Header Ads

NGUVU ILIYOMO KWENYE MAOMBI( UTANGULIZI)

BASAMINISTRY
Maombi kwa wengi huwa ni kuongea na MUNGU kama ilivyoandikwa wafilipi 4:6 Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. lakini maombi kwa kiingereza huwa yamegawanyika sehemu mbili moja ni prayers naya pili ni requests. Kwa Kiswahili zote zinamaana ya maombi lakini request inaweza kuwa kuomba kwa mwanadam ili kutimiza uhitaji wako bali prayer ni kupeleka uhitaji wako kwa ulimwengu mwingine(ulimwengu wa roho) tofauti na huu unaoishi(ulimwengu wa mwili). Kwenye hili somo tutaongelea maombi ya ulimwengu wa roho ambao umegawanyika sehemu mbili nazo ni ufalme wa giza na ulimwengu wa nuru. Ulimwengu wa giza ndio una waombaji  kama wachawi, waganga wa kienyeji, wapiga ramli, wachanja chale, wezi,waabudu shetani au mizimu, freemason,  wazinzi wengine wenye matendo yasiyompendeza MUNGU. Na  ulimwengu wa nuru unawaombaji wake ambao wameitwa kwa jina la BWANA na wametiwa (kujazwa) roho wake yohana 14: 12 Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba.
 13 Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana.
 14 Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya. Hao wote hufanya maombi ili kufanikiwa katika shughuli zao au mahitaji yao. Ili kupeleka maombi lazima kuwe na madhabahu ambayo huchaguliwa na mtu mwenyewe ili kuongea na kiongoozi wa ulimwengu unaoutumikia. Na kila ulimwengu unamashariti yake ambayo huwa yamepingana na ulimwengu mwingine  waefeso:5 Maana neno hili mnalijua hakika, ya kwamba hakuna mwasherati wala mchafu wala mwenye tamaa, ndiye mwabudu sanamu, aliye na urithi katika ufalme wa Kristo na Mungu.
 6 Mtu asiwadanganye kwa maneno yasiyo na maana; kwa kuwa kwa sababu ya hayo hasira ya Mungu huwajia wana wa uasi.. Ili kuipata nguvu ya kutenda au kuumba kile anachotaka huwa ni kuongea juu madhabahu ili kiongozi wako wa ulimwengu wa roho akusaidie kutimiza kusudi lako. Lakini kaa ukijua kuwa mtu ana asili ya kiMUNGU ndani yake ambayo neno lake ndio huumba zaburi148: 5 Na vilisifu jina la Bwana, Kwa maana aliamuru, vikaumbwa.. Kwa hiyo kuomba huwa ni kutoa maagizo katika ulimwengu wa roho nini unataka kifanyike katika ulimwengu wako wa mwili kwa maana hata MUNGU mwenyewe alifanya hivyo. Kwa hiyo maombi ni siyo kwamba MUNGU ndio anafanya bali huwa ni kutoa maagizo katika ulimwengu wa roho kuwa unataka nini kifanyike kwenye ulimwengu wako unaoishi. Haraka ya kufanyika huambatana na:-
  1. Mwenendo wako katika huo ulimwengu unaopelekamaombi yako.(bofya link)
  2. Muungano wako na huo ulimwengu kwakila siku.(bofya link)
  3. Ushikaji wako wa maagizo ya huoulimwengu.(bofya link)
  4. Sadaka au kafara unayotoa kwenye huo ulimwengu.(bofya link)
  5.  Imani yako juu ya huo ulimwengu(bofya link) 
Watu wengi hatujibiwi maombi yetukwa wakati kwasababu hizo hapo juu tunashindwa kuzifikia katika maisha yetu ya kawaida. Nataka uelewe kuwa hizo sababu hapo juu inatakiwa uviishi au kwa maana nyingine viwe ni utamaduni wa maisha ya kila siku.


 mwandishi: MICHAEL BASA 0765 279 698, +255 789 799 199

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.