Header Ads

ONLY GOD CAN JUDGE ME

pakua pdf hapa
Ukweli ni upi kuhusu hukumu? Je,ni kweli kwamba MUNGU pekee ndiye anayetoa hukumu? Na pia hukumu ni nini?.

Nilipokuwa nasoma biblia nikakutana na mstari unaosema “hamjui ya kwamba watakatifu watauhukumu ulimwengu? Na ikiwa ulimwengu utahukumiwa na ninyi, je! hamstahili kukata hukumu zilizo ndogo” (1kor 6:2). Sasa unaweza kujiuliza, je, watakatifu ni miungu? au je watakatifu wapo duniani?.

kama hawapo duniani wako wapi? na kwa muda huu wanafanya nini huko? Imeandikwa “kwa kanisa la Mungu lililoko Korintho, wale waliotakaswa katika Kristo Yesu, walioitwa wawe watakatifu,...” (1kor.1:2). Hapo kuna neno “kwa watakatifu walioko korintho” (ambalo ni jina la hapa duniani), na tena “Watakatifu waliopo duniani ndio Walio bora, Hao ndio niliopendezwa nao” (zab 16:3). Hapa ndipo unagundua kuwa walioitwa kuwa wana wa MUNGU ndio walio watakatifu na ndio watakaouhukumu ulimwengu. Sasa Je wewe ni mtakatifu ambae unaweka ONLY GOD CAN JUDGE ME?.

Ni kweli imeandikwa “Msihukumu, msije mkahukumiwa ninyi” lakini usiishie hapo maana sababu yake imetolewa sehemu nyingine kwa kusema “wewe mtu uwaye yote uhukumuye, huna udhuru; kwa maana katika hayo umhukumuyo mwingine wajihukumu mwenyewe kuwa na hatia; kwa MAANA WEWE UHUKUMUYE UNAFANYA YALE YALE”. (war 2:1). Kwahiyo kama wewe siyo mtakatifu usihukumu kwani “hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa; na kipimo kile mpimiacho, ndicho mtakachopimiwa

Basi amini amini nakuambia, watu wale ambao miili yao ni Hekalu la Roho Mtakatifu ndiyo watakatifu watakaohukumu ulimwengu. Pia hao ndiyo leo kabla hawajatoa hukumu siku ya mwisho ndiyo wanaolitangaza neno la uzima; ili pale watakapokaa kukuhumu uwe unaijua kweli. Na uwe mwenyewe ndiyo umelikataa neno liletalo uzima kwa kufuata matakwa yako mwenyewe. maana imeandikwa “Na yeye asiyetahiriwa kwa asili, aishikaye torati, je! Hatakuhukumu wewe, uliye na kutahiriwa, ukaihalifu torati?” na tena “Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.” (warumi 2:27)

Mungu amesema “Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu”. Basi ndugu yangu nakusihi badilika, ubali hukumu za haki siyo kujivika kiburi cha kwamba MUNGU pekee ndiye anaweza kukuhukumu wakati maaandiko yako wazi juu ya hilo kuwa watakatifu au walioitwa na kutii sheria za MUNGU ndiyo watakatifu watakaohukumu ulimwengu huu.

Ndugu, na wewe pia unaweza kuwa mmoja wa watakatifu ili usihukumiwe kwa hukumu ndogondogo, bali wewe ndiyo uje uwahukumu wale wote wasioamini. Na njia pekee ni kumpokea Yesu Kristo na kukiri kuwa MUNGU alimfufua kutoka katika wafu (war 10:9)
Mwandishi. Michael Basa (0765 279 698 / 0789 799 199)

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.