JE NI MIMI au NI BWANA??.
Kuna kipindi mkanganyiko hutokea sana pindi tu linapokuja suala la mipaka ya Bwana kutenda na wewe mwenyewe kutenda. Kuna mtu mmoja aliwahi kusema nanukuu " usiufiche uzembe au uvivu wako kwenye maombi ukahisi utafanikiwa bali fanya kazi kwa bidii Bwana atakutana nawewe huko huko kazini". Pia kuna mwingine aliwahi kusema kwa kiingereza "hard work beats talent when talent doesn't work hard". Lakini biblia inaseema "Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu." katika wafilipi 4:6. Swali la kujiuliza je kuna mipaka ipi ya kimwili na kiMungu katika utendaji wangu yaani ya kimwili na Roho katika uenendaji wangu wa kila siku?. Kabla ya kujibu hili swali tuangalie kwanza andiko moja nalo ni kutoka wagalatia 5:25 "Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho.". Kuna vitu vifuatavyo katika kuishi katika mwili huku ukifanya ya rohoni navyo ni:-
- Katika mtazamo wa kwenda mbinguni au kuingia Yerusalem mpya inatakiwa uwe kwanza akilini mwako kila mahali unapotembea au kukaa au hata kulala. Kwamaana mshitaki yuko kila mda anaandaa hati yako ya mashitaka nawewe uwe katika hali ya kuvunja shitaka shitaka lolote litakaloletwa{1ptero 5:8}. Hapo cha kwanza ni kujazwa ROHO mtakatifu na kumsikiliza yeye tu kama mwalim, msahuri, mwelekezi wako, mtoa dira wako, mpangaji wa mambo yako yote, msemaji wa mwisho juu yako na rafiki bora kwako.warumi 8:9 pia yoha 14:26.
- Jizoeze kuwa mkazi wa mbinguni kwa kujifunza mambo ya ufalme na kujizoeza katika mambo ya ufalme kila mara. 1Petero 2:11 "Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho.". Wewe ni msafiri tu usitake kuupata ulimwengu kwanza bali tunza kwanza taji ufunuo 3:11, marko 8:36. Safari ya mbinguni iwe ni ya uhakika maishani mwako mwote.
- Acha kuishi kwa mazoea kila siku Mungu anataka kusema na wewe kwa jinsi nyingine na tofauti sana kutoka ile ya jana. Usimzoee Mungu kwa maana ukiona umemzoea sana Mungu jua tu umeshaanguka. Kwamaana mda si mrefu ulishapingana na Roho mtakatifu. Kuna watu wamekariri jinsi moja tu ya kusema na Mungu jua kwamba safari yako haina uhakika sana kwa maana hata shetani anaweza kutumia na akakupoteza na Mungu akatumia njia nyingine ukashindwa kumuelewa kuwa ni YEYE anayesema nawewe. Penda kuona Mungu akijifunua kivingine kila siku katika maisha yako ya kila siku.
- Penda sana kujihoji uhusiano wako wa siku kati yako na ROHO kwa maana unaweza kutana na ishu ngumu au hali ambayo akili yako ikashindwa kutafasiri kwa jinsi ambavyo Mungu anapenda au anataka uelewe. Ukijihoji atakuambia na kukuelekeza kisha unatubu mambo yanakuwa sawia kabisaa.
Baada ya kuanza kutenda hivyo vinne utakuja kugundua kwamba roho yako inaanza kuwa na nguvu sana kuliko mwili wako. Hapo ndipo unakuwa na uwezo wa kuongea na Mungu bila wasiwasi na kuishi kwa imani unakuwa mtu wa mfano kwa jamii yote katika imani. Ukiwa mtu huyo hauhitaji unabii wala nabii akuambie Mungu anasema nini juu yako kwamaana kabla hujaja hapo ulipo tayari kashasema nawewe. Kama ndivyo hivyoo basi mtendaji ni wewe na Muongozaji{mwamuzi} ni Bwana na nyie wawili mnakuwa umoja kwamaana mnaishi ndani ya jumba moja ambalo ni mwili huo ulio nao na nyie mmenakuwa mmoja. Na hapo ndipo kila ufanyalo litafanikiwa kwamaana Mungu anakuwa anataka akutumie sana. Kwahiyo hawezi kuruhusu upoteze mda kwenye mambo yasiyokuwa ya ufalme wake. Kila utakapofanya swali kubwa litakuwa JE NI MIMI au NI BWANA?. Jibu ni Bwana ndani yako kwa nje unaonekana wewe kwa ndani anaonekana Bwana. Ndipo hata mtu akikushukuru haujitukuzi kwamaana ile shukrani ikiingia ndani inamkuta Bwana kila sehem na Yeye ndiye anayeipokea.
Mungu akubariki sana mtumishi kwa kusoma mpaka mwisho tumia namba yangu hapo chini kunipa mrejesho na pia kutoa maoni yako. Pia nataka nisikie kutoka kwako na kwa facebook page usiache ku LIKE
By MICHAEL BASA +255 765 279 698
Hakuna maoni
Chapisha Maoni