Header Ads

JEMEDARI KALALA

 













Kijana mmoja mpole aliyekuwa na haiba ya uoga wa kupindukia ambaye mwanzo alikaa katika hali ya mateso mengi sana kutoka kwa jamii iliyomzunguka ambayo ilikuwa inatawaliwa na nguvu ya mfalme mmoja ambaye hakuwa na chembe ya huruma hata kidogo. Alipotoa amri ya hakuna kulala watu wote walitii na aliyekaidi alimwadabisha bila huruma. Alikuwa na askari maelfu waliomsaidia huyu mfalme asiyekuwa na huruma kwa wannchi wa nchi ile. Viongozi wa hayo majeshi walikuwa sita ambao walisifika sana kwa kutoa adhabu barabara kwa wote waliokaidi kutii amri ya mfalme. Viongozi hao ni

  1. Hofu
  2. Umasikini
  3. Kutotii
  4. Ujinga
  5. Maradhi
  6. Usaliti
Hawa viongozi wa majeshi walikuwa na vikosi vyenye nguvu kila mmoja. Ambapo waliweza kufanya kazi na vikosi kwa kujitegemea au kuungana kwaajili ya kupambana na himaya iliyotaka kujiinua kinyume na mfalme wao. Hii ilisababisha watu wa miji mbali mbali kuwa vibaraka watiifu kwahuyu mfalme. Mfalme alipotoa amri watu walitii, hata waliopinga walihakikisha mioyo yao tu ndio inapinga lakini miili ilitenda sawa sawa na mfalme alichotaka tena bila kusitasita. Kwasababu ya watu wengi kuishi kwa miaka mingi katika hali hiyo ilifika kipindi wakazoea na wakaona ni mfumo kamili wa Maisha ambao bila huo hakuna Maisha tena. Miaka mingi baadaye kijana mmoja alizaliwa kwenye Maisha ya kimaskini sana ambayo kwa wakati huo yalikuwa ni Maisha ya kawaida sana kwa jamii na hakuna aliyekuwa anaweza kukusema wala kukushauri. Kijana yule alipewa jina BASA na BABA yake na alikua katika mazingira yale yale na majeshi yalikuja kuzunguka kijijini kwao na mwenyewe alijionea mateso makubwa watu waliyoyapata. Akaazimu moyoni mwake atakapokua mtu mzima lazima aje awakomboe hawa watu kutoka kwenye mateso yale. Baada ya miaka 25 baade kijana aliamua kuanza harakati lakini akagundua kuwa katika mji ule wote waliosoma walikuwa wengi ni waongo{wanafiki} na wamezibwa midomo kwamaana kusema kinyume na mfalme basi lilikuwa ni kosa kubwa na wote walilijua hilo na wao waliamini hivyo. Mtu alipotaka kufanikiwa kwa elimu ile basi alitakiwa asome kwanza elimu ya mfalme yule na upate baraka zake ndipo usome elimu zingine. Ambazo pia kwa asilimia 90 aliziandika mwenyewe kwa kuweka kile alichoamini ni bora kwa wananchi wake na kitamsaidia katika kuwaongoza kwa utulivu. Katika kutafuta elimu ya kuwakomboa hawa watu kijana BASA alienda kwa mfalme mwingine ambaye watu wa taifa lake walikuwa ni bora katika mambo yote. Katika taifa lile kulikuwa na jeshi imara sana ambalo kiongozi mkuu wa majeshi yale aliitwa EMMANUEL. Huyu alikuwa ni mtumishi mkuu sana kwenye ufalme huu na mwingine aliyemfuatia kwa madaraka alijulikana kwa jina la HOLLY. 

inaendelea.....

mwandishi: Prop,Mwal: Michael Basanorare 0765 279 698, +255 737 919 561

 

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.