Header Ads

NUHU WA KIZAZI HIKI

   Ukisoma kitabu cha mwanzo 5:29 mpaka mwanzo 10:32 utakuta habari za mtu mmoja anaitwa NUHU. Huyu mwanaume aliishi katika kizazi kilichokuwa katika hali ya uovu wakupindukia. Watu walilala na wanyama, walikula nyama za watu, walikuwa ni watu wakaidi wasiotii, wasiosamehe,wauaji. Watu walipoona uovu kuwa ni kitu cha kawaida Nuhu alipata kibali machoni pa Bwana. Kama wewe unampenda Mungu kweli utajiuliza ilikuwaje Mungu akamhifadhi katika uovu kiasi kile?. Je unamkumbuka Lutu aliyepata amani machoni pa Bwana pindi moto uliposhuka na kuangamiza sodoma na gomora?. Uovu ulipozoeleka machoni pa wanadam na kuonekana kitu cha kawaida yeye moyo wake ulimwelekea Bwana. 
   Walipoonekana hawana akili na kuitwa wajinga au wasio enenda na wakati kwa wakati huo lakini mioyoni mwao cha kwanza kilikuwa ni kumpendeza Bwana. Unaweza usinielewe haraka kiasi hiki twende pamoja kwenye kitabu cha mathayo 24:36-39 {Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake.Kwa maana kama vile ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. Kwa kuwa kama vile siku zile zilizokuwa kabla ya Gharika watu walivyokuwa wakila, na kunywa, wakioa na kuolewa, hata siku ile aliyoingia Nuhu katika safina, wasitambue, hata Gharika ikaja, ikawachukua wote, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.}. Hata kuja kwake mwana wa adam kwa mara ya pili maisha yatakuwa yanaendelea tu kama kawaida. Kanisa litaendelea kama kawaida, manbii wauongo nao watakuwepo kama kawaida, wachagua wokovu nao watakuwepo, wang'ang'ania kanisa kuliko Yesu nao wataongezeka maana ndiko ukristo unakoelekea. Yesu hajaleta ulokole, usabato, uroma n.k. Lakini alileta uzima wa milele{Yohana 17:3 Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.}. Tazama leo kuna wokovu wa aina mbili mmoja wa zamani na mwingine wakisasa. Wengine wameanza kuchagua maandiko ya kwenye wokovu wakisasa. 
   Ukimkemea anajenga chuki nawewe hata anaweza kutengeneza somo kwaajili yako tu je huyo Roho anayewapa amani ni kweli ndiyo huyu ninayemtumikia mimi?. Kwamaana kuna wengine mioyo yao ndio waalim wao hata wamemzimisha Roho mtakatifu kasome tena Yeremia 17:9, Yakobo 1:22b na 1Wathesalonike 5:19. Kuna kanisa moja Mungu aliniweka niabudu hapo nikakuta ibada zao ni kusemana baada ya kukosekana nikaazimu moyoni mwangu kulihama ili nikatafute kanisa jingine. Bwana akaniambia hapo ndipo nilipokupangia uabudu. Ikawa ni mtihani kwangu katika wokovu wakuanza kuwatoa watu huko kwenye mafundisho yakusemana na kuja kwenye mafundisho yakutiana moyo na kujengana katika mwili wa Kristo pia msamaha mioyoni mwao. 
   Nilikuwa naongea na mmoja mmoja kisha nikaongea na kundi zima kama Bwana alivyonipa neema na kibali pia. Lakini pia kuna mtu Roho alinishuhudia nikamwambie kuhusu mavazi yake ayabadilishe ili roho{nguvu} ya uasherati isimsumbue tena au imuache. Alikuwa ameokoka akaniambia kuwa hicho ninachomwambia ni wokovu wa zamani sana. Lakini baada ya mazungumzo marefu na kujitahidi kujibu maswali yake akaniambia baadaye atafikria kuhusu kubadili mavazi yake. Lakini haijalishi kuwa kuna wokovu wa zamani na wakisasa lakini sikia nikuambie kuwa {HAIJALISHI DHAMBI WANAFANYA WENGI KIASI GANI?, AU IMEZOELEKA KIASI GANI?, AU WANAFANYA WATU UNAOWAAMINI KIASI GANI LAKINI DHAMBI ITABAKI DHAMBI  SIKU ZOTE NA ITAKUFANYA USIENDE MBINGUNI?}. Mungu wetu ni mtakatifu na mtakatifu pekee ndio atamuona yeye na ndie atakayepata ruhusa ya kuingia kwenye makazi yake. 
itaendelea........
MICHAEL BASA 0765279698

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.