Header Ads

MWONGO NI NANI?

Wengi wanasema; “haijalishi kama wewe ni dini gani, au unafuata njia gani… Mungu ni mmoja… kwahiyo kama unamwabudu Mungu halisi na unatenda mambo mema huko uliko… siku ya mwisho hautahukumiwa”. Je, hii ni kweli au uongo?

Imeandikwa “Je, mwongo ni nani? Mwongo ni mtu yule asemaye kwamba Yesu si Kristo. Mtu wa namna hiyo ndiye MPINGA KRISTO, yaani, yeye humkana Baba na Mwana. Hakuna yeyote amkanaye Mwana aliye na Baba.” (1yohana.2:22-23). Pia Kristo anasema “Mimi ndimi njia na kweli na uzima. Mtu hawezi kuja kwa Baba isipokuwa kwa kupitia Kwangu” (Yohana.14:6). Kwahiyo njia ni moja tu, na imani ni moja tu, yaani Yesu basi. Njia nyingine zote ni za upotevuni (njia pana).

Hii pia ni kwa kila mtu anaetumia majina mengine ili kupata msamaha wa dhambi kutoka kwa Mungu. Yesu anasema “Nanyi mkiomba lo lote kwa Jina Langu, hilo nitalifanya, ili Baba apate kutukuzwa katika Mwana. Kama mkiniomba lo lote kwa Jina Langu nitalifanya” (Yohana.14:13-14, 15:16, 16:23-28) Pia imesisitizwa kuwa; “kama mtu yeyote akitenda dhambi, tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo Mwenye haki. Yeye ndiye dhabihu ya upatanisho kwa ajili ya dhambi zetu, wala si kwa ajili ya dhambi zetu tu, bali pia kwa ajili ya dhambi za ulimwengu wote” (1yohana.2:1-2).

 Hatuna dhabihu wala mwenye haki zaidi ya Yesu kwahiyo nikisema “Mt. Petro au Maria utuombee sisi wakosefu” badala ya “Yesu utuombee sisi wakosefu”; ninakuwa nimepotea kabisa na hiyo ni ibada ya mizimu, kwani wapagani wote hutegemea wafu badala ya Yesu aliye hai.(Isaya.8:19). Sisi ni makuhani(ufunuo.1.5-6), na Kristo ndiye Kuhani wetu Mkuu(waebrania.5.1-10). Sasa ni upotevu ulioje kwa kuhani kumwacha kuhani Mkuu aliye hai na kwenda kwa wafu?

  Pia wote wanaosema “hakuna wokovu duniani” wanatenda dhambi ya kumfanya Mungu mwongo na kwamba hakumleta mwanae ili atuokoe (1yohana.5:9-10). Imeandikwa “tazama,wakati uliokubalika ndiyo sasa; tazama siku ya wokovu ni sasa” (2korintho.6:2) Vile vile; Dini au dhehebu au mtu yeyote anaehubiri injili nyingine zaidi ya injili ya Kristo, yeye amelaaniwa kabisa (wagalatia.1:8-9, 1korintho.16:22).

Ndio maana Mungu alisema “Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Yeyote aaminiye na kubatizwa ataokoka. Lakini ye yote asiyeamini atahukumiwa.”(Marko.16:15). Kwahiyo kila mwanfunzi wa Kristo lazima ahubiri injili hata kwa matendo inatosha… la sivyo mtu huyo anachangia kupoteza wenzake.
Mwandishi: IBRAHIM J. NZUNDA 0754 210 627

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.