Kijana mmoja mpole aliyekuwa na haiba ya uoga wa
kupindukia ambaye mwanzo alikaa katika hali ya mateso mengi sana kutoka kwa
jamii iliyomzunguka ambayo ilikuwa inatawaliwa na nguvu ya mfalme mmoja ambaye
hakuwa na chembe ya huruma hata kidogo. Alipotoa amri ya hakuna kulala watu
wote walitii na aliyekaidi alimwadabisha bila huruma. Alikuwa na askari maelfu
waliomsaidia huyu mfalme asiyekuwa na huruma kwa wannchi wa nchi ile. Viongozi
wa hayo majeshi walikuwa sita ambao walisifika sana kwa kutoa adhabu barabara
kwa wote waliokaidi kutii amri ya mfalme. Viongozi hao ni
- Hofu
- Umasikini
- Kutotii
- Ujinga
- Maradhi
- Usaliti
Hawa viongozi wa majeshi walikuwa na vikosi
vyenye nguvu kila mmoja. Ambapo waliweza kufanya kazi na vikosi kwa kujitegemea
au kuungana kwaajili ya kupambana na himaya iliyotaka kujiinua kinyume na
mfalme wao. Hii ilisababisha watu wa miji mbali mbali kuwa vibaraka watiifu
kwahuyu mfalme. Mfalme alipotoa amri watu walitii, hata waliopinga
walihakikisha mioyo yao tu ndio inapinga lakini miili ilitenda sawa sawa na
mfalme alichotaka tena bila kusitasita. Kwasababu ya watu wengi kuishi kwa
miaka mingi katika hali hiyo ilifika kipindi wakazoea na wakaona ni mfumo
kamili wa Maisha ambao bila huo hakuna Maisha tena. Miaka mingi baadaye kijana
mmoja alizaliwa kwenye Maisha ya kimaskini sana ambayo kwa wakati huo yalikuwa
ni Maisha ya kawaida sana kwa jamii na hakuna aliyekuwa anaweza kukusema wala
kukushauri. Kijana yule alipewa jina BASA na BABA yake na alikua katika
mazingira yale yale na majeshi yalikuja kuzunguka kijijini kwao na mwenyewe
alijionea mateso makubwa watu waliyoyapata. Akaazimu moyoni mwake atakapokua
mtu mzima lazima aje awakomboe hawa watu kutoka kwenye mateso yale. Baada ya
miaka 25 baade kijana aliamua kuanza harakati lakini akagundua kuwa katika mji
ule wote waliosoma walikuwa wengi ni waongo{wanafiki} na wamezibwa midomo
kwamaana kusema kinyume na mfalme basi lilikuwa ni kosa kubwa na wote walilijua
hilo na wao waliamini hivyo. Mtu alipotaka kufanikiwa kwa elimu ile basi
alitakiwa asome kwanza elimu ya mfalme yule na upate baraka zake ndipo usome
elimu zingine. Ambazo pia kwa asilimia 90 aliziandika mwenyewe kwa kuweka kile
alichoamini ni bora kwa wananchi wake na kitamsaidia katika kuwaongoza kwa
utulivu. Katika kutafuta elimu ya kuwakomboa hawa watu kijana BASA alienda kwa
mfalme mwingine ambaye watu wa taifa lake walikuwa ni bora katika mambo yote.
Katika taifa lile kulikuwa na jeshi imara sana ambalo kiongozi mkuu wa majeshi
yale aliitwa EMMANUEL. Huyu alikuwa ni mtumishi mkuu sana kwenye ufalme huu na
mwingine aliyemfuatia kwa madaraka alijulikana kwa jina la HOLLY.
inaendelea.....
mwandishi: Prop,Mwal: Michael Basanorare 0765 279 698, +255 737 919 561
Hakuna maoni
Chapisha Maoni