TUJUE KUUWEZA MWILI
Mtu ni roho inayomiliki
nafsi. Na mtu huyu akiwekwa ndani ya nyumba ya udongo yaani mwili anakuwa nafsi
hai. (mwanzo 2:7). Binadamu nae yupo
katika utatu yaani roho, nafsi na mwili. Kama ilivyoandikwa katika
1wathesalonike 5:23 “Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi nafsi zenu
na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili”(UTATUWA MWANADAM PITIA HAPA)
Yaani kama vile mwili
unavyomiliki "kichwa" vivyo
hivyo roho nayo inamiliki
"nafsi". Kama vile kichwa
chako na mwili vyote ni of the physical... vivyohivyo nafsi na roho vyote ni
vya kiroho (ndio maana mtu akifa hajisahau yeye ni nani ingawa anaiacha
"brain" yake kaburini).. (angalia luka.16:19-31)
Kwahiyo MWILI NI JUMBA
LILOTENGENEZWA KWA UDONGO ili KUTUNZA
PUMZI YA UHAI (roho yako). Ndio maana mtu akifa maana yake ni kwamba roho yake
inakuwa imeachana na mwili. Hivyo ukiomba mtu afufuke inamaana unairudisha roho
yake katika mwili wake. Kama ilivyoandikwa “mwili pasipo roho umekufa (yakobo.2:26)”
Na kwakuwa mtu ni roho
na sio mwili. Kinachoitwa “Mwana wa Mungu” sio mwili bali ni roho yako wewe. Na
kwasababu roho yako haina asili ya kutenda dhambi imeandikwa “mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa
sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu
amezaliwa kutokana na Mungu (1yoh 3:9)”
Lakini kumbuka kuwa
binadamu anazaliwa akiwa na asili ya dhambi katika roho na mwili wake. Sasa mtu
anapookoka mwili wake huchukuliwa na kusulubiwa pamoja na Yesu pale msalabani.
Kama ilivyoandikwa “hao walio wa Kristo
Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake(gala.5:24)”.
Sasa pamoja na kwamba
mwili unakuwa umesulibiwa lakini asili yake ya dhambi haitolewi katika mwili
ila unakuwa umesulubiwa tu pamoja na Yesu pale msalabani. Ndio maana bado miili
hii inazeeka na inakufa kwasabu ya ile asili ya dhambi ndani yake iletayo
mauti. Imeandikwa “nia ya mwili ni mauti;
bali nia ya roho ni uzima na amani. Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya
Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii”war8:6-7
Kwa jinsi hii tunaona kuwa mwili waweza
kutenda dhambi na hauwezi kutii sheria kwani bado unayo asili ya dhambi. Na kwa muda huohuo roho yako haitaki kutenda
dhambi kwani haiwezi kutenda dhambi kwasababu haina asili ya dhambi. Kama
ilivyoandikwa “mwili hutamani ukishindana na roho, na roho kushindana na mwili;
kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka (gal.5:17)” na tena
imeandikwa “Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za
mwili zipiganazo na roho.(1pet.2:11)
Kwa hiyo tamaa za mwili
na matendo ya kimwili yako tofauti na ya
roho yako ndani yako
JE
MATENDO YA MWILI NI YAPI SASA?
WAGALATIA 5:
19 Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu,
ufisadi,
20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi,
wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,
21 husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana
na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba
watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.
Na kwa upande wa roho
ni
WAGALATIA 5:
Na matendo/tunda la
roho ni lipi?
22 Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema,
fadhili, uaminifu,
23 upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna
sheria.
JE KUNA UHUSIANO WOWOTE
KATI YA MWILI NA KUMTUMIKIA MUNGU????
NDIYO UPO
1WAKORINTHO 6:19; Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la
Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu
wenyewe
Kwa hiyo mwili ni
hekalu la ROHO mtakatifu tuliyepewa na MUNGU lkn matendo ya mwili hayapo katika
kumpendeza MUNGU
WARUMI 8:7.
8
Wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu.
Kumbe
ili kumpendeza MUNGU inabidi mtu
asiiufuate mwili je njia zipi za kutoufuta mwili
KUMKIRI
YESU
WAGALATIA 5; 24
WARUMI 8:10 Na Kristo akiwa ndani yenu, mwili wenu
umekufa kwa sababu ya dhambi; bali roho yenu i hai, kwa sababu ya haki.
KUISHI
KWA KUIFUATA roho/ROHO
WARUMI 8: 6 Kwa kuwa nia ya mwili ni mauti; bali nia ya
roho ni uzima na amani.
9
Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali
mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si
wake.
WAGALATIA 5;25 Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho.
KUTOUFUATA
MWILI
WARUMI 8:5 Kwa maana wale waufuatao mwili huyafikiri
mambo ya mwili; bali wale waifuatao roho huyafikiri mambo ya roho.
1PETRO1: 24 Maana, Mwili wote ni kama majani, Na fahari
yake yote ni kama ua la majani. Majani hukauka na ua lake huanguka;
2PETRO2: 9 basi, Bwana ajua kuwaokoa watauwa na
majaribu, na kuwaweka wasio haki katika hali ya adhabu hata siku ya hukumu; 10
na hasa wale waufuatao mwili katika tamaa ya mambo machafu. na kudharau
mamlaka.
KUJUA
DHUMUNI LA MUNGU JUU YA MWANADAM
1WATHESALONIKE4: 3 Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa
kwenu, mwepukane na uasherati;
1WAKORINTHO 6: 20 maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi,
mtukuzeni Mungu katika miili yenu.
KUJUA
KUUWEZA MWILI
1WATHESALONIKE 4: 4 kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake
katika utakatifu na heshima; 5 si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa
wasiomjua Mungu.
Mwandishi; Michael BASA 0765 279 698, +255 789 799 199
Mhariri; IBRAHIM J. NZUNDA 0754 210 627
Hakuna maoni
Chapisha Maoni