NEEMA ILIYOZIDI SHARIA
Neema {grace the free and unearned favour of
God, a divinely given talent or blessing} ni hali ya kupata kitu ambacho
hukustahili kupata kwa matendo,elimu,uwezo au muonekano wako. Kwa mkristo ni neema
imeelezwa ni haki kuupata wana wa Mungu. Kwamaana baada ya Yesu kufa msalabani
kwaajili ya dhambi za watu wengine kwahiyo yeye{YESU} anateswa hali mwenyewe
hajafanya tendo lolote lipasalo kufa. Maana yake ni hii mtu atendaye dhambi
asitahili kifo tena cha aibu kilichojaa mateso. Mwanadam alikuwa na dhambi na
alihesabiwa kifo waefeso 2:1 Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu;
Yesu mwenyewe akajitoa kufa kwaajili ya kuichukua hiyo hatia na huyu mwanadam
ambaye hakustahili mwanzo apate kibali cha kuwa mwana na kupaingia patakatifu
pa Mungu.
Sharia ni taratibu ambazo huwekwa kwa ajili ya kuongoza,kulinda au
kuweka usawa kwenye kundi husika. Hizi huwekwa kwa makusudi ya kumtia mtu hatia
na siyo kumwokoa. Kabla ya Kristo kuja sharia zilikuja kwa mkono wa musa.
Ziliwekwa ili watu wajue kuna Mungu wa baba yao Ibrahim, Isaka na Yakobo ambaye
anapaswa kuabudiwa ndio maana ukisoma torati ya Musa utakuja kuona ni kiasi
tendo la dhambi lilihukumiwa kwa kifo mda wote ndani ya kundi.
Yesu alikuja na second chance ya dhambi
badala ya kifo ndio maana ukisoma (marko 8:1-11). Sharia ipo kwaajili ya
kuonesha makosa na siyo kusahihisha na pia haina nguvu ya kusaidia mtu asitende
kosa husika. Bali husimamia hukumu juu ya mwanadamu. Napenda msomaji unielewe
hivi kwasababu ya sharia ya dhambi, mauti(kifo) ilipata nguvu na kwasababu ya
neema uzima unapata nguvu ya kuishinda dhambi.
Basi neema ilikuja ulimwenguni na kuifanya
sharia kuwa kivuli cha mambo yanayotakiwa kutendwa. Yaani namaanisha kule
kusema usile wala kunywa ni kwa sharia. Bali kwa neema kula vyote na kunywa
vyote katika Bwana. Kwamaana bwana mwenyewe ataandika njia zake katika mioyo
yetu kama ilivyo ahadi(Ezekiel 36:26-27). Ndiyo iliyokuja kutimizwa kwenye efeso
8:9&10.
Tamaa yangu ni wote tujue hili neno katika
Roho 1timotheo 1:8-10 Lakini twajua ya
kuwa sheria ni njema, kama mtu akiitumia kwa njia iliyo halali; akilifahamu
neno hili, ya kuwa sheria haimhusu mtu wa haki, bali waasi, na wasio
wataratibu, na makafiri, na wenye dhambi, na wanajisi, na wasiomcha Mungu, na
wapigao baba zao, na wapigao mama zao, na wauaji,na wazinifu, na wafiraji, na
waibao watu, na waongo, nao waapao kwa uongo; na likiwapo neno lo lote
linginelo lisilopatana na mafundisho yenye uzima;.
Basi neema ni Zaidi ya sharia kwamaana huwaelekeza na kuwakalisha
watu katika uzima na uchaji Mungu. Ile neema ya kuweka{kuandika} sharia za
Mungu katika mioyo ya watu wote wanaolikili neno la neema ya kuwa Yesu ni Mwana
wake kamili. Hakika na wote walioijiliwa na neno la mwana wake walifanyika kuwa
wana wa Mungu. Tena ikaandikwa mimi leo nimekuzaa. Neno hilo halikuwa kwaajili
ya malaika wa mbinguni bali ni wale kwa uchaji wao hufanyika miungu. Basi
naijulikane hivi Maana neema ya Mungu
iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa [tito 2:11]. Tena neema hii huokoa watu wote na haiwaweki chini ya kongwa la
utumwa bali huwaweka huru. Kule kusema wote ni nini basi? Kwamaana kwa neema
wote waliokili na kubatizwa hakika hao ndio walio katika neema hii. Tena
wakaandikiwa wote kwa njia ya wokovu kama ilivyoandikwa kwenye mariko 16:16,
rumi 10:12-17.
Prop,Mwal: Michael Basanorare 0765 279 698, +255 737 919 561
JINA LA BWANA LIBARIKIWE
Hakuna maoni
Chapisha Maoni