Header Ads

UNAWAZA NINI??

unawaza nini
basa jpg
    Kabla ya kitu chochote kudhihirika kwenye ulimwengu wa mwili kiutendaji huanza kama wazo ndani ya moyo au akili ya mtu mwenyewe. Kwa wazo lako  unaweza kuanzisha vita ya kiroho au kujisogeza karibu zaidi na MUNGU wako. Mwanzo 4:7 inasema ........dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde. Angalia kwenye hayo maandishi mekundu utajua kitu tofauti kidogo. Dhambi iko inakuotea mlangoni???? jiulize tena kivipi dhambi ikuvizie mlangoni kwako. Lakini pia inakutamani!!!! kivipi haya yanawezekana kutoka kinywani mwa MUNGU mwenyewe. Kama wewe ni mchunguzaji wa maandiko huenda na wewe ilikutatiza sana au kiasi chake.
       Twende zaburi 36:1{Kuasi kwake yule mwovu hunena moyoni mwake, Hakuna hofu ya Mungu mbele ya macho yake.}au Ezekieli 38:10. Kumbe kabla ya mtu kutenda uovu machoni  pake huja na wazo moyoni mwake likipita ndilo hulitenda bila kuwa na hofu ya Mungu kabisaa. Basi kumbe dhambi haiwi dhambi mpaka ipate kibali moyoni mwako. Usipoipa kibali kamwe wewe hauwezi kutenda dhambi kabisaa katika maisha yako yote. Jikune kichwa kidogo kisha jiulize asilimia kubwa ya mawazo unayowaza je niya ufalme upi??. 
      Soma tena zaburi 66:18 {Kama ningaliwaza maovu moyoni mwangu, Bwana asingesikia}. Swali la kujiuliza je ni Bwana hawasikii watu gani?    Yeremia11:11-17 hapa ndipo utagundua kuwa walioasi au kuiacha sharia ya Mungu ndio ambao Bwana hawasikii. Daudi anaposema Bwana asingesikia basi kwa namna moja au nyingine anakukumbusha kuwa dhambi huanzia moyoni mwa mtu. Huhesabiwa kuwa ni dhambi baada ya kupata kibali moyoni mwako mwenyewe ndio maana katika Yakobo 4:1. Imeelezea kabisa kuw vita tunavyopigana mara nyingi kwa kushindana na miili au viungo vyetu zimetokana na mawazo yetu yasiyo na kibali machoni pa Bwana. 
          Ndio maana YESU akatuonya mapema kwa kutuelekeza kuyatafakri yaliyo juu yapitayo faham zetu. Leo pia nakukumbusha usikomee kuwaza tu mazingira yako hayo yatakukatisha tamaa MUNGU haangalii mazingira wala jamii ya watu waliokuzunguka. Kwamaana hata hao hawajui Mungu anakuwazia nini? bali watasema yajazayo mioyo yao kama  mawazo yao ni maovu . Basi hata mioyo yao huwa imejaa maneno na shuhuda za kutomtukuza Bwana wala kuonesha ukuu wake hata zikikiri kuwa ni muweza wa yote lakini bado huwategemea wanadam maana mioyo yao huwa imeielekea zaidi dunia na siyo ufalme wa Mungu. Yeremia29:11 na akaambiwa asijisumbue wanasema nini juu yake kwa maana hawajui Bwana aliwazalo wala alipangalo juu yako pia  MIKA4:12. 

By Michael Basa 0765 279 698

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.