Header Ads

SOMO: HATUA ZA KUINGIA KWENYE MAOMBI----1

kuomba ni moja ya nguzo muhimu sana katika kuuendea ufalme wa mbinguni. Bali watu wengi tumekuwa tunaona maombi ni sehem ya kutimiza wajibu bali kiukweli ni sehem ya kuongea na BABA yetu ambaye kwa imani katuzaa kupitia kifo cha mwanaye YESU KRISTO. Ili maombi yako yawe ni manufaa kwako unaweza pitia kwanza somo la NGUVU ILIYOMO KWENYE MAOMBI ndani ya BASA MINISTRY. Ndio uje kwenye hiki kipande cha hatua za kuingia kwenye maombi ambazo ni:
1}KUSUDI LA MAOMBI YAKO
Watu wengi tunaamini kuomba kwa masaa mengi ndio kipimo cha maombi au maneno kuwa mengi ndio MUNGU atusikia na kutenda unaweza kuta kuwa maombi ya dakika kumi za mwanzo yamejibiwa na yale ya masaa mawili yote hayajajibiwa hata moja. Ukisoma mathayo 6:7&8 YESU alielezea vizuri sana hili jambo ingawa watu wengi hatuelewi alimaanisha nini? Bali ukweli wake siyo kwamba kutoomba kwa sauti wala kurudia jambo wakati wakati wa maombi (mathayo 26:39-44). Bali kuomba kwa mpangilio ulio mzuri na yawe na mtiririko mzuri hata mtu mwingine akisikiliza unaomba ajue unaombea nini kwa mda na umeombea vitu gani. kwahiyo kusudi la kwenda kufanya hayo maombi ni muhimu pia unaweza liandika kwenye karatasi na kuliainisha kwa vipengele kwamba nitaanza na hiki na nitaishia na hiki kipengele.
2}MAHALI 
mazingira yakufanyia maombi yako ni muhimu sana kuliko unavyoweza kuwaza au kulichukulia. Ukisoma mark 6:46 unaona YESU anajitenga na wanafunzi wake ili akaombe lakini anaenda sehemu ambayo hata makutano hawawezi kumuona kwa mda huo ili akaombe tu. Pia ukisoma mark 1:35 unaweza ona YESU KRISTO anaenda sehemu isiyokuwa na watu akaombe tena alfajiri na mapema. Kwahiyo unapochagua sehem ya kufanyia maombi yako chagua iwe ni sehem ambayo hakutakuwa na ususmbufu wowote. Usumbufu ambao utakutoa kuzama kwenye maombi yako kwa mda huo.
3} MUDA WA KUOMBA
Hii imegawanyika mara mbili
  1.              KUNA MDA WA KUKAA KWENYE MAOMBI hapa ninachoongelea ni kwa mda gani utakaa kwenye maombi yako. Ukisoma mathayo 26:39-44 kwenye msitari wa 40 utaona YESU anauliza Je! Hamkuweza kukesha pamoja nami hata saa moja?. Kwamaana nyingine mda ambao YESU aliuona unawafaa hawa watu kukaa kwenye maombi kwa uchache ni saa moja. Je wewe kwenye maombi yako unakaa kwa mda gani rafiki na ndugu yangu katika IMANI?. Mimi nakushauri fanya mda kidogo zaidi ya wewe kukaa kwenye maombi uwe ni dakika 30 lakini usikae hapo ukalizika nenda mpaka ufikie angalau masaa mawili kwenye maombi yako.
  2.           MDA WA KUINGIA KWENYE MAOMBI YAKO. Muda wa kuingia kwenye maombi hakikisha ni muda ambao wewe umemaliza kazi zako au uko huru inamaana hakuna wazo lakuingilia maombi yako akili yako yote iwe kwenye hayo maombi na siyo uwe na nia mbili [double minded]. Kuna mda ambao kibiblia unasiri kubwa ukiufuata nao ni

  •        ALFAJIRI=mda huu unasiri ya jinsi ya kipekee sana kwasababu ni muda pekee ambao daudi aliamsha utukufu wa BWANA juu yake zaburi 57:7—9. Pia Ayubu alikuwa anawatakasa wanaye asubuhi na mapema ayubu 1:5. Natamani nawewe uanze kuutumia huu mda kwaajili ya kuumba siku yako unayoiendea kwako na kwa familia yako yote.
  •            Saa tatu
  •             Saa sita
  •           Saa tisa
  •            JIONI AU MDA WA KUPUNGA JUA= huu ni mda wa ibaada ya shukrani kwa mda wa siku nzima ambao BWANA amekufanikisha. Pia ni mda wako mzuri wa kutafakari mambo yote aliyokutendea BWANA pia ni mda wa wewe kujitafakari umefanya nini kuhusu BWANA?. Kujitafakari ni njia nzuri zaidi ya kujipanga kwaajili ya BWANA juu ya siku ijayo ppia kuungama kwaajili ya makosa ambayo hukuyatambua mda wote wa mchana.


Lakini kumbuka unapochagua mda wa kuingia na kukaa kukaa kwenye maombi hakikisha kuwa ni mda ambao unakuweka katika hali ya msawazo[relaxation]  wa kiakili na mwili ili uweze kujitoa katika Roho na kuzama kwa kumwita BWANA kwenye roho yako


Mtum: Prop: Mwalim: MICHAEL BASA

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.