KANISA KAMA MAKABURI YALIYOPAMBWA KWA NJE NA WAKATI NDANI YAMEJAA MIFUPA NA VITU VILIVYOOZA.
CHRIST’S GOSPEL INTERNATIONAL MINISTRIES..
Hii
si kumwabudu Mungu bali ni kujifariji, kukimbiza upepo, kujidanganya na
kudanganyika kupoteza muda bilakujielewa na kutembea katika giza ndani ya nuru.
“na hii ndiyo hukumu ya kuwa nuru
imekuja ulimwenguni na watu wakapenda giza kuliko nuru kwa maana matendo yao
yalikua maovu” Yoh 3:19.
Nani kakudanganya kuwa kanisa ni jengo?
Hivyo kuingia kwako katika majengo hayo nawe umekua sehemu ya kanisa!!! Kanisa
ni mwili wa Kristo yaani wa YESU na
hujengwa na watu watakatifu waingiao mahekaluni. Jiulize je, wewe ni mtakatifu? Je wewe ni sehemu ya
mwili wa Kristo? Au unaenda hekaluni kujaza viti na kuuza sura? “Naye ndiye kichwa cha mwili yaani cha
kanisa….” Wakolosai 1:18-19.
Hakuna kitu kibaya kama unafiki,umefika
mbali sana maana hata Mungu unampaka mafuta kwa mgongo wa chupa? Kumuonyesha
mchungaji kuwa muumini wake wakati wewe ni mtenda dhambi haina msaada kwa roho
yako. Yesu mwenyewe anawachukia sana wanafiki kama wewe unayejidanganya kuwa
mtu wa rohoni wakati wewe ni wa dhambini. “ole
wenu waandishi na mafarisayo wanafiki! Kwa maana mmefanana na makaburi
yaliyopakwa chokaa nayo kwa nje yanaonekana kuwa ….bali ndani yamejaa mifupa na
uchafu wote” Mathayo 23:27-33. Mstari wa 33 “enyi nyoka wana wa majoka, mtaikimbiaje hukumu ya jehanamu?”
Acha kuidanganya roho yako ubadilike kuanzia
leo maana matendo unayofanya si ya ki MUNGU
bali ya kishetani kabisa. Unaenda hekaluni kwa lengo la kujulikana tuu na si
kwenda mbinguni, badilika sasa maana Yesu yu karibu kurudi “tubuni kwa kua ufalme wa Mungu umekaribia” Mathayo 3:2.
Hayo uyafanyayo kwa siri ni matendo ya
mwili na watu kama wewe wamewekwa akiba kwa ajili ya ziwa liwakalo moto yaani
jehanamu pamoja na baba yao Shetani au Ibilisi. “basi matendo ya mwili ni dhahiri ndiyo haya uasherati, uchafu,
ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, uzushi,
husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofana na hayo….ya kwamba watu watendao
mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa mungu” Wagalatia 5:19-21. “bali
waoga na wasioamini na wachukizao na wauaji na wazinzi na wachawi na hao
waabudio sanamu na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na
kiberiti….” Ufunuo 21:8.
Sikia nikupe maarifa ya kiMungu haya yote
unayafanya na unasema umeokoka muongo acha mara moja;
1.
Wewe
ni mzinzi mpaka umekua kero kwenye nyumba za majirani zako. (UTAKUFA NA UKIMWI)
2.
Unavaa
nguo za wadogo zako au zilizo kuruka hakuna anayependa kukuona ukiwa uchi (UMEKUWA KAMA MDORI)
3.
Unavaa
suruali kata kei(chini ya kiuno chako) kama
hauna mgongo…………..Mmh
4.
Lugha
yako si Kiswahili wala kiingereza bali ni matusi acha mambo hayo.
5.
Unaishi
na wasiwasi kama unakufa kesho, si mpango wa MUNGU ni wa shetani huo.
Hivyo ni baadhi ya vitu uvifanyavyo na
bado unajiita MLOKOLE na unesema
utafika mbinguni. Mbinguni si rahisi kuingia kama unavyodhani badilika dada na kaka yangu.
Yesu anasema hakuja kwa ajili ya wachungaji, wainjilisti, mashemasi
bali kwa ajili ya mwenye dhambi kama wewe “Sikuja
kuwaita wenye haki bali wenye dhambi wapate kutubu” Luka 5:32. Nafasi ya kutubu
na kusamehewa ipo kwa ajili yako “tazama nasimama mlangoni, nabisha,mtu
akisikia sauti yangu na kufungua mlango nitaingia kwake nami nitakula pamoja
naye na yeye pamoja nami.
Kama unashindwa kuacha dhambi na
unasumbuliwa na shida yoyote nitafute na YESU atakuweka huru
mbali na dhambi kabisa.
TO
THE LORD BE THE GLORY.
PRERARED
BY FOUNDER BUNGUBULIHO F.M Phone
0755285414 or 0716453335
WELCOME
IN THE FAMILY OF JESUS CHRIST. Forwarded by BASA MINISTRY.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni