Header Ads

NGUVU ILIYOMO KWENYE MAOMBI(..mwendelezo)


maombi yangu
MWENENDO WAKO KATIKA HUO ULIMWENGU UNAOPELEKA MAOMBI YAKO.
Kila ufalme unajengwa kwa mila desturi ,masharti na sheria ili uweze kusimama. Ulimwengu wa giza una-miiko yake, pia na ulimwengu wa nuru pia una-miiko yake katika ufanyaji kazi na hivyo ndivyo ulivyojengwa. Ili uenende kwenye ulimwengu kuna masharti ya kiujumla au sharia, na pia kuna masharti ya jamii moja na jamii nyingine.
Mfano jamii ya waganga wa kienyeji iko tofauti na jamii ya wachawi ingawa ni wamoja. Lakini kazi zao zinawafanya wawe tofauti kimiiko ya kiutendaji. Vivyo hivyo mitume na waalim na wao pia wanamiiko ya kiutendaji, haimaniishi kuwa kazi zake mtume haziwezi kufanana na mwalimu au mchawi hawezi kufanana na mganga, hapana hata kidogo.

Kwa maana ufanano wa kazi unajengwa na nguvu inayoshuka kwenye madhabahu wanayotumia kwenye maombi. Wasipoweka miiko huo ufalme utafitinika. Kama ilivyoandikwa “Kila ufalme ukifitinika juu ya nafsi yake, hufanyika ukiwa; tena mji au nyumba yo yote ikifitinika juu ya nafsi yake, haitasimama. Na Shetani akimtoa Shetani, amefitinika juu ya nafsi yake; basi ufalme wake utasimamaje?” (mathayo12: 24-27).

Kwahiyo ili uwe na nguvu kwenye ulimwengu wa roho inatakiwa kushika vizuri masharti ya huo ufalme unaotumika. Mfano ulimwengu wa NURU  ukitumia madhabahu ya walokole unakuta kuna kunena kwa lugha. Mtu anayenena kwa lugha hawezi kufanana kwa nguvu wakati wa kuomba na ambaye haneni kwa lugha.
Au mfano mwingine mchawi hapandi cheo pasi na kuvuka baadhi ya mitihani na pia kuna vyeo kupewa kwenye ulimwengu wa giza mpaka uwe wamekuamini sana. Halikadhallika na kwenye taasisi zetu za kawaida kwenye ulimwengu wa nyama kawaida.

Kwa ulimwengu wa nuru kwenye madhabahu ya wakristo sheria ziko wazi kwenye biblia na msharti yako ndani pia. Ukitaka uwe na nguvu zaidi mda wa kuomba inatakiwa uombe mda mrefu tena kwa mpangilio na siyo kuomba tu. Pia omba kwa kunukuu vifungu vya biblia kwenye aina ya maombi yako kama tulivyokishwa jifunza kwenye   CHRISTIAN  CULTURE.

kwa maana kutoka kwenye utangulizi wa hili somo tuliona kwamba kuna prayers na requests sasa unapopeleka “requests” hakikisha ziko kwenye mpangilio(definite) ili zikubaliwe la sivyo utakuwa unapayuka(speaking in vain). Soma AMPLIFIED BIBLE philipians 4:6 na mathew 6:7

Pia inatakiwa uache uovu  wote, kama ilivyoandikwa “Kila alitajaye jina la Bwana na auache uovu” (2Timotheo 2:19). Kwamaana uovu hautakiwi kutajwa kwako waefeso 5:3 Lakini uasherati usitajwe kwenu kamwe, wala uchafu wo wote wa kutamani, kama iwastahilivyo watakatifu;. Pia anza kufanya kazi ya MUNGU(JEHOVA YIRE). Kama tulivyokwisha ona kwenye MILANGO YA KUVUKA KABLA HUJAFA.

Hapo ndipo nguvu zako na mwenendo wako kwenye huu  ulimwengu utakapokubaliwa na kuwa mwenye nguvu na maombi yako ndivyo yatakavyokuwa yanajibiwa upesi zaidi. Maana “tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka”( mathayo11:12).  

Wiki ijayo tutaangalie moja kati ya zile zilizosalia. MUNGU muumba mbingu na nchi akubariki sana  

Mwandishi: MICHAEL BASA 0765 279 698 , +255 789 799 199

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.