
JIPENI MOYO kwamaana nyingine njia uliyoishika haiwezi kuwa katika wepesi wa
maisha yako bali kwamaana yeye anayeenda kinyume na ulimwengu huu yeye anakuwa
si wa ulimwengu huu yohana 8:23( Akawaambia, Ninyi ni
wa chini, mimi ni wa juu; ninyi ni wa ulimwengu huu,
mimi si wa
ulimwengu huu.)kwa
hiyo kama wewe si ulimwenguu huu hauwezi kuyatenda mapenzi ya ulimwengu huu
ambayo dhahiri ni matendo ya mwili wala si ya ROHO ambayo yapo wagalatia 5:( 19
Basi matendo ya mwilinidhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi,
20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui,
ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,
21 husuda, ulevi, ulafi, na mambo
yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha
kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa
Mungu.)
Ukiyasoma hayo
matendo mengi yanapendwa na watu wa ulimwengu huu lakini ni matendo ambayo
kwayo huwezi kuurithi ufalme wa mbinguni . hebu tazamo jinsi tunavyokaa sisi na
marafiki zetu jinsi wanavyotushauri je ni mambo ambayo yanatupeleka mbinguni au
ni yale ambayo yanatuondolea utakatifu.Na piindi ukiyakataa unaonekana mshamba usiyejua kitu au wa ajabu sana. Namimi nakushauri jipe moyo maana
MUNGU aliyetupenda kwaajili yetu akamtoa mwanawe wa pekee ili afe na afanyike
ondoleo la dhambi kwwetu yupo karibu zaidi na kwa upendo wake usiokoma. Sisi hatukumpenda yeye bali yeye ndo alitupenda sisi
na hakika YESU alipoondoka hakutuacha tutange tange(kama yatima)bali alituachia ROHO
wa MUNGU akae na hao watakaopokea na kuamini INJILI yake yohana 14:( 16 Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele;
17 ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu.
18 Sitawaacha ninyi yatima; naja kwenu.)
yohana 16:(33 Hayo nimewaambieni mpate kuwa na
amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni
moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.)
Mwandishi MICHAEL BASA(0765 279 697,+255 789 799 199)
Hakuna maoni
Chapisha Maoni