Header Ads

KITOKEACHO MTU AKIZINI



Ni vitu gani humpata mtu anapozini? 
Kwanini hadi Mungu atofautishe kati ya uzinzi na dhambi nyingine? Hadi Mungu anasema “Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe” (1kor 6:18).  

Kunanini hasa?

Kwanza; unapoenda kuzini unaenda kupokea mapepo yote yaliyo kwa huyo mtu unaezini naye. Na kwakuwa tendo hilo ni agano la Damu; mwili wako na wa huyo unaezini naye inaunganishwa na kuwa mwili mmoja. Hivyo mapepo yanakuwa na haki kukaa kwa wote wawili.
Kwahiyo kama mtu ana pepo la ukahaba, nawe ukizini nae unajikuta nawewe unafanya ukahaba hata kama huendi sehemu za kujiuza. Ndio hao watu walio wengi sana wanaobadilisha mahusiano kila baada siku au miezi kadhaa. Ndio maana imeandikwa “Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye?” (1kor 6:16). Kama huyo unaezini nae anayo matatizo kama kutokuoa/kutokuolewa, kutofanikiwa, na nuksi; nawe hayo yote unayapokea kama yalivyo
Watu wengi wanapozini siku ya kwanza kabisa, huwa wanajichukia sana na kukasirika na kujutia sana. Na moiyoni mwao hujiona wamepoteza kitu cha thamani sana. Hadi unajiapiza moyoni unasema “sitarudia tena kufanya jambo hili”. Lakini baada ya siku au mwezi mmoja tu hujikuta unatamani sana kufanya uzinzi… na tena unajikuta sasa huwezi kabisa kujizuia.. hii ni kwasababu ya hayo mapepo uliyoyapata siku ile ya kwanza ulipozini… ndio hao watu ambao wakijua kama rafiki yao hajawahi kufanya mapenzi humuuliza “unaishije”?... Hii ni kutokana na wao sasa kumilikiwa na nguvu za mapepo ndani yao kiasi kwamba wao haiwezekani kuishi bila kuzini.
Unapoenda kuzini ni kwamba unajaribu kuvunja agano la damu ya Yesu kwa kufanya agano lingine la Damu na Shetani kwa njia ya Uzinzi. Sasa imeandikwa “Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa kwayo kuwa ni kitu ovyo, na kumfanyia jeuri Roho wa neema? (ebr.10:29)
Nakumbuka mimi na rafiki yangu mmoja tukiwa form six wote tulikwa mabikira… mimi nikaja SUA na kabla sijazini Mungu alinirehemu, akaniwahi, na Yesu akaniokoka nikawa nimeokoka. Lakini mwenzangu yeye alienda Chuo kingine, hakuokoka, na huko akafanya uzinzi… siku moja akaweka picha yake facebook na nilipoiona ile picha nikahisi uharibifu wa nafsi yake. Na baadae bila kumuuliza kwavile alikuwa rafiki yangu akaniambia kwamba alishazini…
Unapozini, nafsi yako pia huharibiwa; Baada ya mtu kuzini kwa mara ya kwanza, nafsi yake huwa twisted na hivyo huwa na tabia au sifa fulani ambazo sio zake kabisa. Uzinzi huharibu personality yako na ku-corrupt true identity ya nafsi yako… kama ilivyoandikwa “Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake” (mithali.6:32).
Uzinzi huambatana na kupoteza kabisa hali ya uthamani wa utu wako wa ndani. Hapa wadada wengi sana (kasoro wachache sana), huanza kuvaa nguo za kikahaba na suruali zinachora maungo yao baada ya kupoteza bikira zao. Hawana aibu tena wala hawaoni haja ya kujitunza, kuisitiri na kuiheshimu miili yao tena, maana tayari wameshapoteza thamani ya utu na wasifu wao wa ndani.
Kibaya ni kwamba huwezi kuitibu nafsi yako au kijitoa kwenye hayo maagano ya damu na nguvu za mapepo Kirahisi. Dawa yake ni moja tu; Umpokee Yesu ili kuyavunja hayo maagano kwa Damu ya Yesu kwa kumpokea Kristo awe Bwana na Mwokozi wako. Kuokoka sio Dini wala kuhama Dhehebu. Kuokoka ni Kuzaliwa mara ya pili yaani born again (yoh.3:3-6), ni kupokea ondoleo la Dambi na kuwa kiumbe kipya (Tit 3:4-6). 

Merry Christmass.

Mwandishi; Nzunda Ibrahim (0754 210 627 / 0785 360 577)

Download Mafundisho haya Hapa!

Maoni 2

TANZANIA AGRONOMY SOCIETY alisema ...

ahsante kwa somo lako basaministry endelea kutoa masomo engine zaidi

Michael Basa alisema ...

karibu sana mkuu

Inaendeshwa na Blogger.