NGUVU ILIYOMO KWENYE MAOMBI(..mwendelezo)
Kama tulivyokwisha
tazama kwenye MUUNGANO WAKO NA HUO ULIMWENGU KWA KILA SIKU tuliona kuna maagizo
ya kila ulimwengu ambayo yanaujenga huo ulimwengu na kwa mtu anayeutumikia
lazima ayashike hayo maagizo ili ukue katika huo ulimwengu unaotumika kwahiyo
mtu yeyote anayepewa masharti ya ulimwengu inapaswa ayashike bila kuyatafutia
sababu kwa ulimwengu wa ROHO maagizo yake yamegawanyka sehemu mbili nazo
ni ‘’ten bible commandments (sheria kumi
za MUNGU’’ and ‘’bible instructions(maagizo)’’ sheria kumi alipewa musa pale
mlima Sinai bali maagizo ya MUNGU yalikuja kwa mdomo wa nabii,kuhani na
waonyaji mbalimbali waliomo kwenye biblia. Maagizo yote yanakuja ili
kuikamilisha ile sheria iliyopewa musa ndio maana YESU hakuja kuitangua sheria
bali kuitimiliza sheria ya musa kwamaana nyingine hakuja kuifuta ile sheria
waliyoachiwa na musa bali kuielezea kwanini MUNGU BABA alitoa zile sharia kwa
kipindi kile na maana kamili ni nini na mambo yapi amabyo kwa mdomo wa
musa au yoshua au suleimani waliyapokea
bali sasa siyo maagizo tena ya kuyashika bali kwenda kwa jinsi mpya ambayo
mungu anaitazamia kwao Mathayo19:8 Akawaambia,
Musa, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu;
lakini tangu mwanzo haikuwa hivi. Marko 10: 5-6 Yesu akawaambia, Kwa sababu ya
ugumu wa mioyo yenu aliwaandikia amri hii. Lakini tangu mwanzo wa kuumbwa
ulimwengu, aliwafanya mume na mke. Ukisoma utaona kuwa alichokuwa akikisema
yesu hakikuwa kwenye amri kumi bali ilikuwa ni ruhusa ya kumwacha mke. Bali
tokea mwanzo haikuwa hivyo bali kwa ugumu wa mioyo yenu ndio maana mkapewa hiyo
sheria. Hapa yesu anathibitisha kuwa kabisa kwa kipindi cha musa ilikuwa ni
halali. Bali sasa kwenye utimilifu wa sheria agizo ni kutoachana. Hapo ndio
unaweza sema kuwa sheria ya bwana haibadiliki na maagizo yake alikuja
kutimilizwa na yesu kristo kwa kumuacha ROHO mtakatifu kama chombo pekee cha
kukupa kile ambacho yesu hakukisema kwa kipindi hicho na baadhi ya mambo ambayo
MUNGU aliyatoa au kuyasema kwa ufupi. Unapoenda kwenye madhabahu ya MUNGU wako
maagizo yake anayaangalia kujua ukaribu wako nayeye. Chukuliana namimi huu
mfano kwenye biblia imeandikwa waziwazi kuwa kitu pekee cha kukufanya umuone
MUNGU ni utakatifu bali njia ya kumfikia MUNGU ni yesu kristo.n kwahapo hata
kama ukiwa na yesu kwa vipimo vyote kama huna utakatifu huwezi kumuona MUNGU
lakini pia ukiwa na utakatifu ukawa huna yesu wewe huwezi kumfikia MUNGU. Hiyo haipo
kwenye amri kumi bali ipo kwenye maagizo.
MWANDISHI: MICHAEL BASA 0765279698/ +255 789 799 199
Hakuna maoni
Chapisha Maoni