FEEL LOVED
Napenda kupendwa na ninapenda kupenda pia nafurahia kila kitu katika maisha yangu kwasababu nakipenda kukifanya na kinanipa amani katika matokeo yake. Nampenda YESU maana yeye alinipenda kwanza mpaka akatoa uhai wake kwaajili YANGU. Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake{yoh 15:13}. Bibilia ilinishangaza sana kuniita rafiki wa YESU kwamaana hatakuja kunificha kile anachofanya kwaajili yangu wala anachowaza hata yale mafumbo ya siri kanipa akili ya kuyajua{yohana 15:13-17}.
Wakati kuna watu wanamiungu yao wanamitume wao wanawaalim wao na haawajawahi kuwa marafiki nao hata hawakuweza kutolala kwaajili yao{yohana 8:31-35}. Lakini mimi nimekarimiwa pendo lipitalo mapendo yote namimi kubaki na agizo la kushika maagizo tu. Namjua yeye ni pendo na yuko karibu nami kuliko watu wote wala hapana mtumwa, wala ndugu ajuaye siri zangu kuliko yeye.
Kanipeleka angali ni mchana kutenda yaliyofichika kwenye hekima za wanadam wenye busara na vichwa vyenye mvi{yohana 12:35}. Naam pendo limenikirimia ujasiri wa kuingia patakatifu pa patakatifu pake bila mbuzi wakutekezwa mkononi wala kafara ya kutekezwa wala kujihesabia hatia. Nikapewa mamlaka juu ya mapepo na yule mkuu wa anga la giza akawekwa chini yangu {mathayo 10:19}. Huku ndiko kutawala kwa mwanzo mwanadam alikopewa edeni. Pia pendo hili limenifanya mfalme na kuhani pia. Likanipa pia nguvu yakushinda kila kushindana kutakapo kuja kwenye njia ya BWANA wangu.
Nimejipumzisha kwenye hili pendo na uzuri wake umenipa amani na furaha navyo havitakishwa kesho maana tumaini lipo mbele yangu siku zote za maisha yangu. Nafurahia kupendwa nami nampenda pia tena ROHO wake amenipa ili kuwa mwana wake nami nipo kwenye pendo la MWANA wake.Mkizishika amri zangu, mtakaa katika pendo langu; kama vile mimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake{yohana 15:10}. Hata aliye mkuu asiyekuwa kwenye hili pendo ameshushwa hata chini kupita kuzimu. Naam mpumbavu yupo aliyemkubali BABA na kumkataa MWANA amekuwa mpumbavu kuliko wengine wote kutoka kwenye tumbo la mwanamke. Kulikataa pendo liloshushwa na BABA ni sawa na kuiona njia ya kuingia uzimani na ukajikwaa katikati yake na kuanguka hata usiweze kuinuka.
Namwingine ni yule aliyejiambia nafsini mwake hakuna MUNGU amekuwa sawa na makapi yapeperushwayo na upepo usiokuwa na hijara huko uendako . Nimejipa neno la maarifa hata limekuwa la kuaminiwa na mataifa pendo husitiri udhaifu wangu kila siku hata sasa nimekuwa kamili katika mambo yote. Aabuduye miungu na ajipepeleze nafsini mwake kwa kazi ya mkono wa mwanadam ameifanya tumaini lake je si mtu asiye na akili tu awezaye kufanya hivyo?.
Nami nilipopungukiwa na akili nikayumbishwa huku na huko kama merikebu katikati ya bahari iliyojaa taabu ni sawa na siku ya utungu wa mwanamke mpaka nilipogundua kumtumikia BWANA pekee. Pendo lake limefuta machozi hata sasa ni mwana wake kweli ampendezaye babaye na BABA kamkirimia pendo lipitalo mapendo yote. Hata amani amenipa ambayo ulimwengu huu hauwezi kunipa. Ninatumaini la maisha ya sasa nayajayo kwenye ulimwengu huu na ulimwengu ujao. wangu Kila kunapokucha na kutafakari ukuu wa BWANA.

I SMILE AND SAY '' I FEEL LOVED''
Hakuna maoni
Chapisha Maoni