Header Ads

MTOTO KAZALIWA KWETU

Wengi wamekuwa wakisherehekea sikukuu ya christmass kama ukumbusho wa kuzaliwa kwa mwokozi wa ulimwengu huu ambaye ni YESU Kristo. Lakini wengi wao huwa wanafurahia siku tu kwa kunywa na kula kwa tamaa zao wenyewe. Kaa hata dakika moja ujiulize “kwanini YESU alizaliwa”? 

Na je baada ya kuzaliwa aliagiza nini? Na je unayashika? Hii sherehe ya kukumbuka ni ya siku moja tu, lakini kuna siku ambazo unatakiwa ushike maagizo na kuyatenda . Basi leo hebu jikumbushe kabla ya hiyo siku ili uwe ni mwenye kufahamu kivipi unaweza kusherehekea kwenye kusudi la MUGU na kudumu katika hilo.
 

Tunaona kwenye isaya 9:6 mtoto mwanamume kuzaliwa ambaye ni utambulisho wa MUNGU kuwa pamoja nasi . Hili ni pendo ambalo MUNGU analitoa kwaajili ya binadamu wote kama ilivyo katika yohana 3:16. Kwa hiyo kuzaliwa kwa YESU hapa duniani ni kitambulisho cha kuja kwa wokovu kwa wanadamu wote bila kubagua rangi wala kabila.
 

Kwahiyo kuna mitume na manabii wengi wamekuja, lakini Duniani kuna Mwokozi mmoja tu na ndiye Bwana wa wote yaani YESU. 

Kama ilivyoandikwa “Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.” (Mdo.4:12)
 

YESU anajieleza kuja kwake duniani ni kwa ajili ya kuleta uzima wa milele na pia wanadamu wawe nao tele. Leo tunapokumbuka kuzaliwa kwa YESU, je tunakumbuka pia ni kwanini alizaliwa? Je, tunakumbuka hata kwa siku hiyo moja tu kujiuliza “uzima wa milele ni nini”? je YESU aliuleta ili ufanye nini kwetu?
 

Pia tusiishie hapo tu; hebu fikria siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake unapotoka kuzini au unapotenda machukizo mbele za BWANA . je ile thamani hasa ya MUNGU kumtoa mwanawe wa pekee aje duniani inakuingia akilini?. Basi ndugu kwa neema na rehema zake MUNGU nakuomba kama bado hujajua ni kwanini YESU alizaliwa hebu badilika sasa ufuate kusudi la MUNGU la kuja kukaa na wewe duniani ili akuokoe kutoka kwenye moto wa milele.
 

Kumbuka,
“Kutomchagua YESU, ni automatically kumchagua Shetani, kutochagua uzima wa milele ni kuchagua moto wa milele. Kutochagua mbingu ni kuchagua kuzimu”. Hivyo ndugu usijidanganye kwa kutofanya maamuzi sasa ukizani uko salama. Hakikisha Jina lako linaandikwa kwenye kitabu cha uzima. kwani imeandikwa “iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto” (ufu.20:15). Sikuukuu Njema sana.

Hakuna maoni

Inaendeshwa na Blogger.