NDANI YA DINI YANGU---3
AMEMKIRI KRISTO NA KUBATIZWA KWA MAJI MENGI {bofya kwa utangulizi}
Soma marko 16:15-17 Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa. Na pia warumi 10:9-10 {Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.}. kukiri kwa kinywa chako mwenyewe hii ndio hatua ya kwanza kabisa ya kuingia kwenye dini ya UKRISTO na siyo kwa kujikuta tu ndani ya ukristo. Kuna watu wamezaliwa babazao ni wachungaji au baba zao ni wazee wa kanisa Fulani wakaona kuwa kwasababu wamekulia kwenye mafundisho basi wao niwa KRISTO. Hapana mwajidanganya tu bure nafsi zenu inatakiwa umkiri KRISTO kwa kinywa chako mwenyewe tena mbele ya watu wengine kwamba mimi nitatembea na huyu KRISTO. Ukishamkiri unamkaribisha kuwa kiongozi wa Maisha yako kwa mda wote wa kuishi kwako. Kukiri kwa kinywa kwa maana ndogo ni kwamba unakubali kuwa kuanzia sasa mimi ni mtumwa wa YESU KRISTO katika mambo yote nakubali kuwa chini yake na nitajifunza magotini pake. Mungu wake ndio Mungu wangu Roho wake ndio Roho wangu na Maisha yake ndio Maisha yangu. Hapo ndipo unasema mimi ni mkristo. Baada ya hicho kitendo kinachofuata ni kubatizwa kwa maji mengi subiri niseme kidogo hapa kwamba kubatzwa siyo ishara bali ni ukamilisho kwa mtu yeyote aliyekubali kumfuata Yesu. Mathayo 3:13-15 soma vizuri hiyo mistari utaona kuwa kwenye msitari wa 15 Yesu mwenyewe anakiri kuwa ni haki na imetupasa wote kuitimiza. Nakuonya ndungu yangu sina ugomvi na mafundisho yenu wala dhehebu lako bali kama unataka kuwa MKRISTO hakika anza kutafuta kubatizwa kwa maji mengi na usikae tu kanisani bila kubatizwa omba kwa viongozi wako ubatizwe kwa maji mengi. Hakika usipobatizwa haki ya mbingu usipoitimiliza hauwezi kuiona mbingu hata kidogo kwa maana Yesu kaagiza kwenye mathayo 6:33{Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.}. kumbuka ubatizo ni haki ya ufalme wa mbinguni na siyo kwa mujibu wa kanisa Fulani. Kwasbabu ni haki ya mbingu yule mwenye kazi ndio anatakiwa kuonesha mfano na siyo kwa mjibu wa dhehebu Fulani tu. Yohana 3:22-23{Baada ya hayo Yesu na wanafunzi wake walikwenda mpaka nchi ya Uyahudi; akashinda huko pamoja nao, akabatiza.Yohana naye alikuwa akibatiza huko Ainoni, karibu na Salimu, kwa sababu huko kulikuwa na maji tele; na watu wakamwendea, wakabatizwa.}. Tazama yohana aliyembatiza yesu alikuwa anabatiza kwenye maji tele. Sikia nikuambie kitu kimoja ndugu yangu katika KRISTO YESU ubatizo ulikuja kwa mkono wa Yohana ndio ambao biblia imeuagiza na sehem zote walipoagiza kubatiza au unapoona kubatizwa kwa maji ile siyo ishara tena bali ni agizo la ufalme wa mbingu. Ukitaka kujua kuwa ubatizo ulikuwa niwa aina moja muone towashi kwenye matendo 8:36-38. Hata pia wakati yesu anakuja kubatizwa yohana alikuwa anabatiza kwenye mto yordani. Basi kumbuka yesu anasisitiza kujifunza kutoka kwake kwenye mathayo 11:29-30 basi katika kujifunza kutoka kwa yesu hakuna cha dhehebu langu limeagiza nini wala cha mchungaji wangu wala kiongozi wa dhehebu letu alikuwa na upako sana wala sijui alikuwa ni mmoja wa mitume au kaandika nyaraka zote maana hata yeye mwenyewe alifanya kubatiza kwa maji mengi pitia hata kwenye matendo ya mitume yote utaona watu wanabatizwa kwa maji tele kila sehem na hakuna sehem biblia imesema ni ishara tu. Basi ndugu achana na roho ya udini kabisaa jifunze kutoka kwa mwanzilishi wa Imani mwenyewe ambaye ni yesu KRISTO.
Mwandishi MICHAEL BASA 0765279698/+255789799199
kama unaswali au ushauri au ombi nipigie au nitumie ujumbe mfupi{sms} kwa namba hizo utampata BASA mwenyewe na utapata vingi zaidi. Kwamaana Bwana ameniita kuwa mtumishi wako.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni