Header Ads

UBATIZO WA WATOTO WADOGO

KUTOKEA KWENYE SOMO LETU LA UBATIZO{kulisoma bofya hapa} Taratibu za kubatiza watoto kwa kunyunyizia maji zilianza mwishoni mwa karne ya 2 B.K, lakini hazikupata ukubali wa wengi mpaka miaka ya 354-430 B.K. Hapo ndipo watu walioasi walipoanza kufundisha kuwa watoto wanarithi dhambi za Adam na Hawa na kwa hivyo wanazaliwa wakiwa na dhambi ya asili na hivyo wanapaswa kubatizwa baada ya kuzaliwa.

Hayo Yalikuwa Ni Mawazo Yao Waliyotunga Na Siyo Fundisho La Biblia.

BIBLIA iNASEMA WATOTO WANAPASWA KUBARIKIWA NA SIYO KUBATIZWA, BIBLIA INASEMA.
"Basi wakamletea watoto wadogo ili awaguse; wanafunzi wake wakawakemea. Ila Yesu alipoona alichukizwa sana, akawaambia, Waacheni watoto wadogo waje kwangu, msiwazuie; kwa maana watoto kama hawa ufalme wa Mungu ni wao.Amin, nawaambieni, Ye yote asiyeukubali ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo hatauingia kabisa.Akawakumbatia, akaweka mikono yake juu yao, akawabarikia."(Marko 10:13-16).

KUNA HATUA AMBAZO INABIDI MTU AZIPITIE KABLA YA KUBATIZWA..

HATUA YA KWANZA.
Kabla ya kubatizwa lazima mtu mwenyewe bila kulazimishwa Aamini. Biblia Inasema. "Wakawa wakiendelea njiani, wakafika mahali penye maji; yule towashi akasema, Tazama, maji haya; ni nini kinachonizuia nisibatizwe? [Filipo akasema, Ukiamini kwa moyo wako wote, inawezekana. Akajibu, akanena, Naamini ya kwamba Yesu Kristo ndiye Mwana wa Mungu.]
Akaamuru lile gari lisimame; wakatelemka wote wawili majini, Filipo na yule towashi; naye akambatiza." (Matendo 8:36-38). Tena hapa anayebatizwa aliamini mwenyewe, Tena hakuna aliyesema kwa niaba yake.

HATUA YA PILI.
Mtu mwenyewe anatakiwa atubu dhambi zake, Tena kutubu dhambi, sharti kuwepo kujutia dhambi yako. Biblia Inasema. "Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu? Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu." (Matendo 2:37-38).

SASA TUMEONA KUWA KABLA MTOTO HAJABATIZWA SHARTI AAMINI KWA MOYO WAKE WOTE.Maswali ya Kujiuliza:-
      1.  watoto wanaamini wenyewe Tena Moyo wote ? Au wanaaminishwa?
      2. Je kitoto kichanga ambacho hakiongei kinaweza kuamini?
      3. Lakini hatua ya pili Sharti mtoto atubu. Swali Je mtoto mdogo, kichanga kinaweza kutubu?
      4. Mtoto mdogo anaweza kujutia dhambi yake?

Yawezekana unapanga kumbatiza mtoto wako ubatizo wa kunyunyizia, Yawezekana ulibatizwa ubatizo wa kunyunyizia Tena ukiwa mtoto bila hiari yako, Tena Yawezekana umekuta una cheti cha ubatizo Lakini ulipobatizwa haukumbuki. Rafiki yangu nataka nikuambie kuwa huo ni uongo wa Shetani, ulio kinyume na Maandiko, maana kazi ya Ibilisi ni kuudanganya ulimwenguni. Biblia Inasema "Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote." (Ufunuo 12:9).
Mpokee Yesu na Kubatizwa ubatizo sahihi wa biblia Tena wa KUZAMISHWA NDANI YA MAJI MENGI , Tena iwe ni baada ya kuamini Bila kuaminishwa.

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.