Header Ads

NDANI YA DINI YANGU

Watu wengi tuna dini zetu au kwa maana nyingine tuna mfumo wetu wa Maisha wenye miiko na sheria pia. Dini yako inaweza kuwa tofauti na ya mwingine au zikawa sawa. Kumbuka miiko ndio inayoifanya dini yako iweke watu waufanano mmoja pamoja kwa lengo moja. Ndani ya miiko yako ndipo lengo kuu huandaliwa kwaajili ya watu wote walio kwenye dini yako kutoa mda wao kwa nguvu zote ili kulifikia. Sheria ndani ya dini yako zipo kukufanya ubaki kwenye njia sahihi wakati unaenda kutimiza lengo la ndani ya dini yako. Swali siyo usahihi wa dini swali ni je bado upo kwenye njia sahihi ya kulifikia lengo la dini yako??. 
            Nataka nielezee lakini nitatumia Zaidi maandiko ya kwenye biblia maana ndiko niliko na maarifa mengi na mifano mingi. Ukisoma yakobo 1:26 Mtu akidhani ya kuwa anayo dini, wala hauzuii ulimi wake kwa hatamu, hali akijidanganya moyo wake, dini yake mtu huyo haifai. Hapa tatizo siyo mtu kuwa na dini tatizo je hiyo dini yake ndio misingi ya Maisha yake?. Je ulimi wake unaua au unaponya? Soma mithali 21:23 na mithali26:28. Utagundua kuwa kama mtu ana dini yake anatakiwa ajifunze kuwa wa haki kwenye hiyo misingi na sheria za dini yake. Kuna watu wamekuwa wakijidanganya kuwa mimi ni dini Fulani wala siyo dini ile lakini matendo yake hayatupi picha ya ile dini anayoisema. Mtu anaweza kusema mimi ni mwisilam wakati hata sura moja hajui kusoma kwa picha sasa unajiuliza huyu dini yake kwa mawazo yake ni uislam lakini kwa matendo anakataa. Mwingine anaenda mbali Zaidi kwa kusema sisi tumezaliwa kwenye uislam lakini kuswali ni ijumaa mpaka ijumaa. Je ndivyo dini yako inavyoagiza?. 
            Mwingine ni mkristo kwamaana nyingine ni mfuasi wa KRISTO swali je wewe umejifunza kwa kristo kweli mbona haujabeba msalaba wako mwenyewe?. Kama wewe una dini kweli mbona hutuambii mwisho au Taraji ya dini yako kwa matendo tujue u katika safari kweli ya kufika kwenye Taraji ya dini yako. Mtu na akasema mimi niwa Paulo na mwingine mimi niwa Petro na wote wakabaki ni wanadam tu. Je wajua unayemuabudu anataka uweje? Soma sheria zake na usizipindishe hata moja ndipo utajua kuwa mungu wa dini yako anataka nini kwako. Leo hii mtu akisimama kuonya kuna watu wanasema sisi na wewe ni dini moja lakini madhehebu tofauti. Sikiliza nikuambie kila dini iko kwenye Imani ya ibada na ya uwepo wa Mungu. Sasa je kwa mwenendo wa ulimi na matendo yako vinamwabudu bado au umekuwa unaidanganya nafsi yako kila mara?. Sikia nikuambie ndugu kusema wewe ni dini fulani halafu ukaacha baadhi ya sharia na ukaamua kufuata baadhi tu kwasababu wewe umeona ni njema machoni pako mwenyewe. 
            Ama zinakupa uhuru wakutii mambo yaliyo kinyume na hicho unachokiamini. Nasema hivi kwasababu kuna watu wako dhehebu Fulani kwasababu tu hawapendi kuambiwa uzinzi ni dhambi au mavazi yao niya kikahaba. Kwa wakristo Hakuna wokovu pasi na kumpenda YESU na kama ukimpenda Yesu inatakiwa ujikane na ushike sheria zake na uzifuate. Kwahiyo kuwa mkirsto siyo kazi ya lelemama inahitaji kujitoa kwa gharama zote kumfuata yesu. Kuna siku moja mtu mmoja aliniuliza Je BASA wewe kweli umeokoka? Nikamjibu HAPANA  unajua kwanini nilimjibu hivyo???

................................inaendelea bofya hapa kusoma...........


Mwandishi MICHAEL BASA  0765279698

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.