Header Ads

NGUVU ILIYOMO KWENYE MAOMBI (mwendelezo/continuing)

SADAKA AU KAFARA UNAYOTOA KWENYE HUO ULIMWENGU.
Nakukumbusha kidogo kwenye somo letu la utangulizi kuhusu hili somo la "nguvu iliyomo kwenye maombi, kwamba tunaangalia maombi juu ufalme wa giza au nuru kwa watu unaowamiliki (wanaotumika).

Ili mtu aenende katika maombi ya ufalme wa roho kuna vitu vingi huhesabiwa kama sadaka(sacrifice) kwa Yule anayemuabudu, nazo zipo aina nyingi na zimetofautiana kwa uzito wake, na sadaka unayotoa ndio inayokufanya uzame kiasi gani kwenye huo ulimwengu. 

kiujumla (bila kujali ni kabla au baada ya Kristo), kuna sadaka kama za 1)mazao 2)fedha, dhahabu, shaba, 3)damu  4)nyimbo za kusifu, n.k.  kwa hizo sadaka ndipo uunganishwo wa kiroho hutokea bila kujali unamtumikia mungu yupi awe mungu mti , mungu kinyago, mungu allah au mungu yehova. 

kwamfano; Wale wa ulimwengu wa giza wanatoa sadaka zao kwenye madhabahu waliyoichagua, lakini pia na wale wa NURU wanafanya vivyo hivyo. Sadaka za mazao hutolewa kama shukrani kwa mungu wako baada ya kufanya kitu ulichokipenda au wakati unataka kufanya jambo fulani ambalo halihitaji nguvu kubwa ili litokee. 

Kuna mda sadaka hutumika kama kiunganisho cha baraka za ardhi na mtu katika ulimwengu wa roho. Maana ardhi ni chanzo cha vyote villivyopo ardhini, na maji ni chanzo cha uhai wote uliopo majini. 

kwenye mwanzo 4:3  imeandikwa "ikawa hatimaye Kaini akaleta mazao ya ardhi, sadaka kwa Bwana".Sasa ukitumia sadaka kama za unga hukufanya baraka zilizopo kwenye ardhi zikupate kwa haraka kuliko ukitumia fedha au damu ndio maana hata wana wa Israel walisisitizwa kutoa sadaka kwa MUNGU kwenye madhabahu maana alitaka kuwabariki kila watakapoiendea ardhi kwa kutafuta Baraka zao. 

Kwa upande wa fedha huwa inatumika kama shukrani baaada ya ulimwengu kukushuhudia na huwa inatolewa katika sehemu mbalimbali kama msaada kwa maskini, sadaka(offerings) ya madhabahuni, kutimiza matakwa ya ulimwengu au kwenye madhabahu kutoka25:1 -3 "Bwana akanena na Musa, akamwambia, Waambie wana wa Israeli kwamba wanitwalie sadaka; kila mtu ambaye moyo wake wampa kupenda mtatwaa kwake sadaka yangu. Sadaka utakayopokea mikononi mwao ni hii; dhahabu, na fedha, na shaba"

Mfano kwa mganga wa kienyeji huwa wanatoa hela ili kusoma uchumi wako na kuunganisha nyota yako na madhabahu ya huyo mganga. Ndio maana hutaka hata kama ni sarafu ili ikae kwenye ungo wake ambayo ndiyo madhabahu yake. 

Kwa upande wa sadaka ya damu, hutumika kwa agano(covenant) kwa ajili ya kuwa moja ya viumbe watiifu wa huo ulimwengu kutoka22:20 Mtu atakayemchinjia sadaka mungu ye yote, isipokuwa ni yeye Bwana peke yake, na angamizwe kabisa. pia  kutoka29:36 Kila siku utamtoa ng'ombe wa sadaka ya dhambi kwa ajili ya upatanisho; nawe utaisafisha hiyo madhabahu, hapo utakapofanya upatanisho kwa ajili ya hiyo madhabahu; nawe utaitia mafuta, ili kuitakasa.

Kinachotokea pindi mtu akiweka maagano inamaana anaweka uhai tofauti ulio ndani ya huyo kiumbe ili damu yake inapodai au kulia kwenye mahabahu, ilie kwa kutaja jina lako. Kwa hiyo jina lako litabaki pale linatamkwa na huo uhai wa kwenye hiyo damu. kama vile kuhusu damu ya Habili Mungu alivyosema "Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi" na tena kuhusu Damu ya Yesu akasema "Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya Habili"  (mwanzo 4:9-10, ebr `12:24)

Huo uhai  utaendelea kulia kwaajili yako mpaka huo uhai utakapokoma kuwa ndani ya hiyo damu. Damu  inaweza kuwa ya mnyama au ndege inategemea na ukubwa wa agano. Kadiri agano linavyokuwa kubwa ndivyo ukubwa wa kitu cha kumwaga damu unavyohitajika. Mfano;mtu aliyetoa damu ya kondoo ni tofauti aliyetoa damu ya kuku hata ikiwa ni kwenye madhabahu moja. Na damu ya mwisho kwa kuwa na thamani kubwa ni damu ya mwanadamu kwa maana yenyewe ina-uungu ndani yake lakini huwa haina nguvu ya kuwa sawa na MUNGU mwenyewe kwasababu ya dhambi. (ndiyo maana ilibidi Yesu azaliwe akiwa ametengwa mbali za dhambi tulizolirithi kwa adamu, ili awe kwetu dhabihu yenye Nguvu, isiyo na mawaa/dosari)

Kwa hiyo ukiwa kwenye madhabahu yako uliyochagua kwaajili ya kumwabudia mungu wako angalia ni nini unataka kutoa kwenye huo ulimwengu je sadaka inatakiwa au haitakiwi na kama inatakiwa ni kubwa kiasi na kwa uzito upi??

.
Wiki ijayo tutaangalie moja kati ya zile zilizosalia MUNGU muumba mbingu na nchi akubariki sana
Mwandishi: MICHAEL BASA 0765 279 698,+255 789 799 199

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.