SHULE YANGU NDANI YA YESU
Elimu ni bahari aka haina mwisho wahenga walisema. Tunajifunza kwaajili ya kupata uwezo wa kufikria zaidi ya hapo mwanzo au Kufikria kwa jinsi bora zaidi. Kuliko ile ya mwanzo tuliyokuwa tunaitumia. Kuna kipindi mwanadam uwezo wake wa kufikri hukoma na huhitaji kupata maarifa au elim zaidi ili aweze kuenenda sambamba na tatizo lake kufikia utatuzi. Kuna maarifa ya safari ya kuwa mkazi wa mbinguni.
Haijalishi uko kanisa gani wala kanisa lako lina historia gani tokea kuanzishwa kwake. Kuna watu wanasifia sana wachungaji wao kuwa ni manabii au wanaupako sana kuliko wa kanisa fulani; lakini huo uasherati wako ndio utakaokufikisha mbinguni?????. Hebu fikria tena hayo mavazi yako ya nusu unayovaa kwa kigezo cha kupendeza je ni upako wa mchungaji wako au ni historia ya kanisa lako ndilo limekuelekeza hivyo??. Kuna watu wanajisifia kuwa wameokoka na wameona kuwa ni sifa kuokoka au ni jambo la kutumainiwa sana lakini je huo uongo wako nao ni moja ya wokovu?.
Unaijua kweli gharama ya kufika mbinguni au kusoma kozi ya mkazi wa mbinguni na kuifaulu kweli wewe??. Subiri ni kuambie kitu ukitaka kujisifu na ujisifu katika KRISTO{2wakorintho10:17}. Faulu kwanza masomo ya ROHO MTAKATIFU amabaye anafundisha masomo sita nayo ni 1}KUUSHINDA MWILI 2}KUSHIKA NENO LA BWANA 3} MAOMBI 4} MIFUNGO 5} KUMTII BWANA na 6}UTAUWA. Hizo ni kozi ambazo ni lazima ufaulu na hapo hakuna kozi ambazo tunajisifia sana huku kwetu kama 1}KANISA LETU TUNASOMA SANA BIBLIA 2}KANISA LETU LINA HISTORIA KUBWA 3} MIMI NIMEOKOKA WEWE HUJAZALIWA 4}DINI YETU INAAMINI KWENYE KULA NA SIKU 5} MUNGU WA ELIYA NDIYO MUNGU.
Hizo zote ni porojo tu za hapa duniani naza watu waliopotea sana. Je hujawahi kuona watu wa mataifa ambao nafsi zao zinashuhudia ndani yao kuwa wamepotea wanakuhukum wewe na bado wakajihesabu wao ni bora kwako hata maramia. Ndio maana nasema rudi SHULE YA YESU ukajifunze tena kwake kwamda zaidi. Ndipo utajua kuwa ni kwanini mmoja wa wanafunzi alifurahia mateso na kuhesabu kila kitu kuwa hakina thamani tena?. Au ni kwanini YESU alisema kuwa mtu akimpenda ndugu yake au mwenza wake kuliko YEYE hafai kuwa mkazi wa mbinguni??. Chagua leo kurudi miguuni pa MUNGU ukajifunze tena upyaa ndipo matunda yataonekana waziwazi na watu watakiri kuwa wewe ni mmoja wa wakazi wa mbinguni.
by MICHAEL BASA +255(0)765 279 698
Hakuna maoni
Chapisha Maoni