JINSI YA KUDUM KATIKA UWEPO WA BWANA
- KUDUMU KWENYE MAOMBI
Kwa
watu wengi maombi kwao ni
- nikupeleka matatizo yao yanayoitaji ufumbuzi
- kupeleka shukrani kwa kile alichotenda MUNGU kwenye maisha yao
- kumsifu MUNGU
ambayo
ni moja ya mambo yanayokamilisha ibada lakini maombi yanaenda zaidi ya hapo na
kuna mda mwingine MUNGU huongea na watu na kutoa majibu mengi kwa watu wake
ambapo huwa ni kuzungumza na mtu na mda pekee kwa wengi ambapo moyo huwa
unamwelekea MUNGU ni kwenye maombi ISAYA
1:18 mungu anataka kuja kusemezana naye bila kujali wewe unadhambi kias gani.
Pia MUNGU kwetu ni baba na tunapaswa kwenenda kama watoto wanaopendwa je ni
baba gani anayependa watoto wake ambaye hana mda wa kuzungumza naye waefeso 5:1
2 USHIRIKA NA WATU WA KIROHO
Tabia huambukizwa au
kurithishwa kutoka mtu mmoja mpaka mwingine na ndio hizo watu husema “nikitaka
kukujua wewe ni nani nionyeshe rafiki zako”. Kukaa na watu wa kiroho kwa mda
mrefu ile tabia ya kutenda mema huwa unairihi kwasababu zifuatazo:-
- Kukatazana kutenda maovu
- Kushauriana kwa neno
- Kungojea ufalme wa BWANA kwa saburi pamoja
- Kuombeana pale wanapokuwa na tatizo Zaburi 33:1,
3.KUSOMA NENO
Biblia
iasisistiza sana kwenye kulijua neno maana neno ni kweli kabisaa na kuijua
kweli humuweka mtu huru yohana 8:32b na
pia neno linatakiwa kukaa kwa wingi ndani yako wakolosai 3:26
kwa kujifunza zaidi pitia HAPA
kwa kujifunza zaidi pitia HAPA
4.KUOMBA UWEPO WA ROHO MTAKATIFU KWENYE MAISHA YAKO
WOKOVU
NI SAFARI ambayo inaanzia pindi tu mtu anapookoka na mwisho wake ni kuingia
katika ufalme wa mungu ambapo huyo ndio anakuwa ni mrithi aliyekuwa thabiti
kutembea chini ya neema ya yesu kristo ambapo kuna watu hukomea njiani na
kukata tamaa kwa kuzongwa na shughuli za kidunia na wengine hushindwa kujilinda
na tamaa za mwili na kujikuta wametawaliwa na mambo ya uharibifu kama uzinzi nk
ambapo hao wote wanahesabiwa kama walioshindwa kuendelea na safari na wala roho
wa mungu hayuko kwao 1YOHANA3:9 Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake
wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na
Mungu..
ROHO
WA MUNGU NI
- MWALIM WA KWELI YA MUNGU
Marko 13:11 Na watakapowachukua ninyi,
na kuwasaliti, msitafakari kwanza mtakayosema, lakini lo lote mtakalopewa saa
ile, lisemeni; kwa maana si ninyi msemao, bali ni Roho Mtakatifu Luka 12:12 kwa kuwa Roho Mtakatifu atawafundisha saa ile ile yawapasayo kuyasema. Yohana 14:26 Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha
yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.
- MLINZI WA ROHO ZETU
2Timotheo 1:14 Ilinde ile amana nzuri kwa Roho Mtakatifu akaaye
ndani yetu.
- KIUNGANISHO CHETU NA MUNGU
Matendo 5:32 Na sisi tu mashahidi wa
mambo haya, pamoja na Roho Mtakatifu ambaye Mungu amewapa wote wamtiio.
2Wakorintho 3:17 Basi Bwana ndiye Roho; walakini alipo Roho wa Bwana, hapo ndipo penye uhuru.
Waefeso 4:30 Wala msimhuzunishe yule Roho Mtakatifu wa Mungu; ambaye kwa yeye mlitiwa muhuri hata siku ya
ukombozi.
- MWOMBEZI WETU
Warumi 8:27 Na yeye aichunguzaye mioyo
aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu.
Warumi 8:26 Kadhalika Roho naye hutusaidia
udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza
kutamkwa.
2Wakorintho1:21 Basi Yeye atufanyaye imara pamoja nanyi katika Kristo, na kututia
mafuta, ni Mungu, 22 naye ndiye
aliyetutia muhuri akatupa arabuni ya Roho mioyoni mwetu.
- KIONGOZI WA WOTE WALIITAO JINA LA BWANA KATIKA HAKI NA KWELI
Wagalatia 5:18 Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria.
- MFARIJI
Matendo 9:31 Basi kanisa likapata raha
katika Uyahudi wote na Galilaya na Samaria, likajengwa, likiendelea na
kuongezeka katika kicho cha Bwana, na faraja ya Roho Mtakatifu.
- MTETEZI WETU KWENYE MATATIZO MBALI MBALI
Luka 12:12 kwa kuwa Roho Mtakatifu atawafundisha saa ile ile yawapasayo kuyasema.
- ALAMA YA WOKOVU
Yohana 16:13 Lakini
yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana
hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na
mambo yajayo atawapasha habari yake.
Warumi 8:14 Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu.
Mwandishi MICHAEL BASA 0765 279 698, +255 789 799 199
Hakuna maoni
Chapisha Maoni