SOMO:- AINA ZA UVIVU
Kuna aina tatu za mtu mvivu kibiblia nazo ni
1. MVIVU WA KUTOANZA KUFANYA JAMBO:- huu ni uvivu
namba moja kwangu kwa maana kwa mtu mvivu kwake ni kitu cha maana kabisaa kuja
na sababu ya kuacha kufanya kitu Fulani pasi na kuangalia sababu za kufanya
hilo jambo. Huwa ni mzuri katika mifano ya kushindwa na mitazamo ya
kutofanikiwa kuliko kufanikiwa kwake. Mtu mvivu anaweza kuamua kuanza kufanya
biashara bali akafikiria kisha akamfikiria mtu mmoja aliyeshindwa kuimudu hiyo bisahara
kuliko watu kumi wanaofanya kwa mda huo na wamefanikiwa. Kwa huyu mtu kila
changamoto kwake ni kamba ya kumrudisha nyuma kuliko kupambana. Kwa huyu mtu ni
ngumu sana kuuona mkono wa MUNGU ukitenda kwake. Mithali 6:9 na mithali 26:13-14
2.
MVIVU WA KUTOMALIZIA JAMBO:- hebu fikria mtu
ambaye anaamua kuanza kula. Anaanza kupika mpaka anamaliza anaweka mezani
ananawa na mikono halafu anajihisi uvivu kula. Huu ndio uvivu ninaouongelea
hapa. Uvivu wa hapa huwa waajabu sana na watu wengi huwa unatukuta.Mfano wa kawaida unaamua kuanza kufanya jambo Fulani na maandalizi yake unayakamilisha halafu kulikamilisha unashindwa au unakata tamaa. ‘Mtu mvivu hutia mkono wake sahanini; Ila hataki hata kuupeleka kinywani pake.’’{mitha 19:24}. Uvivu wa jinsi hii humfanya mtu asione mafanikio ya kila anachofanya. Pia hushindwa kupanua hozi yake na mafanikio yake huhesabiwa kwa leo tu wala si kwa kesho na motto wake ni ngumu kurithi kutoka katika uvivu wa namna hii.
3.
MVIVU ALIYEKOSA MAARIFA:- aina hii ya uvivu ni
maarufu kuliko mwingine wowote. Maana mtu hutumika katika huu uvivu pasi na
kujua. Huu huja katika sura mbili nazo ni 1) kufanya jambo tofauti na mipango
ya MUNGU juu yako.Mungu anaweza kuwa ameweka Baraka zako shambani nawewe upo mjini basi wewe unahesabiwa kuwa ni mvivu katika ulimwengu wa roho. 2)ni mtu ambaye yuko sehem sahihi ya kupokelea Baraka zake. Lakini kumbuka Baraka hazipo kama mvua nyikani bali zipo kwenye kila ufanyalo na yeye akakaa ila kufanya jambo basi atakuwa masikini. ‘’Mtu mvivu hataki kulima wakati wa baridi; Hivyo wakati wa mavuno ataomba, hana kitu’’{mitahali 20:4}. Huyu mvivu anayeongelewa hapa ni yule ambaye majira sahihi ya kufanya jambo anakuwa hataki kulifanya hilo jambo. Majira yakipita ndio hugeuka kuja kulifanya ndio maana biblia ikasema ‘’hataki kulima wakati wa’’. Ingekuwa hataki kulima majira yote isingesema wakati wa……
Basi ndugu katika BWANA anza
kuomba sasa uvivu wa aina yoyote ukuepuke kabisaa. Maana MUNGU anataka
kukubadilisha wewe na kila kitu chako kutoka mhitaji mpaka asiye na uhitaji.
Mwandishi :- MICHAEL BASA
Hakuna maoni
Chapisha Maoni