NGUVU ILIYOMO KWENYE MAOMBI(..mwendelezo)
MUUNGANO WAKO NA HUO ULIMWENGU KWA
KILA SIKU.
Muungano wako na ulimwengu unaotumika
ni muhimu sana kama unataka maombi yako yajibiwe haraka. Maana kukaa kwa mda
mrefu huku ukiwa umeungwa kiroho (spiritually connected) bila kujali nini
kinakukabili kwenye ulimwengu wa nyama inamaana kubwa sana.
Hebu tazama tumekuwa wadhaifu kutii
baadhi ya sheria za kimungu kwasababu muda mrefu tunakuwa tumeungwa na
mihangaiko ya dunia hii. Malaika hawawezi kusumbuka kushika sheria za kimungu
kwasababu ni sehemu ya maisha yao. Kwa hiyo hawawezi kuuona ugumu maana
asilimia mia moja wako wameungwa na ulimwengu mwingine.
Mwanadamu mwili wake ni sehemu ya
dunia nao uko umeungwa na dunia, na hii ndiyo maana kama dunia ilivyo kinyume
na mapenzi ya mungu ndivyo ilivyo kwa mwili wa mwanadamu. Ndio maana unaoshwa
na kafara ili kuutoa kwenye maunganisho na dunia hii, na kuunga na ulimwengu
mwingine wa kiroho.
Tazama yesu msalabani alifanyika kafara
kwa ajili ya dhambi ikaliayo mwili wako
na kuielemea roho yako kushika maagizo ya mungu muumba wako. Kama ukisoma
kwenye UTATU WA MWANADAMU utaelewa zaidi ninachokisema hapa kwa ufupi.
Ukisoma kwenye biblia YESU alimwambia
mtu mmoja kuwa ukitaka kunifuata jikane kwanza mwenyewe kisha unifuate. Kwamaana
nyingine achana na mahangaiko ya dunia hii kisha ujitoe kwaajili ya BWANA MUNGU
WAKO. Maana bila kukataa kuwa na mawazo
mengine (double minded, spiritually you will never grow to extent that the Holy
Ghost needs you to reach). Kiroho hauwezi kukua sana kwa kiwango ambacho ROHO MTAKATIFU
anataka wewe ufikie .
Basi kama ndiyo hivyo tunatakiwa
kupenda kuwa mbele za mungu wetu muda wote. Maana kuwa mbele za Bwana au kukaa
kwenye madhabahu yake kwa muda mrefu unakuwa umeunganishwa kiroho na madhabahu
ile na akili yako, roho yako na mwili wako kwa umoja wao vinakuwa mbele za Bwana.
Hii ndiyo njia ya kuomba mbele ya Bwana inayotakiwa kama ilivyoandikwa kwenye
mathayo 22:37.
Mwili unapaswa kunyenyekea mbele za
BWANA, maana unakuwa unaonesha ishara ya utii kwenye mamlaka nyingine. Pia ni
niya ya kuonesha utii wa kiroho, kwa maana ya kupondeka kwa roho huhesabika kwa
matendo ya mwili isaya 66:2.
Basi kama ndivyo hivyo mwili wako
ulio hekalu la ROHO na utiishwe chini ya madhabahu ya BWANA kama ROHO mwenyewe
alivyoutiisha mwili wa KRISTO; hata mauti na ndipo wokovu ukaja. Hivyo hata
kwako fanya nawewe utaona kama neema za bwana hazitakuzukia.
Roho yatakiwa kushika au kukumbuka
maagizo na kulia mbele za bwana huku ukijitahidi sana kuufanya mwili ushike sheria
za Bwana muda wote. Na nafsi yako na ijae mamlaka ya Bwana Mungu juu ya mwili
wako. Na bwana wa mbinguni atakuwa nawe wala hatakuacha kama alivyokuwa na
mtumishi wake YESU KRISTO.
Wiki ijayo tutaangalie moja kati ya zile zilizosalia. MUNGU muumba mbingu na nchi akubariki sana
Mwandishi: MICHAEL BASA 0765 279 698 , +255 789 799 199
Hakuna maoni
Chapisha Maoni