Header Ads

NGUVU ILIYOMO KWENYE MAOMBI(..mwendelezo)

IMANI YAKO JUU YA HUO ULIMWENGU.
Kila mtu anahitaji kuaminiwaau kuwafanya wengine kuwa na imani juu yake. Inaweza kuwa juu ya jambo Fulani analo weza kulifanya kwa usahihi. Watu huhitaji kuaminiwa na watu wanawaowazunguka ili:-
  1.        Aweze kufanya kitu pasi na kuingiliwa kimaamuzi
  2.       Amani ya kufanya kile anachowaza juu ya hao wamwaminio pasi na kuomba ruhusa.
  3.          Kuwa na amani juu ya hao wamwaminio.
  4.       Kuelezea kile alichofanya juu ya hao watu pasi na hofu ya kuwa inawezekana kukosea.

Mtu akiaminiwa anaweza kufanya vizuri kuliko akifanya huku anahofia kukosea. Kwasababu mtu akiaminiwa huwa anatumia kipaji chake cha ndani ambacho si rahisi kukiona bila kumpa nafasi na uhuru wa mawazo hapo ndipo imani juu ya huyo inatakiwa kuonekana. Imani huanza kidogo kidogo na baadaye hukua kutokana na matendo au faida anazopata kutoka kwa aamaniye.


Siyo ulimwengu wa nyama hata ulimwengu wa roho nao uko vivyo hivyo ndiomaana ukisoma Luka 17:6 Bwana akasema, Kama mngekuwa na imani (trust and confidence in GOD) kiasi cha chembe ya haradali, mngeuambia mkuyu (mulberry tree) huu, Ng'oka, ukapandwe baharini, nao ungewatii. Hata MUNGU mwenyewe ili afanye kazi kwako inatakiwa imani yako kumwelekea yeye iwepo na imani huwa haina shaka (kusita-sita) ndani. waebrania 10:38 Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; Naye akisita-sita, roho yangu haina furaha naye.

Kwa hiyo  Imani ni hakika ya mambo yatarajiwayo na nibayana ya mambo yasiyoonekana  waebrania 11:1. imani hujengwa na mda mwingine huharibiwa pia hubomolewa. Kwahiyo imani nikama kitu ambacho kinanguvu juu ya mtu yuda 1:20 Bali ninyi, wapenzi, mkijijenga juu ya imani yenu iliyo takatifu sana…. Iman Humjenga mtu kwa mitazamo, kiutendaji na kimazungumzo maana imani ya mtu ndio huujaza moyo wa mtu na kiujazacho moyo ndicho mtu hukitoa au hukisema. yakobo 2:26 Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa.

Imani hukua baada ya jambo ambalo lilikuwa ni tatizo kwa mtu/watu kutatuliwa kwa mfano imani ya watu wa karibu na YESU ilikuwa baada ya watu kumuona anatatua matatizo yao yanayowazunguka mfano. Kutoa pepo, kuponywa wagonjwa na kufufua wafu kwa kipindi hicho hakukuwa na watu wa kufanya hivyo. Ndiomaana mtu anafikia kutaka neno tu kwa YESU kwamaana kwa imani yake alijua hata akisema neno tu kitafanyika mathayo 15:25. 

Ili imani ikue inahitaji kuanzishwa au kujengwa. Imani hujengwa juu msingi nayo misingi ambayo imani imejengwa imetofautiana na ndizo hutofautisha kuamini kwetu. Kwamaana kuna imani juu msingi ambao ni kristo, waganga wa kienyeji, wachawi, mizimu, juu ya watu,juu ya kitu asichokijua. Imani inaweza kupimwa ndio maana mtu husema imani yangu ni ndogo juu ya hiki kitu.bas kama ndiyo hivyo bassi amini nami kuwa kipimo cha iamni kipo nacho ni AMANI. Imani hujengwa juu ya misingi bali vifuatavyo huisimamisha na kuikuza imani yako. Navyo ni elimu,mazingira, uzoefu juu ya jambo Fulani, utamaduni n.k . 

MWANDISHI: MICHAEL BASA 0765279698 au+255 789 799 199

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.