KWA KILA DINI
kwa kila dini |
Wote
tunajua kua tumbo la mwanamke limeumbwa kiasi kwamba damu ya mama hai-ingiliani
na damu ya mtoto aliye tumboni mwake. Hili ni jambo la kisayansi na ndio maana
mama mwenye virusi vya ukimwi anaweza kuzaa mtoto asiye na virusi kama
hakutatokea mchubuko kwa mtoto wakati wa kujifungua. Na wote tunajua kuwa MUNGU
anajua mwanzo na mwisho wa kila kitu. Kwahiyo ni kweli MUNGU alijua kuna siku
Adam atafanya uasi na kutenda dhambi.
Na MUNGU
siku zote anaziheshimu sheria zake; Na katika uumbaji wake aliweka sheria ya
urithi. Yaani kila binadamu anaezaliwa kwa muunganiko wa sperm cell na egg
cell lazima arithi sifa za mama na baba (heredity). Kwahiyo kwa njia ya
urithi, dhambi iliingia ulimwenguni kupitia kwa mtu mmoja yaani Adam. Na
kupitia dhambi hii, mauti ikawafikia watu wote, kwani kwa njia ya urithi, wote
wamefanya dhambi hata kama hawakutenda dhambi kama Adam.
Baada
ya dhambi kuingia ulimwenguni… Siku ileile MUNGU alikuja na mpango mwingine
akasema Mwanzo.3:15 “nitaweka uadui kati yako (shetani) na huyo
mwanamke, na kati ya uzao wako na wake, huo atakuponda kichwa, nawe utamgonga
kisigino”. Na haya maneno ni ya kinabii ambayo Kwa tafsiri ya
neno “kichwa”ni utawala na “kugonga kisigino” ni majaribu, mateso au taabu
Ukiangalia
vizuri…mwanaume hajahusishwa kwenye huo mpango, bali ni mwanamke peke yake; Kwani
MUNGU anasema, “nitaweka uadui kati yako (shetani) na huyo mwanamke”.
Kwahiyo ni kwa uzao wa mwanamke tuu bila ya kuhusisha mwanaume. Na kwa njia hii
lazima mwanamke awe bikira.
Lakini
hata kisayansi yai pekee haliwezi kutunga mimba bila ya Sperm cell. Kwa njia hii pia hata yai
halikuhusishwa kutunga mimba. Kwahiyo mwanamke anakuwa incubator tu;
kwa ajili ya kukuza mtoto atakae-fanywa kwenye tumbo lake kwa nguvu za MUNGU.
Na kwasababu damu ya mama na mtoto hazichangami… mtoto anaezaliwa anakua nje ya
dhambi ya asili ya urithi (sinless).
Kwa
njia hiyo mtoto anaezaliwa sio mtoto wa mwanadamu, kwani hajahusisha yai wala
mbegu ya mwanadamu. Bali kwa uwezo wa Nguvu za MUNGU, mwili unafanyika kwenye
tumbo la mwanamke, na mwanamke anakua incubator kwa huyo mtoto. Na kwasababu ni
MUNGU ndiye aliefanya hivyo… basi mtoto anaezaliwa anaitwa “Mwana wa MUNGU”.
Hata MUNGU alisibitisha akasema “Huyu
ni Mwanangu mpendwa, ambaye ninapendezwa sana naye” mathayo.3:17’’
na tazama, sauti kutoka mbinguni ikisema,
Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye.’’ Mtu kuzaliwa na bikra ndio ishara ambayo
hakuna nabii au mtume kutoka dini yoyote aliyeishi hapa duniani alienayo. Nabii
Isaya alitabiri; “Bwana mwenyewe atawapa ishara: Bikira
atachukua mimba, naye atamzaa mwana”
Sasa
kwakuwa dhambi iliingia ulimwenguni kupitia kwa mtu mmoja (Adam), na mauti
ikawafikia watu wote, kwa sababu kwa njia ya urithi wote wametenda dhambi;
Vivyo hivyo kwa kupitia mtu mwingine mmoja, ambaye yupo kama Adam kabla ya
dhambi watu wote wanasamehewa dhambi zao na kupata uzima wa milele. (Warumi.8:12-21)
Kama
vile dhambi ilivyoingia kwa Mwana wa MUNGU mmoja yaani Adam (Adam hakutokana
na muunganiko egg na sperm cell), hatimae watu wote wa egg+sperm cell
wakawa na dhambi na mauti… basi tena kwa kupitia mwana mwingine wa MUNGU
yaani YESU, dhambi inaondolewa kwa hao watu wote na hivyo uzima wa milele (luka.3:23-38)
INAKUWAJE
YESU MWENYE HAKI ASULUBIWE?
Kwamaana
imeandikwa “Mtu mwenye haki huokolewa
kutoka katika taabu, nayo huja kwa waovu badala yake” (Mithali.11:8). Wote
tunajua kua Kitendo cha mtu mwenye haki kuamua kupoteza kitu chake cha thamani
kwa kupenda, kwa ajili ya kumuokoa yule asie na haki huitwa “sacrifice”.
Sasa sheria hiyo inatimizwa hivi; Huyu mtu
mwenye haki (YESU), asiye na dhambi na ambae hawezi kufa kwasababu yuko nje ya
dhambi ya Adam… anaitoa haki yake kwa hiari kwenda kwetu, tena
alitupatia baraka zake, na kupokea unajisi, na laana zetu zote. Kwani kwenye
torati imeandikwa “amelaaniwa yeye aangikwae juu ya mti” Na baada ya kua
najisi, Roho wa MUNGU akamuacha hadi yeye akalia “MUNGU wangu MUNGU wangu
mbona umeniacha?” kwa mabadilishano hayo… waovu (wengi) wakawa wenye
haki, na mmoja mwenye haki akawa mwovu. Kwahiyo Watu (wengi) wenye haki
huokolewa kutoka katika taabu (kusulubiwa/mauti), nayo hiyo taabu huja kwa
mwovu mmoja (YESU) badala yao.
Mwandishi: IBRAHIM
NZUNDA 0754 210 627
Hakuna maoni
Chapisha Maoni