Makanisa ni sehem nzuri
sana ya kusanyiko kuonyana, kuelekezana, kufundishana na kutiana moyo katika
njia ya BWANA. Lakini kanisa hilo pia linaweza kupotoka na kuacha kuweka mkazo
kwa washirika kwenye safari ya kwenda mbinguni na kurukia mambo ya kidunia. Kuna
makanisa yanapinga injili za kufanikiwa sijui wanatumia biblia gani?? Hebu soma
torati 28:1-22 lakini rudia tena kuusoma msitari wa 12{hasa hapa………nawe utakopesha mataifa
mengi, wala hutakopa wewe.} fikria kwa kina huu msitari. Je ulishawahi
kumuuliza ROHO mtakatifu kuhusu kanisa lako juu ya huu msitari. Naye alikujibu
nini?? Je alikujibu kuwa na mali ni anasa na je matajiri wote hawataenda
mbinguni??
2wakorintho
8:9 { Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi
alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi
mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake.}. je huu nao haupo
kwenye biblia yako mtumishi wa MUNGU aliye juu??. Haijalishi wewe ni nabii au
mwinjilisti kwangu hakuna tofauti kwamaana biblia yasema kila mtu na atuhesabu
hivi tu watenda kazi pamoja na KRISTO.
Lakini katika kutenda kazi pamoja na
KRISTO kumbuka kumtumia ROHO wake ili kutengeneza mambo yaliyopo na yajayo kwa
usahihi zaidi. Kwamaana watu makanisa yameacha injili kamili ya KRISTO na
kujikita kwenye magomvi ambayo yanamuudhi ROHO wa BWANA na kumpa ibilisi
utukufu. Na kuna mmoja ambaye alianza katika ROHO naye kamalizia katika mwili. Kaligawa
kanisa kati ya wallio nacho na wasiokuwa nacho.
Ewe mwana wa laana ni nani
aliyekupa ruhusa ya kugawa mafungu watu wa aliye juu kwa tamaa zako mwenyewe. Basi
BWANA amekutaa wewe na wana wako na nyumba yako omboleza kwa tumbo na kwa
utungu anza sasa. Lia wewe uliye nyamaza naamu kesha mavumbini hata asubuhi
maana BWANA hatakuacha salama.
Kuna mwingine aliyepotea
yeye na kanisa lake lote hata dhambi imekuwa kitu cha kawaida kanisani. Mchungaji
anatafuta injili ya kutafuta watu waongezeke lakini hawapi nafasi ya kukutana
na kumjua ROHO MTAKATIFU. Hii siyo injili ambayo YESU aliitaka ihubiriwe na
watu wake ni injili ambayo cha kwanza kitakuwa ni kuingia YERUSALEM MPYA na
siyo kuimiliki dunia.
By MICHAEL BASA
0765279698
Hakuna maoni
Chapisha Maoni