VITA FEKI VYA KIROHO
Kuna watu wanapigana vita vya kiroho ambavyo havina uhalisia katika ulimwengui wa kiroho. Ni vita ambavyo ukivitazama unaona kabisaa huyu mtu yupo katika vita maana mbinu zote za kivita anazitumia lakini vita haiishi. Vita huwa katika mwili na siyo roho ya mpiganaji. Ukitazama moyo nao unanjia zake ambazo unaweza kuziona ni njema sana lakini mwisho wake ni mauti. Lakini kuna vitu ambavyo ukipigana watu wa mwilini watakuona unajaribu kweli kweli mpaka wengine watajitokeza kupigana nawe au kukusaidia lakini kweli hata silaha unayotumia siyo ya kweli haina risasi za kweli. Hata unayepigana naye hawezi kuonekana na utasumbuliwa mpaka na vijaribu visivyoumiza kwenye maisha yako navyo utavikimbia pia.
Jinsi ya kushinda hivi vita
1. Ijue vita unayoipigana
2. mjue baba wa hiyo vita
3. tafuta mistari ya kupigania hiyo vita kutoka kwenye biblia
4. badilisha baadhi ya vitu ambavyo unavipenda kama misuko yenye utata, mavazi yenye utata, minyoo yenye utata, michezo yenye mizaha na baadhi ya mawazo ambayo huamsha ukosefu wa Amani ndani yako mf kuona unashindwa kutimiza lengo Fulani au kuendelea au kujiona wewe huwezi kuwa mtumishi bora
5. wewe ni nabii mbele za Bwana, tumia ulimi wako kujitabiria mema kila siku yaseme hayo mema mpaka mtu wako wa ndani aamini na awe anayakumbuka kila uamkapo na ulalapo.
6. Usilazimishe lisiliokuwa kusudi la Mungu litukie juu yako.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni