MTAZAMO WANGU
Usimkosee Mungu kwa vitu vitatu naam kwa vitu vinne
hautakiwi kuikosa mbingu
- TUMBO
- MAVAZI
- UPAKO
- NDOA
1. Hakuna kitu kizuri kama kula
na kunywa mbele za Bwana maana nayo ni karama aisee {mhubiri 3:13 Tena ni karama ya Mungu kila mtu apate kula na kunywa, na kujiburudisha kwa mema katika kazi yake yote.} hata mimi napenda kula na kunywa sana na
kufurahia kila chakula na kinywaji changu. Lakini kuna kitu cha kuchunga kila
karama ina mipaka yake hata karama ya kulihudumia tumbo inamipaka yake tena
mikubwa. Mwanzo 2:16-17{Bwana Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema,
Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula,walakini matunda ya mti wa ujuzi wa
mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa
hakika}. Umepewa kula na kunywa na kufurahi lakini
yakumbuke masharti ya kula na kunywa n siyo kujiendea kama usiye na akili. Huo
mwili unaohitaji chakula inatakiwa upate nguvu na afya siyo kufa ndio maana
adam akaewa angalizo mappema kabisaa. Naamini katika biblia sheria ya kwanza
ilihusu chakula kwa mwanadam na ndio agizo la kwanza kabisaa. Kuna watu
wanahisi kila kitu ni chakula na kunywa tu huku afya zao au uzima ndani yao
unatetereka kila siku na magonjwa ya ajabu ajabu yanaongezeka. Wataalam wa afya
wanadai kuwa ulaji mbaya umefanya magonjwa yasoyoambukiza kuongezeka.
Kwenye
angalizo la kwanza lilikuwa ni kula chakula ulichoewa mwenyewe na ambacho
unauwezo wa kuamua ule nini na nini usile?. Basi tumbo hutamani kila kitu kwa
mda wote bali roho hutafuta ibada kwa kila jambo hapa nasemea mtu aliyempokea
KRISTO nasivinginevyo. Kuna watu siyo Amani ya KRISTO ndani yao bali ni mazoea
yao ndio huamua ndani yao. Ni kweli andiko lasema wazi kuleni vyote kwaajili ya
dhamiri lakini kumbuka siyo kila chakula chafaa kuliwa na mwandam na si kila
kinywaji cha chafaa kwa afya yako anza sasa kula na kunywa kwaajili ya roho
yako mwenyewe na kwaajili ya uzima wako ndani ya KRISTO. Kula kwaajili ya
kufurahia hii karama lakini uwe na KIASI katika kula kwako na kunywa kwako. Kuna
watu wamejaa ubatili kwaajili ua kula tu na kunywa. Nawaonya mapema isafisheni
mikono yenu na muzitakase nia zenu ili roho zimrudie YEYE aliye juu na yote na
juu ya vyote ni Bwana wa vyote pia na ndie aliye mmiliki wa vyote Mungu wa enzi
na miliki zote. Kwamaana wokovu wafaa sana kwake yeye aliye nao na Roho wa
ahadi afaa kwa vyote na yote pia. Kuna watu walimfuta Yesu kwasababu tu
walikula mikate waksahau kuwa hawajanywa maji ya uzima, je wewe tumbo lako limeokoka
na vyakula vya laana na makao ya kuzimu yako nje ya viuongo vyako. Mkate usikutoe
kwa Yesu kwamaana 1wakolintho 6:13 Vyakula ni kwa tumbo, na tumbo
ni kwa vyakula; lakini Mungu atavitowesha vyote viwili, tumbo na vyakula.
Lakini mwili si kwa zinaa, bali ni kwa Bwana, naye Bwana ni kwa mwili.
Utapata hasara
kama uliwekeza kwa tumbo kwamaana hakuna kitakachobaki kwako siku ya hukumu
lakini wewe basi jifariji kwa hii yohana 6:51 Mimi ndimi chakula chenye uzima
kilichoshuka kutoka mbinguni; mtu akila chakula hiki, ataishi milele. Na chakula
nitakachotoa mimi ni mwili wangu, kwa ajili ya uzima wa ulimwengu. Hakikisha tumbo
lako limejaa hiki chakula kila siku za Maisha yako
Mandishi MICHAEL BASA 0765279698
Hakuna maoni
Chapisha Maoni