NDANI YA DINI YANGU ---2
Kuna siku moja mtu mmoja aliniuliza Je BASA wewe kweli umeokoka?
Nikamjibu HAPANA unajua kwanini
nilimjibu hivyo kwasababu sijafikia kwenye viwango vya wokovu ninavyovitaka na
ambavyo biblia imeagiza mtu angalau kuvifikia tu kwa mawazo ya fikra yake. Kuwa
mfuasi wa dini Fulani haishii kwenye jina wala kushiriki ibaada zao tu au
kuhudum kwenye baadhi ya mikusanyiko ya dini hiyo. Kama hushiki sheria za dini
yako hakika wewe siyo mfuasi wa hiyo dini bali ni mtu kama wasio wafuasi {KAFIRI}.
Elewa kitu kimoja kwamba kuishi Maisha halisi ya dini yako kwa kufuata sheria za dini yako na miiko yake yote huko ndiko kuwa mwana dini wa hiyo dini yako. Ukiwa ni mwisilam hakikisha masharti ya uisilam unayafuata kwa kila kitu na kuitwa HAMIS siyo sifa ya wewe kuwa mwisilam kabisaa. Kuitwa LUKA haikufanyi wewe kuwa mfuasi wa KRISTO katika Maisha yako bali kuishi kwa mjibu wa maandiko ya kitabu chako au miongozo ya viongozi wa dini yako. Kwa mkristo Kuna madhara ya kuwa Mkrisito halafu humfuati kristo. Swali lako linaweza kuwa nitajijuaje kuwa namfuata Kristo na bado nipo kwenye njia sahihi ya kumfuta Kristo?. Kwamaana kuna watu ni wa Kristo kwa majina na madhehebu yao tu lakini kwa matendo Yesu hawajui watu hao. Kuna sifa za mtu anayemfuata Kristo kweli na siyo kwa maigizo kama watu wengi wanayofanya sasa kwamaana wameacha kazi ya msalaba na kujivika udini ambao Yesu hajaagiza hata kidogo. Hakuna Roho mtakatifu ambaye atashudia ndani yako akasema wewe niwa PENTEKOSTE au wewe niwa KATOLIKI au KKKT kama umefikia hapo wewe unajidanganya nafsi yako tu bure hakika humfuati Kristo bali umevaa roho ya udini.
Kama ukiweza kusema mimi niwa Kristo na matendo yako yakakiri kuwa wewe ni waKristo huyo ndio mtu ambaye ndani yake anadini ya UKRISTO. Kuna watu unawambia wewe hivyo unavyotenda ni kinyume na maadili ya dini. Anakujibu mimi si dini yako au mimi siyo dhehebu lako je hujui kuwa wizi ni dhambi je huji kuwa uongo ni dhambi?. Je ni dini gani iliyoagiza watu wasipendane au wasichukuliane katika makosa yao. Kuna watu wengine vinywa vyao vimejaa matusi na chuki wanatukana dini za wengine mara hivi mara vile. Lakini je dini yako inasemaje kuhusu kumfanya mwingine aawe dini moja nawe au kanisa moja dhehebu moja nawe?. Pia siyo kazi nyepesi kumfanya mtu mmoja atoke dini yake ya mda mrefu aje kwenye dini yako. Kuna sifa za MKRISTO aliye mfuasi wa KRISTO kweli nazo ni:-

- AMEMKIRI KRISTO NA KUBATIZWA KWA MAJI MENGI {bofya hapa kuisoma}
- AMEJAZWA ROHO MTAKATIFU{bofya hapa kuisoma}
- AMEJIKANA KATIKA KUMFUATA KRISTO
- ANASHIKA SHERIA ZOTE PAMOJA NA SABATO ZOTE ZA BWANA
- ANADUMU NA KWELI SIKU ZOTE
- MATENDO YAKE HUMTANGAZA KRISTO{bofya hapa kuisoma }
- ULIMI WAKE UMEJAA UZIMA
- ANAIJUA KWELI NA HIYO KWELI IMEMUWEKA HURU
- HUCHUKIA DHAMBI KWA MATENDO YAKE
Tutaaanza kujadili sifa moja baada ya nyingine kadiri BWANA atakavyotupa uzima na mda pia.
MWANDISHI MICHAEL BASA 0765279698/+255789799199
Hakuna maoni
Chapisha Maoni