Header Ads

UTATU WA BINADAM( HUMAN DIVINITY)

basaministry
HUMAN DIVINITY
Kutoka kwenye uumbaji kila mtu unayemuona bila kujali ameokoka au hajaokoka amegawanyika sehemu tatu ambazo MUNGU anazihesabu nazo ni 1. roho,  2. mind (soul),  3. Mwili. Kama ilivyoandikwa kwenye  1wathesalonike.5: 23 Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.
Ili binadamu afanye ya kazi yoyote hapa duniani kwa mafanikio inatakiwa vitatu vyote vifanye kazi kwa pamoja.  Ila kazi ya kiMUNGU inahitaji viwili kati ya hivyo au vyote vitatu; ambapo MUNGU alichagua roho ili iwe sehemu kuu ya kupokea maagizo na kutunza maagizo yake.
Bali shetani hutumia mwili kama mlango wa udhaifu wa mwanadam yeyote ili ayafanye mapenzi ya shetani warumi 7: 18 Kwa maana najua ya kuwa ndani yangu, yaani, ndani ya mwili wangu, halikai neno jema; kwa kuwa kutaka nataka, bali kutenda lililo jema sipati.
warumi8: 8 Wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu.
.  Nafsi yenyewe husubiri ni upande upi kati ya roho na mwili unaokuwa na nguvu kwa muda huo. kwahiyo mind (nafsi)  huwa kiunganisho cha mawasiliano kati ya mwili na roho.
Mtu akiokoka anatakiwa roho yake ndiyo iwe na nguvu ya kumiliki na kutawala nafsi (akili) yake, na kwamba mwili uwe unafuata kile roho inataka kifanyike warumi 7: 19 Kwa maana lile jema nilipendalo, silitendi; bali lile baya nisilolipenda ndilo nilitendalo.
 20 Basi kama lile nisilolipenda ndilo nilitendalo, si mimi nafsi yangu nilitendaye, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu.
Sasa  mwili, nafsi na roho kwa pamoja huunda utatu wa binadamu.  Utaona kuwa roho inatakiwa ibaki imeungunishwa na muumba wake, na mwili ni kutaka kutenda tamaa za dunia hii  (warumi 8: 19 Kwa maana lile jema nilipendalo, silitendi; bali lile baya nisilolipenda ndilo nilitendalo.
 20 Basi kama lile nisilolipenda ndilo nilitendalo, si mimi nafsi yangu nilitendaye, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu.
warum12:2 Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu
kwa hiyo kama ilivyoandikwa kwenye  warumi.8:6-7,  mwili nia yake ni kinyume na nia ya roho, hivyo kunakuwa na uadui kati ya mwili na roho. Basi matendo yote ya kidunia ambayo ni ulevi,wizi,uongo, maseng’enyo,uzinzi, uasherati ,kiburi, kutaka sifa,husuda,chuki,uchoyo,kutunza hasira,kushindwa kusamehe na mengine kama hayo yote ni matendo ya mwili na kamwe hayampendezi MUNGU 1petro2:11 Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho.
Njia pekee ya kuyashinda matendo ya mwili au njia pekee ya kumpendeza MUNGU ni kuiruhusu roho yako kuutawala mwili wako. Na njia pekee ya kuifanya roho yako ipokee maagizo ya muumba wako ni kuruhusu roho yako na ROHO MTAKATIFU kuwa kitu kimoja.
Na jinsi ya kumfanya ROHO MTAKATIFU kuwa kitu kimoja na roho wako ni kumpokea YESU KRISTO aje atawale maisha yako kweli kweli au kwa maana nyingine kumwabudu MUNGU katika roho na kweli (yohana 4:24), kisha baada ya hapo ni UBATIZO WA MAJI MENGI na baada ya hapo ni kumpokea ROHO MTAKATIFU ili aje akufundishe yote yakupasayo (yohana 14:26)


Kila anapokufundisha inatakiwa ukiweke kwenye vitendo hicho alichokufundisha (yakobo1:22). Pia ujitahidi matunda ya ROHO MTAKATIFU yaonekane kwako ambayo ni  upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.(wagalatia 5:22-23)

Mwandishi MICHAEL BASA 0765 279 698, +255 789 799 199

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.