BARAKA ZAKO ZIKUJIAPO
MUNGU ni mfano wa
mwanadam uliojificha wenye sifa na maamuzi na hisia kama mwanadam uliozungukwa
nautukufu pande zote. Tofauti kubwa kati ya mwanadam na MUNGU ni ibada na
dhambi. Mwanadam hutafuta kitu chenye uwezo mkubwa na kukipa sifa ya
MUNGU{maana mungu ni cheo tu na siyo jina ni kama kusema raisi hi hutegemea na
nchi yako na mtu aliyepo madarakani na siyo mtu fulani} na chenyewe hakiwezi
kukipeleka hiyo sifa sehem nyingine. Ndio maana mwanadam humwabudu mungu na
wala mungu hamwabudu mwanadam. Ukikuta mungu ana mungu wake kuna sifa ya kiungu
hupungua kwake mfano mungumtu. Basi ukikuta mungu wako ana mungu mwingine ujue
huyo yupo kwa kazi fulani na kuna anashindwa kutenda mpaka umjue mungu mkuu
wake maana yeye ndio anampa mungu wako nguvu za kujibu maombi yako. Kingine ni dhambi, haya ni
matendo au fikra ambazo mungu unayemtumikia anazipinga kwenye ufalme wake au
kwenye ibada zake. Mfano wake ni MUNGU-YESU kutamani uasherati na mfanya
uasherati wote ni wamefanya zinaa katika ullimwengu wake. Basi tujikite kwa
MUNGU muumba mbingu na nchi na aliyeandikwa kwenye biblia tu maana sitajikita
kwa miungu wengine waliobaki nje ya huyo.
Baraka ni mafuta au nguvu anayopokea mtu
kwaajili ya kumiliki kitu vitu au eneo pamoja na vilivyomo ndani yake. Basi
MUNGU akikubariki kwenye kazi fulani amekupa kila kitu kinachohusiana na hiyo
kazi kinachobaki ni wewe tu kujua nguvu ipi itumike wakati gani?. Mfano mzuri
maarifa yapi yatumike wapi na kwa wakati gani?, busara itumike kwa mtu gani
na kwanini??, watu wa jinsi fulani uwamiliki vp?, pia nguvu ya maono ya kazi
unayofanya utaweza kujua kipi ni muhimu kwa majira na nyakati zake. Lakini ili MUNGU akubariki
inakubidi ujitahidi kugusa moyo wake maana bila hivyo huwezi kufanikiwa katika
baraka atakayoiachia kwako. Ukisoma torati 28 utakuta baraka nyingi sana
ameahidi MUNGU kukupa lakini baraka zote hizo zimegeuka laana kwa maana msitari
wa kwanza wa torati 28 unasema kwamba ''Itakuwa utakaposikia sauti ya Bwana,
Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo,
ndipo Bwana, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani;''.
Baraka zote ulizoahidiwa zinaweza kukupata kama nguvu ya yakufanikiwa au nguvu
yakukurudisha nyuma{laana} kwasababu ya sautu ya MUNGU. Kuna vitu vitatu katika
msitari huu ambavyo ni muhimu sana navyo ni:-
- Itakuwa utakaposikia sauti ya Bwana, Mungu wako,
- kwa bidii,
- kutunza
- kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo,
Kuna kitu muhim cha
kuelewa hapo nacho ni kusikia ssauti ya MUNGU. Hii inaonesha MUNGU anasema
nawewe baada na kabla ya kukupa hiyo nguvu. Pili usisikie tu kwa jinsi ya
kawaida lakini uwe mtu wakujitaabisha kwaajili ya kusema na MUNGU wako ndio
maana kuna neno bidii hapo. Tatu baada
ya kuisikia ni lazima kutunza kwa maana nyingine ROHO ananiambia hapa ni
kuchambua ili kuvijua {mtumie ROHO tu hapa ili uwe vizuri zaidi katika kipande
hiki}. Baada ya kuvichambua na kuvijua vyote chukua ambayo ni maagizo ndiyo
ukayafanye kwama alivyoagiza MUNGU mwenyewe katika kusema kwake. Usitende kwa
jinsi ya kibinadam maana itahesabika kama uasi mbele za MUNGU.
imeandikwa na MICHAEL BASA
Hakuna maoni
Chapisha Maoni