Header Ads

MFUMO NA UTAMADUNI WA MAISHA YA KILA SIKU YA KIKRISTO (CHRISTIAN CULTURE)



 
1.NENO LA MUNGU
Kwa mteule yeyote anatakiwa kusoma neno la msalaba kila siku na kulitafakari kila mda ili azidi kutenda mema 
WAKOLOSAI 3:16 Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu. 
Pia WAEFESO 6:17 Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu;

Kuna faida nyingi katika kutunza NENO moyoni mwako nazo ni:-
a. KUJIEPUSHA NA DHAMBI:- ukilitunza neno liitakusaidia kujua kipi kinaruhusiwa kufanya na kipi hakiruhussiwi kufanya ili kumfurahisha muumba wako na pia litakufanya kushindana na shetani na kumshinda kwa maana ukitumia neno point utakayotoa itakuwa na pumzi ya BWANA ZABURI 119:11 Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi.

b. KUJUA BARAKA ZAKO ZILIPO:-ukisoma biblia na kuzitafuta ahdi za bwana utagundua vitu vyote ambavyo bwana ameahidi kutupa viko katika neno lake alilotupa na ndiko Baraka zilikofichwa kwa hiyo unapoweka neno lake kwa wingi ndipo unapojua nini cha kuomba kwa mda huo na kwa kazi uliyofanya ZABURI1:1-

c. KUMJUA MUNGU:- MUNGU haonekani wala hakuna mwanadam anayeweza kumuona mungu na akabaki huru lakini kaelezewa katika neno lake takatifu na ppia akatoa roho wake mtakatifu ili kila aaminiye kwa maana nyingine kusikia neno lake na kukubali kupitia neno hili nitashika sharia zako. Na kwakuwa sharia za BWANA zipo katika biblia takatifu kila ashikaye neno ndiye atakayemjua MUNGU kwa kupitia roho wake mtakatifu

d. KUSUKUMIA MAOMBI:- maranyingi tumekiwa tukiomba hasa tunapokuwa na shida huwa tunatumia neno aliloahidi ni vizuri ten asana maana bwana anaposema leteni hoja zenye zenye nguvu inamaana maombi yetu yawe yale ambayo akiyasikia ajue kuwa huyu mtu anahtaji kweli au pale anaposema njooni tusemezane (ISAYA 1:18) 
bila neno lake huwezi kusemezana na mungu kwa sababu anapoongea huwa anatukumbusha kile alichokisema kwa mananbii wake zamani na hayo maneno yapo katika maandiko matakatifu hata ukisoma mafundisho ya yesu alitumia sana neno la manabii na mitume kufundisha
e. KUKUZA HEKIMA YA KIMUNGU NDANI YAKO:-WAEBRANIA 4:12 maana neno la mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.

2.MAOMBI.
Ni mawasiliano na mungu wako na hufanywa kwa ajili ya kupeleka shida(tatizo) lako,shukrani au kumsifu. Kuna aina za maombi yafuatayo:-

a. MAOMBI YA KUMSIFU MUNGU:- mungu wetu hushuka katikati ya sifa hili huonyesha  kuwa mungu wetu anapenda kusifiwa kwa ajili hiyo mtu anaweza kufanya maombi ya kumsifu tu mungu 1NYAKATI 29:10-13

b. MAOMBI YA SHUKRANI:-watu wengi huwa tunategemea pindi tukitoa kitu kumpa  mwingine au kutenda kitu kwa ajili ya mwingine huwa tunapenda na tunajisikia vizuri pindi mtu akirudi kushukuru kwa maana ya kiundani zaidi ni kwamba tunafanya akili zetu kujua kuwa bila mimi hilo jambo lingekuwa halijafika na huuwatunajisikia vibaya pindi ambapo mtu anashindwa kukushukuru kwa jambo ambalo nimefanya kwaajili yake ndio maana huwa tunafundishwa kushukuru tokea tukiwa watoto wadogo ili tukue katika njia hiyo. Je MUNGU wetu si zaidi ukimshukuru anajisikia vizuri(be proud of you) na utamfanya atende vizuri zaidi WAFILIPI4:6,WAKOLOSAI 3:15

c. MAOMBI YA KUTUBU:-mtu anapookoka au baada ya kuanguka katika tamaa za dunia hii anapojirudi anatakiwa kutubu makosa yake kwa kinywa chake mwenyewe na wengine pia huwa tunavunja sharia kwa kutojua au kwa kufaham na ROHO anaposhuhudia ndani yetu pamoja na sisi kwamba ni watakatifu au tunahitaji kutubu mfano mwepesi ni mtu aliyeokoka ambaye hata ukimuuliza kama ameokoka anaweza kukataa kwasababu roho inakosa hadhi ya kuwa mlokole ndipo kipindi hiki mtu anapotakiwa kurudi kutengeneza na BWANA MUNGU wake na maombi atakayofanya ni maombi ya kutubu ZABURI 51:1-15 WAKOLOSAI2:18

