Header Ads

CHURCH GIRLS AND CHURCH BOYS

Siku moja nilikuwa engineering pale SUA najisomea mara akapita msichana mmoja kavaa tisheti imeandikwa church girl. Nilishangaa kwa mda kisha nikajiuliza huyu ni nani? mbona mavazi yake na mwonekano wake hayana hilo neno?. Nikagundua kuwa ni mkristo mmojawapo katika makanisa ya kikristo. Kwa mtazamo wa nje linaonekana ni neno zuri lakini kwa mtazamo wa ndani halina maana yoyote. Subiri nikuambie kitu mwana wa mungu aliye hai. Kinachotakiwa kumtangaza kristo ni matendo  yako siyo maandishi ya kwenye nguo. Kristo aliyekufa msalabani na kwakufuata maagizo yake huwa hakuna mwana kanisa fulaani kwamaana kwake sisi kwa umoja wetu ni mwili mmoja. Hautakiwi hata mara moja kuwa church girl wala church boy. Kwa maana hilo ni mojawapo la tendo la mwilini kwamaana kanisa ni hali ya kupatanishwa kwa mwili na siyo roho. Soma biblia tena uone kama kuna sehem yoyote ambayo yesu anaongelea kujazwa mwili. Bali roho yako ndio inayopaswa kukaa kwa YESU na ukijazwa ROHO kamwe hauwezi kuwa wa mwilini tena bali utakuwa mtu wa kuishinda dhambi. Tazama church boys na church girls wengi. Utaona maisha yao ya kiroho ni machanga kwa maana upendo wao hauko kwa kristo bali kwa jengo na jina la dhehebu analotumika. Lakini kristo ambaye kwa pendo lake ndio tunapaswa kuliishi na kulitangaza ni uzima wa milele tu. Na uzima wa milele ndio huu wakujue wewe Mungu mmoja wa kweli na wapekee na Yesu kristo uliyemtuma. Kuna wengine wameenda mbali zaidi kwa kuanzisha mijadala kuhusu dhehebu Fulani ni bora kuliko dhehebu Fulani. Sikiliza nikuambie huo siyo upendo wa kristo kwa maana vipimo vya ubora vipo katika maarifa ya kujua Mungu anataka nini kwa mda huo juu yako. Soma tena biblia uone kama pendo la kristo ndilo hilo unalotangaza wewe kwenye mijadala yako. Yesu alikufa msalabani kwaajili ya watu wote na siyo baadhi ya watu tu. Hakuna ubora wa dhehebu ndani ya KRISTO mwenyewe bali kuna ubora wa mtu atendaye mema ndani ya KRISTO. Kwahiyo hayo majengo yanayowachanganya mpaka mkaanza kujifunza historia ya dhehebu lenu ili ukitembea ujisifu kwa wengine ni upuuzi na kujilisha upepo. Soma neno ujazwe Roho mtakatifu uone kama utabaki mtu wa kuwaza chini ya viwango vya kiroho kiasi hicho. Unamkuta mtu  kajiandika I LOVE JESUS lakini maisha yako hayaakisi hata kidogo hilo neno hata mawazo yako tu hayajui kama kweli kuna YESU ndani yako. Badilika ndugu mpende YESU kwa moyo wako wote, roho yako yote, matendo yako yote, nafsi yako yote na akili zako zote. Ili yeye aliye Bwana wa rehema na neema akutakase mwili wako, nafsi yako na roho yako siku zote za maisha yako. Biblia inasema wazi kabisaa kuwa utatambuliliwa kwa matunda yako mathayo 7:20. wala siyo kwa maandishi kwenye mashati yenu wala siyo kwa kuwa church girl and church boy ambao ni ushetani mkubwa ndani ya kanisa.  

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.