NANI ASIMAME AKEMEE ???.
Tazama tena kwa mabinti zetu nguo walizovaa
makahaba miaka 1970 leo ndio zinavaliwa na waimbaji wa makanisa yetu . Mtoto wa mchungaji
akifanya dhambi ni nani wa kukemea huo uasi. Sikia mbinguni hatuingii kwa vyeo
vyetu ndani ya kanisa wala huduma zetu ndani ya kanisa hakika nakuambia BASA
MINISTRY haitanipeleka mbinguni bali UTAKATIFU ndio utanipa kibali cha kukutana
na Bwana wangu. Waumini wameanza kuchagua mafundisho ya kushika wakati biblia ni
moja wewe usiye na akili ni nani aliye kuroga wainjilisti wamesema wazi na
kukemea wazi mbele zako nawewe ukainua kimdomo chako kumsema vibaya pole sana. Kwamaana
wafanya vita na Bwana mwenyewe nawe hutaokoka kwa mawazo yako maovu wala
kujihesabia haki kwako.
Ni nani kati ya mabinti zetu aliyetaka kununua kimini
akaammua kufunga na kuomba kwaajili ya kupata maono na ruhusa ya Roho mtakatifu
na baada ya kupata jibu akashirikisha mwingine zaidi kwenye kuomba maono kuwa
Roho analionaje hilo vazi?. Vijana wa kanisa nao hawako nyuma kwa msemo wa modo
zao nguo inabana kila sehem. Mwanzo wanawake walivaa kuamsha hisia{lust} za
wanaume je kijana wa kiume unaamsha hisia za nani?. Je unajua madhara ya
kutumika kwenye kitu ambacho mwanzilishi{author} wake siyo Mungu?.
Nakuambia acha kuiga
iga vitu ovyo tamani kwanza kujazwa Roho mtakatifu kisha ipeleke injili kwa
jinsi ulivyoitwa tamaa za mwili huwezi kuzikamilisha milele mpenzi wangu
nikupendaye na pia shetani ni mdanganyifu sana wewe jisifu kwa Amani yenye
mapengo mapengo na roho yako mwenyewe imechoka na haiwezi kumuona MUNGU.
By MICHAEL BASA 0765 279 698
Hakuna maoni
Chapisha Maoni