Header Ads

WIFE & HUSBAND MATERIAL

DOWNLOAD HII PDF

Kuna maarifa ya Ki-Mungu ambayo ukiyakosa yanasababisha ukose au uchelewe kumpata mtu wa kufunga naye ndoa. Mimi mwenyewe nimejionea Mtumishi wa Bwana akitumwa na Mungu kumwambia dada mmoja; Mungu akasema “ulitakiwa kuolewa mwaka huu, lakini kwa kutokujua kwako umekosa watu wawili mpaka sasa” na huyo mtumishi akasema “nakwambia hili ili usije ukakosea tena, kwani Mungu anakuletea mtu mwingine wa tatu sasa”.

Pia yapo mambo yanayomfanya mtu atafutwe au awe anakutana na wale wa hit and run badala ya mtu wa ndoa. Mkaka akiulizwa “unataka uoe mwanamke wa namna gani?, cha kwanza atasema “awe mcha Mungu na mwenye tabia Njema”. Mdada naye atasema “nataka mume mwenye Hofu ya Mungu, anayejua kupenda na mwenye akili za kimaisha”; Hii ni njema, lakini je nawewe uko kama huyo unaemtaka? (Maana Hakika Bwana atakupa wa kufanana naye).

Bwana anasema “Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna. Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele. (gal.6:7-8) .

Kwahiyo kama mwanamke unataka uwe na mwanaume mwenye hofu ya Mungu; Inamaana huyo kijana mwenye hofu ya Mungu lazima atakuwa hataki kutenda dhambi na anaziogopa dhambi, ikiwemo ile dhambi ya kuwaka tamaa. Sasa kama wewe ni dada na unavaa nguo na suruali za kubana, zinawasha tamaa wanaume; utasumbuka sana kumpata mtu mwenye hofu ya Mungu.

Hata kama umeokoka na unanena kwa Lugha; Lakini mavazi yanakugharimu wewe. Kwani kwa kufanya hivyo unawasukumia mbali wenye hofu ya Mungu na kuwavutia wale waharibifu, unawavutia wawaka tamaa, wale watu wa “hit and run”. Usiutumainie mwili kumpata mwenzi wa ndoa, maana Bwana anasema “yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu;” (gal.6:7). Ukitaka kupendwa kwa kuvaa kimitego unaishia kuvuna watu wa “hit and run”

Tambua kwamba; tabia yako, mwenendo na usemi wako ni mbegu kwa wengine na ni matunda kwako. Na kutoka kwenye hayo, anaetaka kuwa nawe anapata picha ya jinsi gani maisha ya ndoa yatakuwa kama ukiwa naye. Bwana anasema “uwe kielelezo…, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi” (1tim.4:12). Maana mtu wa ndoa atakupenda na kutambua kama unafaa kutokana na jinsi unavyo-behave; kwasababu “Mtawatambua kwa matunda yao” (mt.7:16-20)

Kama unataka kumpata mwenzi wa maisha sasa… lazima uwe presentable. Jiandae basi uonekane unastahiri kuolewa au kuoa. Lazima uwe wife au husband material. Ili wale wanaotafuta mke wakikuona moyoni mwao waseme “huyu anaweza kuwa mke” au wadada waseme “huyu anafaa kuwa na mke sasa”. Sio kila wakikuangalia waone bado hujielewi au waone hujiheshimu. Kristo anasema “nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema” (mt:5:16)

Chukulia kama umezaliwa ili uwe mtoaji mali mkubwa kwa ajili ya kanisa la Bwana, alafu ukakataa kuokoka kabla ya kuoa, then ukaoa mwanamke mwenye moyo wa ubahiri; unategemea nini hapo kama ukiokoka baada ya ndoa?. Kwahiyo ni hatari sana kwa kijana kuishi bila wokovu.

Mwanamume imekupasa uwe na Roho Mtakatifu, yaani uwe umezaliwa mara ya pili (born again/kuokoka)(tit.3:3-7). Pili lazima uwe na maono, uijue assignment ambayo ilikuleta duniani. Uzuri wa sura na umbo unayo thamani kwa mwanamke kama anaye Kristo ndani yake, lakini kama Yesu sio Bwana na Mwokozi wake; uzuri wake ni ubatili, tena ni harufu ya uharibifu. Kama ilivyoandikwa “uzuri ni ubatili; Bali mwanamke amchaye Bwana, ndiye atakayesifiwa” (mit.31:30)


Mwandishi: Nzunda Ibrahim (0754 210 627)

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.