HUYU MUNGU NI BABA
Bwana wewe ni nguvu na ngome kwangu ahadi zako
ni za milele kwangu umeniinua juu ya mataifa nawe umekuwa mji wa nguvu moyoni
mwangu mataifa sikieni nanyi mkaweke ushuhuda mioyoni mwenu “Heri walio kamili njia zao, Waendao katika
sheria ya Bwana”. Tena ni “Heri wazitiio shuhuda zake, Wamtafutao kwa moyo
wote.Naam, hawakutenda ubatili, Wamekwenda katika njia zake”. Bwana Mungu wangu
anawapenda watu hao nao kamwe hawatakuwa makapi mbele za adui zao maana Bwana
yeye atawashindia vita na wao milele watakuwa washindi. Je wachamungu
wametaabika mioyoni mwao na nyongeza zimeteka ufahamu wao sikieni leo
niwakumbushe fadhili za Bwana zilizo za milele tena aliahidi hatakuacha enyi
mtangao je hamkusoma imeandikwa “Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au
Tunywe nini? Au Tuvae nini?. Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu
Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote. Bali utafuteni kwanza
ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.”. Je hamkuamini kwa neno
la injili nalo ni hili yeye aketiye mahali palipoinuka ametuamru kuyashika
mausia yake Ili sisi tuyatii sana. Neno langu naomba kibali mbele zako Bwana nalo
ni hili “Ningependa njia zangu ziwe thabiti, Nizitii amri zako.Ndipo mimi
sitaaibika, Nikiyaangalia maagizo yako yote.Nitakushukuru kwa unyofu wa moyo,
Nikiisha kujifunza hukumu za haki yako”. Kwa maana Hakuna mtu aliyeacha nyumba,
au ndugu waume, au ndugu wake, au mama, au baba, au watoto, au mashamba, kwa
ajili ya Injili, akapata hasara bali atapewa mara mia sasa wakati huu, nyumba,
na ndugu waume, na ndugu wake, na mama, na watoto, na mashamba, pamoja na
udhia; na katika ulimwengu ujao uzima wa milele.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni