Jumatano, 31 Agosti 2016

UBATIZO

Kwanini nibatizwe? Ubatizo upi ni sahihi kibilia?. Ni wakati upi na nani anatakiwa kubatizwa? Je, ni kabla ya kupokea wokovu au baada? Faida zake ni zipi? .

Kwanza kabisa; kuna batizo zitokazo kwa wanadamu na pia upo ubatizo unaotoka kwa Mungu. Tunajua hili kutokana na Yesu alipowauliza makuhani na wazee wa Israel kwa Kusema “Nitawauliza neno moja, nanyi mnijibu, kisha nitawaambia ni kwa mamlaka gani nayatenda haya. Ubatizo wa Yohana ulitoka mbinguni, au kwa wanadamu? Nijibuni” (Mk.11:30-32).

Kutoka hapo tunajuwa kumbe ubatizo ule wa Yohana ulitoka Mbinguni. Pia kabla ya Yohana Mbatizaji, kulikuwa na aina mbalimbali za batizo ambazo hazikuwa kama ubatizo wa yohana. Hii ni kutokana na swali ambalo watu kadhaa waliulizwa na mtume Paulo kwa kusema “Basi mlibatizwa kwa ubatizo gani? Wakasema, Kwa ubatizo wa Yohana” (matendo,19:3). Hivyo kutoka hapo pia tunajua kumbe hata wakati wa mitume kulikuwa na batizo aina mbalimbali zilizoletwa na wanadamu
Kabla Yesu hajaondoka duniani, naye alikuwa anabatiza watu kupitia wanafunzi wake. Na aina ya Ubatizo aliokuwa anautumia ulikuwa ni ule uliotoka Mbinguni ulioletwa kwa mkono wa Yohana. Kama ilivyoandikwa “Baada ya hayo Yesu na wanafunzi wake walikwenda mpaka nchi ya Uyahudi; akashinda huko pamoja nao, akabatiza” (yoh.3:22,10:40). Na huu ndiyo ubatizo sahihi kibibilia ambao Yesu aliowaachia wanafunzi wake mpaka leo.

Sasa Ubatizo wa Maji Mengi huu wa Yohana Mbatizaji Mungu ameuweka ili kwa Njia hiyo nawewe ushiriki kifo cha Yesu kwa kufa pamoja naye na kufufuka pamoja naye kwa njia ya kuzamishwa na kuinuliwa katika maji. Kama ilivyoandikwa “sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake” na tena “tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima”. na tena “Mkazikwa pamoja naye katika ubatizo; na katika huo mkafufuliwa pamoja naye” (Rum.6:3-6, Col.2:12). Hivyo tunaona kumbe unapobatizwa, mambo halisi hufanyika wala sio ishara tu.

Siku unayo-batizwa kwa maji mengi ndiyo siku ambayo 1) unakufa pamoja na Kristo msalabani. 2) unafufuka pamoja na Yesu mautini. 3). Unapokea Uwezo wa kuenenda katika hali ya “upya wa uzima” alionao Yesu sasa. 4) unakuwa umetimiza haki yote. Maana imeandikwa “mshahara wa dhambi ni mauti”. Na kwasabu wewe hapo mwanzo ulikuwa mdhambi… Unahukumiwa mauti pamoja na Yesu kwa njia ya msalaba na mauti yake. Hivyo hutahukumiwa mauti ile siku ya kuuhukumu ulimwengu wote (yohana.5:24)

Tunajuwa kuwa Yesu aliposulubiwa msalabani hakufa muda uleule; bali alisulubiwa saa tatu lakini akafa saa tisa (Mk. 15:24,34). Vivyohivyo Kuokoka maana Yake ni kuzaliwa mala ya pili kunako ambatana na kupokea utakaso wa dhambi zote na kunyweshwa ua kumpokea Roho Mtakatifu ndani yako aishi nawe milele. Na kwasababu hiyo wewe unakuwa kiumbe Kipya uliye Mwana wa Mungu, uliye mtakatifu na uzima wa Milele unakuwa ndani yako. Kama ilivyoandikwa “alituokoa;…, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa mara ya pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu”, na tena “Yeye aliye naye Mwana, anao huo uzima; asiye naye Mwana wa Mungu hana huo uzima “(tito.3:4-7, 1yoh.5:12).

Kwahiyo mtu huyu alie-okoka anakuwa amezaliwa mara ya pili na amesulubiwa msalabani pasipo kuzikwa utu wake wa kale na kufufuka pamoja na Yesu. Kama ilivyoandikwa “hao walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake” (gal.5:24). Hivyo utu wake wa kale unakuwa bado haujazikwa, kwasababu utu wa kale huzikwa katika ubatizo wa maji mengi.Kwahiyo kama hujabatizwa atakuwa kwenye vita kali daima kati ya roho yako na mwili wako mpaka pale atakapouzika huo utu wako katika ubatizo.

Hivyo haijalishi wewe umeokoka miaka mingi kiasi gani. Lakini pasipo ubatizo wa maji Mengi bado haujakamilika. Hauja-itimiza haki yote. Kwani kumbukumbu za wewe kufa na kufufuka pamoja na Kristo hazipo mbele za Mungu mpaka utakapo kubali kubatizwa kwa ubatizo wa Maji mengi. Usitegemee ubatizo wa kunyunyizia kichwani kwani kwa huo haiwezekani kushiriki mauti na ufufuo wa Yesu Kristo. Kama inavyosema “Mkazikwa pamoja naye katika ubatizo; na katika huo mkafufuliwa pamoja naye”.

Siku unayobatizwa ndiyo siku unayozika utu wako wa kale na kuhukumiwa mauti pamoja na Yesu msalabani ili siku ile ya hukumu usije ukahukumiwa mauti kama wengine ambao wao watahukumiwa mauti. Maana imeandikwa “tumehukumu hivi, ya kwamba mmoja alikufa kwa ajili ya wote, basi walikufa wote” (2Kor.5:14). Kwahiyo huo ubatizo wa Kuzamishwa kwenye maji ni ili uunganishwe na Yesu katika mauti na uzima wake. Ukibatizwa unafanya “final separation from the world”.
Mtu anatakiwa kubatizwa baada ya kupokea wokovu kwanza na sio kabla ya kuamini (Mk.16:16). Maana sababu nyingine ya kubatizwa ni matokeo ya utii yathibitishayo kuwa dhamiri zako zimefanywa upya. Kama ilivyoandikwa “ubatizo, unaowaokoa ninyi pia siku hizi; .., jibu la dhamiri safi mbele za Mungu, kwa kufufuka kwake Yesu Kristo” (1pet.3:21). Sasa jibu la dhamiri haliwezi kuwepo kwa mtoto mchanga kimwili, kwasababu mtu anapo-okoka (born again) ndipo anatakaswa dhamiri zake na kuanza kuzichukia dhambi alizokuwa anazitenda kabla, na roho yake huanza kuumia akiziona dhambi (ebr.9:14, 2pet.2:8)

“utashiriki vipi mauti ya Mwanangu Yesu kwa kunyunyiziwa maji kichwani? Niambie, Je, kwa kunyunyiziwa maji utatimizaje neno langu lisemalo “Mkazikwa pamoja naye katika ubatizo; na katika huo mkafufuliwa pamoja naye”?. “kama vile ambavyo haikuwezekana Mwanangu afe bila kwenda ndani ya nchi chini; vivyohivyo nawewe haiwezekani kushiriki mauti ya Mwanangu pasipo kwenda ndani ya maji”. kwa kubatizwa Yesu ndani ya maji, akatia mhuri na kutangaza mauti na ufufuo wake jinsi utakavyokuwa. Hivyo nawewe imekupasa kuenenda kwa jinsi hiyohiyo.
Laana na magonjwa ya kurithi hukaa na hupata kibali kutokana na wewe kuwa na utu wa kale. Lakini unapobatizwa hayo yote huzikwa na hayawi na mamlaka tena kwani unakuwa “katika upya wa uzima” (rum.6:4). Baada ya kuokoka nilikuwa nabisha sana. Hadi Mungu mwenyewe aliposema na mimi. Na baaada ya kufunuliwa tu bila kuchelewa nilienda nikabatizwa kwa maji mengi. Hivyo hata wewe unaweza ukaenda ukabatizwa bila kuhama hilo dhehebu lako. Nenda Kabatizwe usifungwe na udhehebu ukakosa ufalme.

Sio dhambi, na sio ukosefu wa imani kuamua kubatizwa kwa mala nyingine kama ukigundua ubatizo wa kwanza huakuwa kama neno linavyotaka. Hata mimi nilitumia hoja kama hiyo kukataa kubatizwa kwa maji mengi kwa kusema “nilibatizwa tayari tangu mtoto”. Lakini Bwana akasema “mbona kwenye Matendo 19:2-5 mtume Paulo aliwabatiza mala ya pili watu kadhaa waliokuwa wamebatizwa na yohana mbatizaji?”.

Hautakiwi kubatizwa kama hujapokea wokovu kwanza. Kibiblia mtu haokoki kwa kubatizwa kwa maji. Unapokea wokovu kwanza ndipo unaenda kubatizwa. Mtu asikudanganye kwa kusema siku unayobatizwa ndiyo unayozaliwa mala ya pili- Huo ni uongo. Ukibatizwa kabla ya wokovu ni sawa na mtu anae-oga tu.

Kama kweli wewe ni mteule wa Mungu; Jambo hili la ubatizo hutakuwa na amani nalo mpaka utakapokubali na kutii kwa kwenda kubatizwa. Ndipo moyo wako utakapotulia. Maana Mungu hawezi kumtumia mtu “to the full” kama bado hujabatizwa. Yesu anasema “Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu”(Yohana.3:5). AMINA.
Mwandishi: NZUNDA Ibrahim (0754 210 627)

Jumamosi, 27 Agosti 2016

MWONGO NI NANI?

Wengi wanasema; “haijalishi kama wewe ni dini gani, au unafuata njia gani… Mungu ni mmoja… kwahiyo kama unamwabudu Mungu halisi na unatenda mambo mema huko uliko… siku ya mwisho hautahukumiwa”. Je, hii ni kweli au uongo?

Imeandikwa “Je, mwongo ni nani? Mwongo ni mtu yule asemaye kwamba Yesu si Kristo. Mtu wa namna hiyo ndiye MPINGA KRISTO, yaani, yeye humkana Baba na Mwana. Hakuna yeyote amkanaye Mwana aliye na Baba.” (1yohana.2:22-23). Pia Kristo anasema “Mimi ndimi njia na kweli na uzima. Mtu hawezi kuja kwa Baba isipokuwa kwa kupitia Kwangu” (Yohana.14:6). Kwahiyo njia ni moja tu, na imani ni moja tu, yaani Yesu basi. Njia nyingine zote ni za upotevuni (njia pana).

Hii pia ni kwa kila mtu anaetumia majina mengine ili kupata msamaha wa dhambi kutoka kwa Mungu. Yesu anasema “Nanyi mkiomba lo lote kwa Jina Langu, hilo nitalifanya, ili Baba apate kutukuzwa katika Mwana. Kama mkiniomba lo lote kwa Jina Langu nitalifanya” (Yohana.14:13-14, 15:16, 16:23-28) Pia imesisitizwa kuwa; “kama mtu yeyote akitenda dhambi, tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo Mwenye haki. Yeye ndiye dhabihu ya upatanisho kwa ajili ya dhambi zetu, wala si kwa ajili ya dhambi zetu tu, bali pia kwa ajili ya dhambi za ulimwengu wote” (1yohana.2:1-2).

 Hatuna dhabihu wala mwenye haki zaidi ya Yesu kwahiyo nikisema “Mt. Petro au Maria utuombee sisi wakosefu” badala ya “Yesu utuombee sisi wakosefu”; ninakuwa nimepotea kabisa na hiyo ni ibada ya mizimu, kwani wapagani wote hutegemea wafu badala ya Yesu aliye hai.(Isaya.8:19). Sisi ni makuhani(ufunuo.1.5-6), na Kristo ndiye Kuhani wetu Mkuu(waebrania.5.1-10). Sasa ni upotevu ulioje kwa kuhani kumwacha kuhani Mkuu aliye hai na kwenda kwa wafu?

  Pia wote wanaosema “hakuna wokovu duniani” wanatenda dhambi ya kumfanya Mungu mwongo na kwamba hakumleta mwanae ili atuokoe (1yohana.5:9-10). Imeandikwa “tazama,wakati uliokubalika ndiyo sasa; tazama siku ya wokovu ni sasa” (2korintho.6:2) Vile vile; Dini au dhehebu au mtu yeyote anaehubiri injili nyingine zaidi ya injili ya Kristo, yeye amelaaniwa kabisa (wagalatia.1:8-9, 1korintho.16:22).

Ndio maana Mungu alisema “Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Yeyote aaminiye na kubatizwa ataokoka. Lakini ye yote asiyeamini atahukumiwa.”(Marko.16:15). Kwahiyo kila mwanfunzi wa Kristo lazima ahubiri injili hata kwa matendo inatosha… la sivyo mtu huyo anachangia kupoteza wenzake.
Mwandishi: IBRAHIM J. NZUNDA 0754 210 627

Jumatano, 17 Agosti 2016

AINA ZA WAKRISTO NA TABIA ZAO

welcome to basa ministry
WAKRISTO Ni wafuasi au watu wanaomilikiwa na kristo Yesu ,yani wako ndani ya utawala wake,na kwa Mara ya kwanza neno wakristo lilitamkwa Antiokia  LAKINI hapo kwanza likiitwa kanisa/watakatifu
    matendo 11:26  ……Na wanafunzi waliitwa Wakristo kwanza hapo Antiokia
    yohana.   15:4
AINA ZA WAKRISTO
   Zipo aina tatu za wakristo nazo ni
         1.WA MWILINI          2.WACHANGA         3.WA ROHONI

TUANGALIE KWA UNDANI TUNAWEZA KUJIFUNZA KITU

1.WAKRISTO WA MWILINI
     Hawa ni wale waliookoka siku nyingi lakini maisha yao  hayabadiliki kutokana na uvivu wa kujifunza  waebrania 5:11-12
Huyu hata ukimhimiza kujifunza atakwambia"nilishayajua kabla hujazaliwa" lakini mtu mwwenye safari wa mbinguni hawezi kuwa hivyoo maaana hawezi kummaliza kumjua MUNGU wa kweli.
*SIFA ZAO*
1,anakuwa na sura mbili ya kanisani (utakatifu)na ya mitaani (kawaida) Tito 1:16
2,akikaa na watu wasio mjua Yesu ni vigum kumtofautisha 2timotheo 2:15
3,huona aibu kujitambulisha kama ameokoka  luka 22:54-60
4,ni mtu wa mizahaa
5,wakitukanwa hujirudishia
6,wepesi kukasirika wakolosai 3:8
7,hujisifu kwa miaka mingi walivyokaa wokovuni
8,hawapend kukemewa/ kuonywa wakikosea warumi 15:14, 1korintho 4:14,wakolosai 3:16
9,waongo sana  mith 26;19
10,ni kikwazo kwa wanaotaka kuokoka

2.WAKRISTO WACHANGA
     Hawa ni wale walio amin hiv karibun, hawa hupaswa kupewa maziwa yasiyoghoshiwa ili waukulie wokovu 1petro 2:1-2
*SIFA ZAO*
1,uwezo wa kupambanua JEMA na baya ni mdogo
2,chakula kigum hawakiwezi wanahitaj zaid kufundishwa kuhusu Yesu
3,hawana uwezo wa kujua kama majaribu ni kipimo cha imani (1korintho 3:1-2)
4,hawakosekani kukutwa na utu wa kale
5,hupenda kupewa kipaumbele na kutendewa
6,wokovu ni faida yake lkn hupenda kubembelezwa
7,kusoma neno na kuomba ni mpaka wakumbushwe

3.WAKRISTO WA ROHONI
     Hawa ni wakristo waliomwamini Yesu na hudum katika neno la MUNGU, likabadili maisha YAO nao wakafananana neno (Yesu) yohana 1:1-5   matendo 9:19-22
*SIFA ZAO*
1,Hujulikana kabla hawajajitambulisha yohana 19:38-42
2,Hakuna wanachokilinda zaidi   ufunuo 2:25 mithal. 4:23  yuda 1:3
3.Hakuna mzaha kwao  zabur 1:1-6
4,ni waaminifu katika yote
5,hawana roho ya kusengenya wala kunung'unika  wafilipi 2:14
6,hutoa kipaumbele kwa mambo ya MUNGU mathayo 6:33
7,huzaa matunda maana ndio kusudi la kuitwa kwao  mathayo 13:23
8,huongozwa na ROHO na wala hawamuhuzunishi  warumi 8:14 Galatia 5:16-26
9,biblia(neno)ni rafiki yao MKUU zabur 119:11
10,ni watetezi wa IMANI yao yuda 1:20  1petro 1:5-8
  
Yaani ukiona kuna maswali yanahusu imani yako na kuyajibu huwezi hadi aje mchungaji wako basi huna uwezo kwa nafasi hiyo  matendo 4:18-21 Marko.   5:25-32
Nategemea umejijua kuwa upo kundi gani kama la kwanza piga hatua ufike la tatu kama ni la pil pia piga hatua kufika la tatu  tunaujua kuwa kuna wali umepikwa kwa harufu yake maana wali unatabia ya kusambaza harufu
JICHUNGUZE TABIA ZAKO  NA  MUNGU AKUBARIKI

MWALIM DENISY 0759735473&0658316011

Mhariri Michael BASA 0765279698,+255789799

Jumapili, 14 Agosti 2016

KUMPENDEZA MUNGU (PLEASING GOD)

PLEASE=cause to feel happy and satisfied (oxford 11th edit) kwa Kiswahili ninaweza kusema inamaana ya kufanya ahisi (awe na) furaha na kujitosheleza. Kumbe kumpendeza MUNGU inatakiwa umfanye MUNGU awe na furaha na kujitosheleza. Kwa hiyo mtu akiamua kumtumikia MUNGU inatakiwa kujitoa kwa mwili wake ili iwe dhabihu ya kumfanya MUNGU awe na furaha na wewe na aridhike na kile unachokitenda ndani ya mwili wako (jumba la roho/ROHO) warumi 12:1-2. Somo la mwili linapatikana tayari pitia hapa kulisoma  na ia somo la utatu wa binaadam pitia hapa kulisoma ili kujua kwanini MUNGU alikupata mwili na katika warumi 12 anasisitiza kuitoa miili yetu kama dhabihu iliyo hai. Ili kujua maana ya dhabihu pia pitia hapa kuiona na kwa upande wa kafara pia bofya hapa kulisoma. Katika smo leo tutajikita kwenye roho/ROHO ikiwa ndani ya mwili na jinsi MUNGU anavyotaka kutokea hapo.

JE MATENDO YAPI AMBAYO ROHO NDANI YA MWILI IKITENDA HUMPENDEZA MUNGU??
 Bila utumishi uliotukuka mbele za BWANA wetu kamwe hatuwezi kumendeza MUNGU maana mtu akiuhurumia mwili wake hawezi kujitoa kwa ajili ya MUNGU. Roho wa MUNGU anataka wewe ufunge kwa ajili ya BWANA halafu wewe katika maisha yako yote haujawahi kufunga kwahiyo cha kwanza kufikria ni mwili kukosa chakula chako cha kila siku. Na ndip shetani atakukumbusha juwa juna vidonda vya tumbo. 

Ndio maana inatakiwa kuona mwili kama vazi ambalo MUNGU kakupa ili umtumikie na siyo ushindwe kwaajili ya vazi maana yeye mwili wako umejaa uharibifu na nia yake ni uadi juu ya MUNGU. Kwa hiyo mtu akiacha kula kwaajili ya MUNGU huyo ndiyo MUNGU atapendezwa naye.
Warumi 14:11&18 ‘’Kwa kuwa yeye amtumikiaye Kristo katika mambo hayo humpendeza Mungu, tena hukubaliwa na wanadamu. Mkiwezeshwa kwa uwezo wote, kwa kadiri ya nguvu ya utukufu wake, mpate kuwa na saburi ya kila namna na uvumilivu pamoja na furaha’’

MATENDO YENYEWE NI:-

      1}KUJUA MAPENZI YA MUNGU
    Watu wengi tunashinddwwa kumpendeza MUNGU maana hatujui mapenzi yake wala ya mwanaye aliyemtuma. Maana mapenzi ya KRISTO ni kufa msalabani ili kila mtu aokolewa kupitia yeye. Naomba uelewe kitu kimoja kwamba MUNGU alichofanya msalabani ni kujitoa kwa kila mtu kupitia roho wake ili kila mmoja amjue yeye katika kweli yote na kumtii yeye kama bwana na mfalme wake. Basi hakikisha unajengwa katika imani moja roho mmoja na ubatizo mmoja. Ili mapenzi ya MUNGU YATIMIZWE NDANI YAKO. WARUMI 11:6 

    Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale  Na wala MUNGU hawezi kukuacha maana siku zote atakuwa pamoja nawe
yohana 8:29 Naye aliyenipeleka yu pamoja nami, hakuniacha peke yangu; kwa sababu nafanya sikuzote yale yampendezayo.

    2}  KUYATENDA MAPENZI YA MUNGU
Baada ya kuyajua maenzi ya MUNGU BABA kinachofuata ni ukamilifu wa imani ndani ya kristo. Ili kuikamilisha imani inatakiwa kuanza kuyatenda maenzi ya mungu maana imani bila matendo imekufa. James 2:26 Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa. Kingine ni ibaada katika roho na kweli Hebrews 12:28 Basi kwa kuwa tunapokea ufalme usioweza kutetemeshwa, na mwe na neema, ambayo kwa hiyo tumtolee Mungu ibada ya kumpendeza, pamoja na unyenyekevu na kicho;

 3} KUJIVIKA UTAKATIFU NA KUTENDA MAAGIZO YOTE YA BIBLIA
Utakatifu ni kama vazi kwa mkiristo yeyote ambaye anasafari ya kumuona MUNGU muumba mbingu na nchi. Maana pasi na utakatifu imani si kitu wala dini zetu si kitu . ndio maana watu wanaohubiri wengi husema dini haimpeleki mtu mbinguni wala haikufanyi wewe umuone MUNGU bali dini ni kusanyiko la watakatifu ambao kwa umoja wao kama ilivyo desturi hukutana ili kumtafuta MUNGU wa kweli na kujifunza kwa umoja wao ili kufaidiana na kuzidisha upendo ndani yao. Lakini kama huwezi kuwa kumtakatifu huwezi kumuona MUNGU. Wakolosai 2:10 mwenende kama ulivyo wajibu wenu kwa Bwana, mkimpendeza kabisa; mkizaa matunda kwa kila kazi njema, na kuzidi katika maarifa ya Mungu; 1Petro 1:15 bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; waebrania 12:14 Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;

MATUNDA YA KUTENDA YALE YAMPENDEZAYO MUNGU
  •     Kujibiwa maombi yako  1yohana 3:21-22 na lo lote tuombalo, twalipokea kwake, kwa kuwa twazishika amri zake, na kuyatenda yapendezayo machoni pake
  •        Kuwa mwana wa MUNGU kweli
  •       Kumuona MUNGU waebrania 12:14
  •       Kuwa rafiki na ndugu wa YESU KRISTO mathayo 12:47-50
  •        Kuwa mrithi wa ufalme wa mbingu tito 3:7
Mwandishi MICHAEL BASA   0765 279 698,  +255 789 799 199

Alhamisi, 11 Agosti 2016

DHABIHU(sacrifice)

Defn
Nikitendo cha kutoa kitu chenye thamani kubwa kwa tegemeo la kupata kitu chenye thamani au umuhimu mkubwa kwako kama ishara ya ibada {Killing an animal or person and offering to GOD or gods} kutoka 10:25, 1wafalme 11:8,  zaburi 106:37. Pia katika somo letu la
NGUVU ILIYOMO KWENYE MAOMBI kipengele cha SADAKAAU KAFARA UNAYOTOA KWENYE HUO ULIMWENGU. Tulitazama kwa  upana hiki kipengele cha sadaka lakini kwenye hili tutazama kwenye ulimwengu wa nuru tu.  Unaweza kulipitia kwanza hicho kipengele ili Kupata mwanga kwanini tunatoa sadaka au dhabihu.

  •       Kwanini tunatoa dhabihu
  • ·         Kumuabudu MUNGU
  • ·         kutafuta amani na MUNGU kutoka 5:3,8:8 hesabu 7:19-25
  • ·         Kuvunja nadhiri numbers 15:3
  • ·         Kushukuru MUNGU 2nyakati 7:3&4,zaburi 50:14-23,zaburi56:12
  • ·         Kama sadaka mbele za MUNGU
  • ·     Kusafisha dhambi 1samuel 3:14 Zaburi 51:17 
Dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika; Moyo uliovunjika na kupondeka, Ee Mungu, hutaudharau.
        
KUNA AINA TATU ZA DHABIHU
  1.       YENYE NGUVU:-Ni ile ambayo mtu anatoa kilicho bora kutoka kwenye vile alivyo navyo
  2.      ILIYO SAFI:- Ni ile inayofuata sharia zote za biblia wakati wa kutoa dhabihu.
  3.     ILIYO HAI:- ni ile dhabihu ambayo kwa unayotoa ajili kufanya kazi ya MUNGU;hii hubaki inakushuhudia siku zote za uhai wako.

JE NI KWANINI LEO HATUTOI ZA DHABIHU ZA KUTEKETEZWA KAMA WANA WAISRAEL WALIVYOKUWA WANAFANYA???
Kwasasa hatutoi dhabihu kama wana waisrael walivyokuwa wanafanya ni kwasababu ya agano jipya ambalo mwana wa adam alikuja kuliacha.  waebrania 10:9-14,9:26
          Je kwasasa inatakiwa kutoa dhabihu za namna gani??
waebrania 13: 15 Basi, kwa njia yake yeye, na tumpe Mungu dhabihu ya sifa daima, yaani, tunda la midomo iliungamayo jina lake.
1petro 2: 5 Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo.


Mwandishi MICHAEL BASA   0765 279 698,  +255 789 799 199

Jumatatu, 8 Agosti 2016

NGUVU ILIYOMO KWENYE MAOMBI (..MWISHO)

 
BWANA ANAKUJA 
    
Baada ya kutazama vitu vitano muhimu wakati unapoamua kupeleka maombi yako juu ya madhabahu unayoitumia kuuufikia ulimwengu wa ROHO  katika hii sehemu ya tutaangalia sana ulimwengu wa nuru tu na ulimwengu wa giza hatutaugusa kabisaa lakini masomo yanayohusu jinsi ya kuushinda yatakuja kadri muumba atakavyonipa neema nawewe pia ukipewa neema yakusoma maana mpaka dakika hii sitaki mtu awaye mtu yeyote apotee kwa uzembe wangu bali kila atende kwa upande wake kwa bidii katika kumtafuta BWANA wa majeshi ili akaiponye nchi yake mwenyewe,familia yako, biashara yako, ndoa yako, na pia masomo yako. Vile vitano vya mwanzo ni vitu ambavyo mtu unaviishi lakini kuna vitu vitatu ambavyo vya kuwa navyo unavyoenda kuomba kwa mungu navyo vinapatikan katika 2nyakati 7:14 hapo unakuta vitu vitatu vya kuwa navyo ili kumwendea bwana ambavyo ni:-

basi tuitazame pia kujinyenyekeza inamaana ya kujishusha au kuiacha thamani yako na kuiona si kitu mbele za bwana muumba wako. Ambayo inakuwa imejengwa na mambo matatu nayo ni:-
  1.           kukubali kufundishika
  2.          kutii
  3.           kuwa na kicho(hofu)


hivi vitu vitatu mbele za bwana ni muhimu sana na vyote huanzia rohoni na kufikia kuviona nje kwa mtu ni baada ya moyo wake kuwa umejaa hivyo vitu nakuwa mmoja na vitu hivyoo ndio huyo mtu hata matunda ya roho unaweza kuyaona kwa wepesi kwake. Nje ya hapo utajijua wewe tu ukiwa unamtukia mungu bali watu wa nje hawawezi hata kulijua hilo. Hapa sizungumzii walokole nazungumzia mtu mwenye safari ya kwenda mbinguni kwamaana YESU alileta uzima wa milele ambao hakusema kuwa ni kuokoka bali ni kumjua MUNGU wa pekee na yesu kristo mwanaye aliyemtuma yohana 17:3.
                   Na pia haiishi hapo inatakiwa kujivika nila yake ili tuwe naye kweli lakini ili MUNGU asikuache inabidi kufanya yale yampendezayo kwamaana nyingine ili udumu katika uso wa bwana mungu wetu inabidi ufanye mda wote yampendezayo yeye. Ukisoma yohana 8:28-29 utakutana na neno wakati wa kufundisha yesu anasema neno siyo la kwake bali la kufundishwa na baba na akilisema au kulitenda naye baba anakuwepo mda wote naye ili kulilinda neno aliloagiza lisemwe au litendwe kwa jina lake. Unaweza usielewe kwa haraka lakini namaanisha mtazame YESU aliposema lolote muombalo kwa jina langu hilo nitalifanya. Lakini siyo kila mtu akitumia jina la yesu, yesu atatenda bali lazima uwe umeitwa kwa jina lake au umefanyika kuwa mwanafunzi wake . na ili akuhesabu hivyoo ataangalia ushikaji wako wa  maaagizo yake
           . Hapo ndipo njia mbaya nazo hutazamwa YESU aliweka kila kitu kiendacho kwa baba kipitie kwake yeye na hakuna njia nyingine na kama ukitumia jina jingine  kuomba kitu utakuwa unaomba kutoka kwa mungu wa ulimwemgu huu wala siyo mungu wa mbinguni aliyeumba mbingu na nchi 2wakorintho 4:4. Basi ndugu na rafiki yangu achana na njia zako mbaya naye MUNGU atakusikia na atakusamehe dhambi zako. Na ndipo macho yake yatafumbuka, na masikio yake yatasikiliza maombi yako 2nyakati 7:15&17. 
                    Kingine ni hofu ya kutenda dhambi inatakiwa itawale ndani yako maana utakuwa unaogopa kumkosea MUNGU na ndipo utaenenda vizuri. Na wala siyo kuogopa waumini wenzio maana hukumu nao ipo juu yao. Kwamaana kwa sheria wote tulihukumiwa kifo na mwanzo tulikuwa hapo wote. Bali ROHO alibatilisha kwa kutuhuisha kutoka uharibifu mpaka kutoharibika ambako ndiko kuwa na uzima wa milele. Basi pia tafuta kujazwa na ROHO WA MUNGU ndipo dhambi utaishinda na wala siyo kwa kushika sheria. Maana ashikaye sheria huyo ni mtumwa wa hiyo sheria bali sisi kwasasa ni watumwa wa YESU na malipo ni ROHO MTAKATIFU aletaye uzima wa milele ndani yetu.
MWISHO
MWANDISHI: MICHAEL BASA 0765279698 au+255 789 799 199

Alhamisi, 4 Agosti 2016

NGUVU ILIYOMO KWENYE MAOMBI(..mwendelezo)

IMANI YAKO JUU YA HUO ULIMWENGU.
Kila mtu anahitaji kuaminiwaau kuwafanya wengine kuwa na imani juu yake. Inaweza kuwa juu ya jambo Fulani analo weza kulifanya kwa usahihi. Watu huhitaji kuaminiwa na watu wanawaowazunguka ili:-
  1.        Aweze kufanya kitu pasi na kuingiliwa kimaamuzi
  2.       Amani ya kufanya kile anachowaza juu ya hao wamwaminio pasi na kuomba ruhusa.
  3.          Kuwa na amani juu ya hao wamwaminio.
  4.       Kuelezea kile alichofanya juu ya hao watu pasi na hofu ya kuwa inawezekana kukosea.

Mtu akiaminiwa anaweza kufanya vizuri kuliko akifanya huku anahofia kukosea. Kwasababu mtu akiaminiwa huwa anatumia kipaji chake cha ndani ambacho si rahisi kukiona bila kumpa nafasi na uhuru wa mawazo hapo ndipo imani juu ya huyo inatakiwa kuonekana. Imani huanza kidogo kidogo na baadaye hukua kutokana na matendo au faida anazopata kutoka kwa aamaniye.


Siyo ulimwengu wa nyama hata ulimwengu wa roho nao uko vivyo hivyo ndiomaana ukisoma Luka 17:6 Bwana akasema, Kama mngekuwa na imani (trust and confidence in GOD) kiasi cha chembe ya haradali, mngeuambia mkuyu (mulberry tree) huu, Ng'oka, ukapandwe baharini, nao ungewatii. Hata MUNGU mwenyewe ili afanye kazi kwako inatakiwa imani yako kumwelekea yeye iwepo na imani huwa haina shaka (kusita-sita) ndani. waebrania 10:38 Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; Naye akisita-sita, roho yangu haina furaha naye.

Kwa hiyo  Imani ni hakika ya mambo yatarajiwayo na nibayana ya mambo yasiyoonekana  waebrania 11:1. imani hujengwa na mda mwingine huharibiwa pia hubomolewa. Kwahiyo imani nikama kitu ambacho kinanguvu juu ya mtu yuda 1:20 Bali ninyi, wapenzi, mkijijenga juu ya imani yenu iliyo takatifu sana…. Iman Humjenga mtu kwa mitazamo, kiutendaji na kimazungumzo maana imani ya mtu ndio huujaza moyo wa mtu na kiujazacho moyo ndicho mtu hukitoa au hukisema. yakobo 2:26 Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa.

Imani hukua baada ya jambo ambalo lilikuwa ni tatizo kwa mtu/watu kutatuliwa kwa mfano imani ya watu wa karibu na YESU ilikuwa baada ya watu kumuona anatatua matatizo yao yanayowazunguka mfano. Kutoa pepo, kuponywa wagonjwa na kufufua wafu kwa kipindi hicho hakukuwa na watu wa kufanya hivyo. Ndiomaana mtu anafikia kutaka neno tu kwa YESU kwamaana kwa imani yake alijua hata akisema neno tu kitafanyika mathayo 15:25. 

Ili imani ikue inahitaji kuanzishwa au kujengwa. Imani hujengwa juu msingi nayo misingi ambayo imani imejengwa imetofautiana na ndizo hutofautisha kuamini kwetu. Kwamaana kuna imani juu msingi ambao ni kristo, waganga wa kienyeji, wachawi, mizimu, juu ya watu,juu ya kitu asichokijua. Imani inaweza kupimwa ndio maana mtu husema imani yangu ni ndogo juu ya hiki kitu.bas kama ndiyo hivyo bassi amini nami kuwa kipimo cha iamni kipo nacho ni AMANI. Imani hujengwa juu ya misingi bali vifuatavyo huisimamisha na kuikuza imani yako. Navyo ni elimu,mazingira, uzoefu juu ya jambo Fulani, utamaduni n.k . 

MWANDISHI: MICHAEL BASA 0765279698 au+255 789 799 199
Inaendeshwa na Blogger.