d. MAOMBI YA UHITAJI:- moja ya sehemu ambayo kanisa huomba kwa bidii ni kwenye mahitaji yao hasa ya kimwili lakini wnasahau kuwa kukua kwa karama na huduma zao ni muhimu zao kwamaana mtakatifu anatakiwa kufanikiwa kama roho yake ifanikiwavyo 2YOHANA1:2 pia hata MITHALI 3:5-8 bado kwenye msitari wa 7&8 kaonyesha uwiano kati ya kumcha BWANA na kufanikiwa kimwili na BWANA MUNGU yupo anasubiri kusikiliza mahitaji yakokupitia maombi ya uhitaji YEREMIA 33:3

e. MAOMBI YA KUWAOMBEA WATU WENGINE:- ni eneo jingine ambalo sehemu a. kubwa limesahauliwa saana hata tukiamua kuomba tunawaombea tu wale wa karibu yetu na siwatakatifu wote WAEFESO 6:18 na jinsi ya kufanya namna hii ya maombi ipo imeelezwa vizuri kwenye kitabu cha 1TIMOTHEO2:1-10

Aina zake:

  • Kwa watu unaowafaham 
  • Kwa watu usiowafaham
Faida za kuwaombea wengine
  • Kubarikiwa
  • Kufanya wengine wasimame
  • Kupata kile ulichoombea kwa mwingine kabla ya yeye
f. MAOMBI YA KUKOMBOA:-haya ni maombi ambayo tunayafanya katika kusaidia watu  wengine kutoka kwenye vifungo vyao vinaweza kuwa vya magonjwa MATHAYO 10:8 au kufunga kwenye maswala ya nchi au kufungua lolote kama vita. magonjwa ya milipuko MATHAYO18:18 kwa maana MUNGU amekupa mamlaka hayo kwa wateule wake yeremia 1:10

3. MAHUSIANO NA WATU WA KARIBU YAKO

a. KUWA MTAKATIFU
b. KUBARIKIWA
c. KUKUZA IMANI


d. KUJADILI NENO 1WAKORINTHO14:26 Basi, ndugu, imekuwaje? Mkutanapo pamoja, kila mmoja ana zaburi, ana fundisho, ana ufunuo, ana lugha, ana tafsiri. Mambo yote na yatendeke kwa kusudi la kujenga.

e. KUONYANA KATIKA NJIA YA BWANA:- Hii inawapasa wote wale walitajao jina la MUNGU mmoja wao akienda kinyume inapaswa kumuonya ili amrudie BWANA sasa kama hamna mahusiano mazuri utamuonyaje?? WAKOLOSAI 1:2

f. KUPIMWA MAWAZO YAKO NA MATENDO YAKO
:-MATHAYO 5:16 Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.

g. KUMTANGAZA MUNGU:- 1PETRO 2:9 Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;

h. KUONYESHA UPENDO WA KRISTO KWA WATU WENGINE:
WARUMI 12:9-21
 9 Pendo na lisiwe na unafiki lichukieni lililo ovu, mkiambatana na lililo jema.
 10 Kwa pendo la udugu, mpendane ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu;
 11 kwa bidii, si walegevu; mkiwa na juhudi katika roho zenu; mkimtumikia Bwana;
 12 kwa tumaini, mkifurahi; katika dhiki, mkisubiri; katika kusali, mkidumu;
 13 kwa mahitaji ya watakatifu, mkifuata ukarimu; katika kukaribisha wageni mkijitahidi.
 14 Wabarikini wanaowaudhi; barikini, wala msilaani.
 15 Furahini pamoja nao wafurahio; lieni pamoja nao waliao.
 16 Mpatane nia zenu ninyi kwa ninyi. Msinie yaliyo makuu, lakini mkubali kushughulishwa na mambo manyonge. Msiwe watu wa kujivunia akili.
 17 Msimlipe mtu ovu kwa ovu. Angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote.
 18 Kama yamkini, kwa upande wenu, mkae katika amani na watu wote.
 19 Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana.
 20 Lakini, Adui yako akiwa na njaa, mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe; maana ufanyapo hivyo, utampalia makaa ya moto kichwani pake.
 21 Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema.
Naam mpenzi msomaji,tumeona kwa sehemu utamaduni halisi na mfumo wa maisha ya kila siku ya mkristo yaani mtu yeyote yule aliyeamua kumpa YESU KRISTO maisha yake na moyo wake na kuamua kuishi kwa kufuata njia zake!
Je,wewe ni mkristo? umempa YESU maisha yako na moyo wako? kama bado fanya hivyo sasa ili uone uzuri wa maisha ya kuishi kuongozwa na yeye na kuenenda kwa kuufuata mfumo wake
ikiwa una swali lolote au maoni usisite kuwasiliana nasi!
MUNGU AKUBARIKI. 

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.