NDANI YA DINI YANGU----5
MATENDO YAKE HUMTANGAZA
KRISTO{kusoma utangulizi bofya hapa}
"Usiangalie matendo yangu bali sikia nasema nini kwako au
fuata ninachosema" moja ya hoja maarufu sana kwa wakristo wengi wasiojua
kwanini wanamfuata KRISTO. Ni kweli Mungu huichunguza mioyo kama biblia
inavyosema kwenye mstari wa 1 Samuel 16:7…Bwana
haangalii kama binadamu aangaliavyo; maana wanadamu huitazama sura ya nje, bali
Bwana huutazama moyo. Subiri nikuambie kitu kimoja
ambacho unatakiwa ukielewe kutoka kwangu na si kwamwingine biblia ni kitabu
kitakatifu huwa kinachanganya kama usipoweza kufunuliwa kwa Roho mtakatifu.
Kuna wachungaji kwa kutojua maana halisi ya neno au msitari huitafasiri vibaya
na huenda nawewe ulichukua kwake.
Wengine huitafasiri kwaajili ya kuficha
udhaifu wao na hao ndio laana imekaa kwao na ndio waalim wa uongo walionenwa
ujihadhari nao mapema nakuonya pia. Kuna siku nilikuwa nafundisha nakumbuka
nikataka kutoa mfano nikaonya mapema natumia tafsiri isiyo takiwa kuitumia
kwenye kila mazingira bali ni kwa mazingira ya mfano huu tu. Sasa kama
nisingetoa hiyo kuna watu wangechukua kama ni tafsiri ya kijumla na kuna
mazingira ingepingana na wao wenyewe kutumika. Swali la msingi JE NI KWELI
MUNGU HUANGALIA MOYO TU? KAMA NDIO KWANINI NIANDIKE MATENDO? KAMA HAPANA JE HUO
MSITARI NI WAUONGO?. Nikutoe hofu kwanza kama umeshaanza kuwaza nitajibuje
kwenye hayo maswali mawili hapo juu. Kwa msitari huo hauna tatizo kabisaa kama
ukiutumia kumuonya mtu ambaye kwa nje ni msafi au unasisitiza usafi ndipo
unasema Bwana haangalii nje bali huangalia mioyo na kuvichunguza viuno yeremia
17:10{Mimi, Bwana, nauchunguza moyo, navijaribu viuno, hata kumpa kila mtu
kiasi cha njia zake, kiasi cha matunda ya matendo yake}.
Je unakumbuka kuwa
dhambi huanzia ndani ya mtu na siyo nje kama wengi wanavyodhani soma tena
mwanzo 4:7{Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani
wewe, walakini yapasa uishinde.}jiulize sasa hapo mlango ni upi?. Soma tena
ayubu{Job 38:17 Je! Umefunuliwa malango ya mauti, Au umeyaona malango ya
kuzimu?}. Uone kitu kingine kipya kabisaa ndipo ujue kuwa biblia haishii hapo
wewe unapoona kwa upeo wako wala kwa maandiko ya BASA tu. Pia maandiko siyo
ulokole na wala siyo UKRISTO kwamaana UKRISTO ni kuwa ndani ya KRISTO na
ULOKOLE ni kumiminwa ndani ya ROHO MTAKATIFU. Ukitaka kuwa MKRISTO kweli
jifunze msalabani sana na ukubali na kutii kila andiko kama lilivyo bila kusema
mtumishi fulani alisema hivi au vile. Kuna mtu mmoja alifundishwa na watu
wawili tofauti mtu wa kwanza alifundisha kutopenda kumpa mkono kila mtu na
hakuelezea kwanini na kwa mazingira gani?. Mtu wa pili akafundisha kuwapenda
wale wa nje na kuwasalimia kwa kupeana mikono na kama ni jinsia moja unaweza
kuwakumbatia kabisaa. Swali likaja kwangu sasa je amfuate nani kwamaana wote ni
wachungaji na anawaamini sana na hahisi kama kuna mmoja kasema uongo. Mimi nikacheka
kisha nikamfundisha chimbuko la mafundisho yote mawili na kwanini yapo hivyo na
kwenye ulimwengu wa roho yanachukuliwaje kisha na yeye afuate lipi?. Lakini
nilichogundua kwa huyu mtu hajazama ndani ya Roho mtakatifu vizuri ndio maana
hakuelewa ashike lipi sasa?.
Ndio maana nasema kwamba matendo yako yote
yanatakiwa yamhubiri KRISTO, watu waduniani wanaangalia porn na wewe mkristo
unaangalia halafu unataka uione mbingu sahau tu. Mungu siyo wa mzaha kiasi
hicho aisee tena pole sana. Watu wanajitesa kwa kufunga na kuomba na kukesha
wewe unakula siku 365 kwa mwaka na kulala masaa yote. Kuomba dakika tano nyingi
halafu unataka eti ufunuliwe kwenye ulimwengu wa roho sahau tu. Mtu unatembea
uchi halafu unataka Yesu aonekane kwako au ajidhihirushe labda utumie pepo
aisee. Hakika Mtu ambaye roho yake inamwabudu Mungu kweli au moyo wake unakicho
cha Bwana halafu kwa nje anachotoa ni uongo, uasherati, wizi, uuaji, chuki,
uchonganishi, ufiraji, kuchora tattoo, huombi, husomi neno, disko umo, sehem za
laana hukosi. Wasioamini wanassema kabisaa kama nawewe ukiingia mbinguni basi
mimi nitakuwa malaika {mathayo 5:20}halafu unajibu utaona Mungu anaangalia moyo
wa mtu haangalii matendo pumbavu kabisaa mwana wa laana wewe.
Wewe ndio
unafanya injili inakuwa ngumu kwa watu kuipokea na kuitii kwamaana haoni
tofauti yako wewe ambaye ni mfuasi wa KRISTO na yeye ambaye bado anaabudu
miungu mingine. Basi tuangalie matendo yako kama Mungu anayatazama kama moyo au
vyote viwili. Tito 1:16
Wanakiri ya kwamba
wanamjua Mungu, bali kwa matendo yao wanamkana; ni wenye machukizo, waasi, wala kwa kila tendo jema hawafai.
Huyo siyo mimi bali ni walaka kwa tito ambao mwandishi anaonesha kitu kidogo
kwamba kuna matendo ambayo ukiyafanya unakuwa unamkataa Mungu kabisaa. Mkirsto
mwenzangu hujui kwamba mdomo wako unaweza kuwa unamkubali Mungu kweli lakini
mwili wako unafanya ibada za miungu kila siku. Badilika wewe mkristo mwenzangu
hakikisha matendo yako yanatoa kile kilichoko ndani ya moyo wako ambacho Yesu
mwenyewe alifundisha. Hatuna kipimo kingine cha utakatifu isipokuwa matunda ya
ROHO MTAKATIFU.
Mwandishi: MICHAEL BASA 0765279698/+255789799199
Hakuna maoni
Chapisha Maoni