BASA VISION
Moja ya mijadala au maswali magum kwa kipindi hiki au kwa wakristo wote ni kwanini shetani anawasumbua?. Nami katika njozi ya usiku wa kuamkia tarehe 28 Aug 2017 Bwana alinionesha. Kwanza siku mbili kabla moyo wangu ulikuwa na kiu ya kitu ambacho sikijui nikaona labda tamaa ya kumtumikia Bwana imekuwa kubwa kuliko jinsi ambavyo naweza kuhimili. Nikaendelea na mienendo yangu ya kawaida ya kila siku huku nikijichunga nisije mtenda Bwana dhambi. Jumapili ya tarehe 27/8/2017 nilipokuwa kanisani nikawa kama amani inaisha kwa kuwa nilihitaji kujua kitu ambacho sijui ni nin?{yaani unaahisi unahitaji kuwa na maarifa fulani ambayo huna lakini mtu akikuuliza maarifa gani huwezi kusema maana hata akili yako haijui moyo unataka nini?}. Amani ikaendelea kupungua mpaka nikawa natamani kuondoka kanisani kuacha ibada nikawa mtu wa mawazo. Nikaamua kuingia kwenye maombi nikanena kwa lugha sikujua hata naomba nini?.Roho alininyima maana yake baada ya mda kule kukosa amani kukapungua kidogo nikaendelea na ibada mpaka mwisho.
Usiku ndipo Bwana akanionesha katika maono nilikuwa natembea sehem ambayo kuna kisima na bwawa upande mwingine namimi nilikuwa napita katikati yake huku nikiwaza jinsi ya kumtumikia Bwana kwa uaminifu huko niendako?. Kwamaana Bwana alikuwa amenituma lakini sehem siijui, nilipokuwa katika mawazo yale mara mbingu zikafunguka nikamuona Roho mtakatifu akishuka kwa mfano wa hua. Yesu akasema na mimi akaniambia kuna kanisa hapa nataka ukafundishe ndipo uendelee na safari. Nikakubali nikafunguliwa macho nikaona kanisa ndani ya Yesu mwenyewe nililokuwa natakiwa kwenda kulifundisha nalo lilikuwa na watu wengi sana.
Walikuwa wakisifu mbele za Bwana hakika walipendeza sana. Nilipokubali ndani ya moyo wangu mda ule ule Roho alinichukua nikajiona naiacha ardhi na kuingia ndani ya lile kanisa madhabahuni. Waumini wakakaa kimya kila mtu mahali pake ndipo nikafungua biblia nifundishe moja ya masomo ninayoyafaham. Nilipoanza tu kufundisha Roho akaniambia siyo somo hilo tazama huku uwaelezee yote utakayoyaona nami nitakuwa nawewe. Nikaona tazama binti mmoja mlokole aliyekuwa na njaa ya kumtumkia sana Mungu na Mungu akambariki kwa KARAMA ya ualim na huduma ya uimbaji watu wote wakampenda sana kwa jinsi alivyojitoa kwa Bwana. Shetani alijaribu maranyingi sana kumtoa kwa Yesu kwa kumzuia kuimba akashindwa, kwa kumtenga na marafiki, kumkosanisha kanisani hata hakujali walipomkataa kanisani yeye alihudumia wa nje ya kanisa. Watu wakampenda sana kwa nyimbo zake na mafundisho yake mazuri hata Yesu alimpenda pia. Kikao kikafanyika kuzimu kuhusu ufalme wao kutetereka sana kupitia kwa huyu binti wa Yesu. Shetani akaja na mpango mpya ambao angetumia miaka miwili kufikia kumuangusha kabisa na kumtoa nje ya Yesu. Nao mpango ulikuwa katika hatua zifuatazo:-
1. Kuanza kucheza na mawazo yake ya kila siku kuhakikisha mawazo yake yanaanza kuwa na chembe za uovu kwa mbali kwa vitu vifuatavyo:
- MWILI WAKE MWENYEWE:- atakapofikria kuhusu nguo za kuvaa kwaajili ya huduma cha kwanza kabisaa ni kumpa wazo la kwamba hizo nguo ni za zamani pia hazimpendezi kwasasa na atakapojiuliza avae nguo gani?. Picha ya kwanza kumletea ni zile za watu waliopotea na bado wanafanya huduma au bado wako kanisani.
- MARAFIKI:-kuwasogeza marafiki wengi waliopotea kwake wakanisani na wasio wakanisani karibu yake ili pindi akiwaza uovu wao ndio wamshauri uovu ule kwamba hauna madhara kwake kwa maana hata wao bado wanatumiwa na Roho au wanasfari ya kwenda mbinguni
- MAVAZI:- kuanza kumpa mawazo ya kuvaa nusu uchi na kwa nia ya kupendeza maana huduma siyo ma nguo marefu au mapana sana lakini ni kupendeza kwanza kisha huduma itavutia watu wengi.
- AKILI YAKE:- ipunguze kuwaza kuhusu Mungu sana au ikiwaza isiwe katika uzito ule wa mwanzo kwa kumpa kitu mbadala cha kuwaza kila anapotaka kufikria kuhusu Mungu.
2. Baada ya hivyo kufanikiwa kinachofuta ni kumpa roho ya kukosa mda kwa maana atapunguza maombi na tamaa ya kuhudumia kwa bidii au kupanda viwango iondoke.
3. Wazo la mume limjie kwa kasi ya ajabu ambayo mwili wake na akili zake zishindwe kuhimili.. Ambapo iwe rahisi kumpa mtu ambaye atashindwa kufanya jukum la Bwana au kufikia viwango pia iwe rahisi kuingilia ndoa na kila kitu cha ndani ya ndoa.
4. Kumuacha ahudum huku akiona kila kitu kipo sawa hata asipopotea yeye lakini kazi za ufalme wa giza zitaendelea kuwepo na kukua na kushamiri sana duniani kote.
Baada ya kile kikao nikaona kundi kubwa likimvamia la pepo wachafu kila pepo alitoa wazo ambalo anahisi linaweza kufanikiwa. Baada ya mda mrefu sana hatimae yule binti akaweka mguu mmoja nje ya msitari wa wokovu na nguvu za giza hata bega lake kushoto lilikuwa na alama ya uovu. Mwili wake uliosalia ulikuwa ndani ya Yesu ukipokea baraka zote na kila kitu lakini kuenea kwa ufalme wa Mungu kupitia yeye ilikuwa tayari imekuwa ngumu.
MICHAEL BASA +255765 279 698
Hakuna maoni
Chapisha Maoni