Header Ads

UKITAKA NISIWE HAPA FANYA HAYA

 
         Nilikuwa nafikria mfano wa kwamba kama majira ya kuzaliwa YESU asingekuwepo bikra je angezaliwa au angesubiria?. Ndipo nikagundua kwamba utakatifu wa MARIA ulikuwa ni sifa ya kumtofautisha kutoka kwa mabikra wengine wa kipindi hicho. MUNGU hujisazia watu anaowataka yeye mwenyewe kwa kazi yake maalum na shetani anapewa ruhusa tu ya kumgusa yeye na siyo kugusa kile kinachobeba utukufu wa MUNGU. 
             Ukitaka kujua kwanini upo unaishi mpaka leo tafuta kujua kususdi lako la kuzaliwa sio la kuishi. Kuna tofauti kati ya kuzaliwa kwa kusudi na kuishi kwa kusudi. Kuzaliwa ni hatua ya kuwekwa kwenye mazingira ya kufanyia kazi yako{To be born is the chance of a new man to be exposed to a working field}. Lakni kuishi ni kipindi cha kufanya kazi yako uliyopewa. Ndio maana unaweza kuacha kufanya kazi uliyopewa kwenye mazingira uliyowekwa na bado ukaishi. Kuacha kutumikia kusudi halisi inasababishwa na mambo matatu makuu nayo ni:-

  1. KUHARIBIWA KWA WAZAZI WAKO: kwa kawaida mtu huzaliwa hajui chochote maarifa yote huyakuta duniani. Lakini yeye mwenyewe anakuwa hana uwezo wa kutofautisha chochote mpaka ajifunze. Nayo huchukua mda kujifunza na baadaaye huamua nini ashike na nini asishike. Ndio maana mtu aliyepata nafasi ya kuishi na watu wengi tofauti anakuwa na uwezo wa kufkria zaidi kuliko yule ambaye hajapata huo wasaa. Wazazi wa mtoto ndio humfanya mtoto achague ujenzi wa msingi wa mtoto wao baada ya kuzaliwa. Wazazi ukitaka wanawaza tofauti na kile cha ndani yako ambacho MUNGU amekupa kwaajili ya watu wengine. Hakika utakufa nacho kikiwa bado hujawahi hata kukitumia kabisa. Wazazi wengi kwa ufaham wao wanajua kuwa mtoto akisoma ataajiriwa na kisha maisha yake yatakuwa mazuri tu. Na mtoto anakua anajua hivyoo kwasababu kafundisshwa hivyoo. 
  2. MAZINGIRA YASIYO RAFIKI:- Mtu anakulia kwenye mazingira yasiyo rafiki kabisaa. Pata picha kwa hicho unachokifanya je nichako mwenyewe au ulikiona kwa mtu kafanya au hata hujui kwanini unakifanya?. Kuna watu ni waanzilishi wa vitu kutokea na kuna watu niwaendelezaji tu. Ukikuta anayetakiwa kuanzisha anawekwa kwenye mazingira ya kuendeleza basi hakuna atakachoanzisha maisha yake yote.
  3. KUHARIBIWA KWA UWEZO WA KUFIKRI:- Kuna mifano mingi sana kwenye huu upande kuna watu wapo na kila kitu cha kuonesha karama zao lakini wameshindwa aidha hawajiamini au hawaoni umuhimu wa kuwa mtu maarufu kwa karama hiyo. Kuna wamezaliwa kuongoza na watu wa kuwatia moyo wapo na pengine watu wakuwaunga mkono wapo. Lakini hawapendi kuongoza lakini kwenye mkumbo wa kulalamikia uongozi wamo. Ukichunguza unakuta uwezo wao wakufikria kiuongozi hawana kabisa hili ni tatizo kubwa sana.
BASA asingekuwepo leo BASA ministry isingekuwepo. Kuna mda MUNGU huamua kutumia mazingira magumu{harsh condition} kwaajili yako wewe kuonesha uwezo alioweka ndani yako. Ngapi umejaribu kuwa mtu asiye wewe na umeshindwa hebu rudi Mungu anataka kukufundisha na kukuelekeza wewe ni nani na uanze kufikria vipi?. Once you fail to be who you are?. Soon you will be the enemy of yourself and prey of your opportunities. Live in JESUS and become who you are.  

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.