Header Ads

NGUVU ILIYOMO KWENYE MAOMBI(..mwendelezo)

  
USHIKAJI WAKO WA MAAGIZO YA HUO ULIMWENGU.
Kama tulivyokwisha tazama kwenye MUUNGANO WAKO NA HUO ULIMWENGU KWA KILA SIKU tuliona kuna maagizo ya kila ulimwengu ambayo yanaujenga huo ulimwengu na kwa mtu anayeutumikia lazima ayashike hayo maagizo ili ukue katika huo ulimwengu unaotumika kwahiyo mtu yeyote anayepewa masharti ya ulimwengu inapaswa ayashike bila kuyatafutia sababu kwa ulimwengu wa ROHO maagizo yake yamegawanyka sehemu mbili nazo ni  ‘’ten bible commandments (sheria kumi za MUNGU’’ and ‘’bible instructions(maagizo)’’ sheria kumi alipewa musa pale mlima Sinai bali maagizo ya MUNGU yalikuja kwa mdomo wa nabii,kuhani na waonyaji mbalimbali waliomo kwenye biblia. Maagizo yote yanakuja ili kuikamilisha ile sheria iliyopewa musa ndio maana YESU hakuja kuitangua sheria bali kuitimiliza sheria ya musa kwamaana nyingine hakuja kuifuta ile sheria waliyoachiwa na musa bali kuielezea kwanini MUNGU BABA alitoa zile sharia kwa kipindi kile  na maana kamili ni  nini na mambo yapi amabyo kwa mdomo wa musa  au yoshua au suleimani waliyapokea bali sasa siyo maagizo tena ya kuyashika bali kwenda kwa jinsi mpya ambayo mungu anaitazamia kwao Mathayo19:8 Akawaambia, Musa, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu; lakini tangu mwanzo haikuwa hivi. Marko 10: 5-6 Yesu akawaambia, Kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu aliwaandikia amri hii. Lakini tangu mwanzo wa kuumbwa ulimwengu, aliwafanya mume na mke. Ukisoma utaona kuwa alichokuwa akikisema yesu hakikuwa kwenye amri kumi bali ilikuwa ni ruhusa ya kumwacha mke. Bali tokea mwanzo haikuwa hivyo bali kwa ugumu wa mioyo yenu ndio maana mkapewa hiyo sheria. Hapa yesu anathibitisha kuwa kabisa kwa kipindi cha musa ilikuwa ni halali. Bali sasa kwenye utimilifu wa sheria agizo ni kutoachana. Hapo ndio unaweza sema kuwa sheria ya bwana haibadiliki na maagizo yake alikuja kutimilizwa na yesu kristo kwa kumuacha ROHO mtakatifu kama chombo pekee cha kukupa kile ambacho yesu hakukisema kwa kipindi hicho na baadhi ya mambo ambayo MUNGU aliyatoa au kuyasema kwa ufupi. Unapoenda kwenye madhabahu ya MUNGU wako maagizo yake anayaangalia kujua ukaribu wako nayeye. Chukuliana namimi huu mfano kwenye biblia imeandikwa waziwazi kuwa kitu pekee cha kukufanya umuone MUNGU ni utakatifu bali njia ya kumfikia MUNGU ni yesu kristo.n kwahapo hata kama ukiwa na yesu kwa vipimo vyote kama huna utakatifu huwezi kumuona MUNGU lakini pia ukiwa na utakatifu ukawa huna yesu wewe huwezi kumfikia MUNGU. Hiyo haipo kwenye amri kumi bali ipo kwenye maagizo.
MWANDISHI: MICHAEL BASA 0765279698/ +255 789 799 199

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.