NGUVU ILIYOMO KWENYE MAOMBI(..mwendelezo)
MWENENDO WAKO KATIKA HUO ULIMWENGU UNAOPELEKA MAOMBI YAKO.
Kila ufalme unajengwa
kwa mila desturi ,masharti na sheria ili uweze kusimama. Ulimwengu wa giza una-miiko
yake, pia na ulimwengu wa nuru pia una-miiko yake katika ufanyaji kazi na hivyo
ndivyo ulivyojengwa. Ili uenende kwenye ulimwengu kuna masharti ya kiujumla au
sharia, na pia kuna masharti ya jamii moja na jamii nyingine.
Mfano jamii ya waganga
wa kienyeji iko tofauti na jamii ya wachawi ingawa ni wamoja. Lakini kazi zao
zinawafanya wawe tofauti kimiiko ya kiutendaji. Vivyo hivyo mitume na waalim na
wao pia wanamiiko ya kiutendaji, haimaniishi kuwa kazi zake mtume haziwezi
kufanana na mwalimu au mchawi hawezi kufanana na mganga, hapana hata kidogo.
Kwa maana ufanano wa
kazi unajengwa na nguvu inayoshuka kwenye madhabahu wanayotumia kwenye maombi.
Wasipoweka miiko huo ufalme utafitinika. Kama ilivyoandikwa “Kila ufalme
ukifitinika juu ya nafsi yake, hufanyika ukiwa; tena mji au nyumba yo yote
ikifitinika juu ya nafsi yake, haitasimama. Na Shetani akimtoa Shetani, amefitinika
juu ya nafsi yake; basi ufalme wake utasimamaje?” (mathayo12: 24-27).
Kwahiyo ili uwe na
nguvu kwenye ulimwengu wa roho inatakiwa kushika vizuri masharti ya huo ufalme
unaotumika. Mfano ulimwengu wa NURU
ukitumia madhabahu ya walokole unakuta kuna kunena kwa lugha. Mtu
anayenena kwa lugha hawezi kufanana kwa nguvu wakati wa kuomba na ambaye
haneni kwa lugha.
Au mfano mwingine
mchawi hapandi cheo pasi na kuvuka baadhi ya mitihani na pia kuna vyeo kupewa
kwenye ulimwengu wa giza mpaka uwe wamekuamini sana. Halikadhallika na kwenye
taasisi zetu za kawaida kwenye ulimwengu wa nyama kawaida.
Kwa ulimwengu wa nuru kwenye
madhabahu ya wakristo sheria ziko wazi kwenye biblia na msharti yako ndani pia.
Ukitaka uwe na nguvu zaidi mda wa kuomba inatakiwa uombe mda mrefu tena kwa
mpangilio na siyo kuomba tu. Pia omba kwa kunukuu vifungu vya biblia kwenye
aina ya maombi yako kama tulivyokishwa jifunza kwenye CHRISTIAN CULTURE.
kwa maana kutoka kwenye
utangulizi wa hili somo tuliona kwamba kuna prayers na requests sasa
unapopeleka “requests” hakikisha ziko kwenye mpangilio(definite) ili zikubaliwe
la sivyo utakuwa unapayuka(speaking in vain). Soma AMPLIFIED BIBLE philipians
4:6 na mathew 6:7
Pia inatakiwa uache
uovu wote, kama ilivyoandikwa “Kila
alitajaye jina la Bwana na auache uovu” (2Timotheo 2:19). Kwamaana uovu hautakiwi
kutajwa kwako waefeso 5:3 Lakini uasherati usitajwe kwenu kamwe, wala uchafu wo
wote wa kutamani, kama iwastahilivyo watakatifu;. Pia anza kufanya kazi ya
MUNGU(JEHOVA YIRE). Kama tulivyokwisha ona kwenye MILANGO YA KUVUKA KABLA HUJAFA.
Hapo ndipo nguvu zako
na mwenendo wako kwenye huu ulimwengu
utakapokubaliwa na kuwa mwenye nguvu na maombi yako ndivyo yatakavyokuwa
yanajibiwa upesi zaidi. Maana “tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme
wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka”( mathayo11:12).
Wiki ijayo tutaangalie moja kati ya zile
zilizosalia. MUNGU muumba mbingu na nchi akubariki sana
Mwandishi: MICHAEL BASA 0765 279 698 , +255 789 799 199
Hakuna maoni
Chapisha Maoni