Header Ads

NDANI YA DINI YANGU---4

AMEJAZWA ROHO MTAKATIFU (KUSOMA UTANGULIZI BOFYA HAPA)
      Kuna Rafiki zangu wa dhehebu Fulani Roho kwao ni stori za zama za kale sana kabla ya dunia kuwepo. Huwa nacheka tu kwamaana hadithi za kizee zisizokuwa za dini ndizo zimekuwa sahihi kwao na usahihi wa neno umekuwa ni upotofu kwao. Kuna wengine pia ukiwakuta wanajiita makanisa ya kiroho sikatai maana wao wanajiona hivyo wanategemea viongozi wao kwa kila jambo hata ambalo Mungu anatakiwa kuonekana kwa uwazi kwao wenyewe wanamsubiria mchungaji wao au nabii wao. Sipingi kuwafuata maana hata mimi nina baba zangu wa kiroho lakini hawatakiwi kuchukua nafasi  ya Mungu. Yesu alitoa uhuru kwa kila mtu kujiombea nasiyo kutegemea mtu Fulani. Ndio maana kwa biblia ikasema Bwana anazichunguza nyoyo na huvijaribu viuno. Sasa wewe na huyo kiongozi hamjui kuwa mnamtenda Mungu dhambi. Je mmesahau kuwa amelaaniwa mtu yule amtegemeeaye mwanadam??. Wengine pia kuna roho kiburi na roho uhuru wamewaingia hao hata ukiwahubiria vipi hawaelewi kitu. Tena chunga unaweza kuambulia matusi yanguvu kweli au ukaishiwa kutengwa na kanisa lako. Huwa naukumbuka sana wimbo wa MUNISHI unaitwa “WANAMWABUDU NANI?”. 
      Wengine wamejazwa roho wakajihisi watamuona Mungu wakati biblia imeagiza kujazwa ROHO tena siyo ROHO tu bali awe mtakatifu ambaye anakuja kwako kwa kazi zifuatazo:-
     ➤KUKUFUNDISHA 
     KUKUONYA
     KUKUELEKEZAKUKUJULISHA MAMBO YAJAYO
     ➤KUKUFUMBULIA MAFUMBO MAKUU YA MUNGU
     ➤KUKUPA AMANI
     KUSHUHUDIA PAMOJA NA NAFSI YAKO KUWA WEWE NI MWANA WA MUNGU
     KUKUOMBEA
     KUKUONGOZA
     KUKUPA HUDUMA KWAAJILI YA UFALME
       Unapomkataa Roho mtakatifu inamaana umekataa vyote hivyo. Inakuwa ni ngumu sana kwa wewe kujua mipango ya Mungu juu yako kwa wakati huo. Pia chamaana Zaidi ya hivyo vyote soma nami warumi 8:14{Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu}. Kuwa MKRISTO kwamaana nyingine ni kuwa mwana wa MUNGU kuwa au kuwa chini ya miliki ya Mungu mwenyewe au kuonesha kuwa Mungu yupo katikati ya wanadam. Kuonesha mfano wa watu watakaoingia mbinguni na kustarehe kwa Mungu baba. Mtu hapokei Roho wa Mungu akabaki na matendo au tabia ya asili ya dhambi 1wakorintho 2:14 kwamaana mtu wa matendo ya asili bado amepotea.
        Yohana 14:16-18 {Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele;ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu.Sitawaacha ninyi yatima; naja kwenu}. Roho siyo maamuzi ya dini Fulani tu bali ni agizo la kutobaki yatima kama Yesu mwenyewe alivyoagiza kwa wanafunzi wake. Ukimpata Roho mtakatifu unaanza kukamilishwa sasa katika ukristo wako na siyo dini ile ndio wanajazwa Roho mtakatifu au watu wa jinsi hii ile pekee ndio wanatakiwa kuwa na Roho mtakatifu. Kwamaaana wote waliompokea aliwapa uweza wa kuwa wana wa Mungu hapa haijasema na lazima uwe msabato au mlokole au mkatoliki au lutherani bali ni kule kuwa Mkristo na ukampokea Roho wa Mungu basi wewe umekuwa mwana wake kweli. Kwamaana Roho wa Mungu hakai sehem chafu bali hukaa sehem safi tu. Unaweza anza jiuliza napokea Roho wa Mungu kwasasa hapa nilipo, nakutoa wasiwasi kwamba kumpokea ni rahisi sana fanya yafuatayo:-
○ Jichunguze njia zako je ni kipi ambacho unafanya lakini hakipo sawa kabisaa kibiblia anza kukiacha hicho maana huwezi kujazwa ukiwa bado unatenda dhambi, kama dhehebu lako halizingatii ubatizo wa Roho basi hamia dhehebu jingine ambalo linasisitiza kuacha dhambi na kujazwa Roho mtakatifu. Tubu dhambi zako zote kwa kumaanishan jutia dhambi zako zote ulizotenda wakati bado unahangaika kwenye dhambi na usitamani kurudi huko tena. Elewa kitu kimoja unaweza kumdanganya BASA lakini huwezi kumdaganya Mungu kwamaana yeye huichunguza mioyo ya wote wamwendeao kwa kumtaka YEYE na kama bado unawaza maovu hawezi kukusikia hata kama ukeshe unaomba na kufunga juu. BADILISHA NJIA ZAKO
○ Uwe na njaa ya kujazwa Roho mtakatifu, tamani kuwa na Roho mtakatifu toka moyoni mwako omba kwa Mungu kila siku kuwa naye. Usiache kuomba hata baada ya kujazwa kwasababu kumpata siyo kinga ya YEYE kutoondoka kwako. Kwahiyo omba kila siku aje kwako uzidi kuzama zaidi ndani yake upate mafunuo kupitia Roho mtakatifu. TAMANI KUWA NAYE KILA SIKU
○ Mtumie kila siku ili adhihirike kwa wingi zaidi kwa maana kadri unavyomtumia ndivyo unavyozidi kuimarika kiroho. Kuzama kwako kutakupa kujua zaidi alama na tafsiri za kiroho na pia ndio utaanza kufurahia kumfuata KRISTO. 
         Baada ya kujazwa Roho mtakatifu furahia kuwa ndani yake wala usiruhusu akakuondolea uwepo wake ndani yako. Kuna watu walipokea na wao wakampoteza na kipimo cha Roho mtakatifu siyo kunena kwa lugha bali ni udhihirisho wake kwako kwa matunda yake tisa ambayo ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; ukiona mtu anayo matunda ya Roho mtakatifu huyo ndio mwana kweli wa Mungu na amejazwa Roho wake kweli. Ukisoma hayo matunda hayajasema dini fulani bali yanamtaka mtu ambaye anataka kuwa mfuasi kweli wa KRISTO awe nayo. Kwamaana huyo msaidizi mwingine ndiye humtengeneza mtu kuwa hivyoo. Tunda la Roho mtakatifu inatakiwa lionekane kwa nje na siyo wewe kujitangaza kama BASA anadharau watu wengine haijalishi nitakuwa dhehebu gani wala kanisa la mchungaji nani na awe na upako kiasi gani?. Lakini bado nitakuwa sina Roho mtakatifu na siku ya mwisho makao yangu ni kwenye ziwa liwakalo moto. Basi ndugu yangu nakusihi kwa upole wake KRISTO YESU hebu tafuta ahadi yake ya Roho uwe na uzima wa milele ndani yako. Barikiwa sana

Mwandishi MICHAEL BASA 0765279698/ +255789799199

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.