Jumapili, 26 Juni 2016

NGUVU ILIYOMO KWENYE MAOMBI(..mwendelezo)


maombi yangu
MWENENDO WAKO KATIKA HUO ULIMWENGU UNAOPELEKA MAOMBI YAKO.
Kila ufalme unajengwa kwa mila desturi ,masharti na sheria ili uweze kusimama. Ulimwengu wa giza una-miiko yake, pia na ulimwengu wa nuru pia una-miiko yake katika ufanyaji kazi na hivyo ndivyo ulivyojengwa. Ili uenende kwenye ulimwengu kuna masharti ya kiujumla au sharia, na pia kuna masharti ya jamii moja na jamii nyingine.
Mfano jamii ya waganga wa kienyeji iko tofauti na jamii ya wachawi ingawa ni wamoja. Lakini kazi zao zinawafanya wawe tofauti kimiiko ya kiutendaji. Vivyo hivyo mitume na waalim na wao pia wanamiiko ya kiutendaji, haimaniishi kuwa kazi zake mtume haziwezi kufanana na mwalimu au mchawi hawezi kufanana na mganga, hapana hata kidogo.

Kwa maana ufanano wa kazi unajengwa na nguvu inayoshuka kwenye madhabahu wanayotumia kwenye maombi. Wasipoweka miiko huo ufalme utafitinika. Kama ilivyoandikwa “Kila ufalme ukifitinika juu ya nafsi yake, hufanyika ukiwa; tena mji au nyumba yo yote ikifitinika juu ya nafsi yake, haitasimama. Na Shetani akimtoa Shetani, amefitinika juu ya nafsi yake; basi ufalme wake utasimamaje?” (mathayo12: 24-27).

Kwahiyo ili uwe na nguvu kwenye ulimwengu wa roho inatakiwa kushika vizuri masharti ya huo ufalme unaotumika. Mfano ulimwengu wa NURU  ukitumia madhabahu ya walokole unakuta kuna kunena kwa lugha. Mtu anayenena kwa lugha hawezi kufanana kwa nguvu wakati wa kuomba na ambaye haneni kwa lugha.
Au mfano mwingine mchawi hapandi cheo pasi na kuvuka baadhi ya mitihani na pia kuna vyeo kupewa kwenye ulimwengu wa giza mpaka uwe wamekuamini sana. Halikadhallika na kwenye taasisi zetu za kawaida kwenye ulimwengu wa nyama kawaida.

Kwa ulimwengu wa nuru kwenye madhabahu ya wakristo sheria ziko wazi kwenye biblia na msharti yako ndani pia. Ukitaka uwe na nguvu zaidi mda wa kuomba inatakiwa uombe mda mrefu tena kwa mpangilio na siyo kuomba tu. Pia omba kwa kunukuu vifungu vya biblia kwenye aina ya maombi yako kama tulivyokishwa jifunza kwenye   CHRISTIAN  CULTURE.

kwa maana kutoka kwenye utangulizi wa hili somo tuliona kwamba kuna prayers na requests sasa unapopeleka “requests” hakikisha ziko kwenye mpangilio(definite) ili zikubaliwe la sivyo utakuwa unapayuka(speaking in vain). Soma AMPLIFIED BIBLE philipians 4:6 na mathew 6:7

Pia inatakiwa uache uovu  wote, kama ilivyoandikwa “Kila alitajaye jina la Bwana na auache uovu” (2Timotheo 2:19). Kwamaana uovu hautakiwi kutajwa kwako waefeso 5:3 Lakini uasherati usitajwe kwenu kamwe, wala uchafu wo wote wa kutamani, kama iwastahilivyo watakatifu;. Pia anza kufanya kazi ya MUNGU(JEHOVA YIRE). Kama tulivyokwisha ona kwenye MILANGO YA KUVUKA KABLA HUJAFA.

Hapo ndipo nguvu zako na mwenendo wako kwenye huu  ulimwengu utakapokubaliwa na kuwa mwenye nguvu na maombi yako ndivyo yatakavyokuwa yanajibiwa upesi zaidi. Maana “tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka”( mathayo11:12).  

Wiki ijayo tutaangalie moja kati ya zile zilizosalia. MUNGU muumba mbingu na nchi akubariki sana  

Mwandishi: MICHAEL BASA 0765 279 698 , +255 789 799 199

Jumapili, 19 Juni 2016

NGUVU ILIYOMO KWENYE MAOMBI (mwendelezo/continuing)

SADAKA AU KAFARA UNAYOTOA KWENYE HUO ULIMWENGU.
Nakukumbusha kidogo kwenye somo letu la utangulizi kuhusu hili somo la "nguvu iliyomo kwenye maombi, kwamba tunaangalia maombi juu ufalme wa giza au nuru kwa watu unaowamiliki (wanaotumika).

Ili mtu aenende katika maombi ya ufalme wa roho kuna vitu vingi huhesabiwa kama sadaka(sacrifice) kwa Yule anayemuabudu, nazo zipo aina nyingi na zimetofautiana kwa uzito wake, na sadaka unayotoa ndio inayokufanya uzame kiasi gani kwenye huo ulimwengu. 

kiujumla (bila kujali ni kabla au baada ya Kristo), kuna sadaka kama za 1)mazao 2)fedha, dhahabu, shaba, 3)damu  4)nyimbo za kusifu, n.k.  kwa hizo sadaka ndipo uunganishwo wa kiroho hutokea bila kujali unamtumikia mungu yupi awe mungu mti , mungu kinyago, mungu allah au mungu yehova. 

kwamfano; Wale wa ulimwengu wa giza wanatoa sadaka zao kwenye madhabahu waliyoichagua, lakini pia na wale wa NURU wanafanya vivyo hivyo. Sadaka za mazao hutolewa kama shukrani kwa mungu wako baada ya kufanya kitu ulichokipenda au wakati unataka kufanya jambo fulani ambalo halihitaji nguvu kubwa ili litokee. 

Kuna mda sadaka hutumika kama kiunganisho cha baraka za ardhi na mtu katika ulimwengu wa roho. Maana ardhi ni chanzo cha vyote villivyopo ardhini, na maji ni chanzo cha uhai wote uliopo majini. 

kwenye mwanzo 4:3  imeandikwa "ikawa hatimaye Kaini akaleta mazao ya ardhi, sadaka kwa Bwana".Sasa ukitumia sadaka kama za unga hukufanya baraka zilizopo kwenye ardhi zikupate kwa haraka kuliko ukitumia fedha au damu ndio maana hata wana wa Israel walisisitizwa kutoa sadaka kwa MUNGU kwenye madhabahu maana alitaka kuwabariki kila watakapoiendea ardhi kwa kutafuta Baraka zao. 

Kwa upande wa fedha huwa inatumika kama shukrani baaada ya ulimwengu kukushuhudia na huwa inatolewa katika sehemu mbalimbali kama msaada kwa maskini, sadaka(offerings) ya madhabahuni, kutimiza matakwa ya ulimwengu au kwenye madhabahu kutoka25:1 -3 "Bwana akanena na Musa, akamwambia, Waambie wana wa Israeli kwamba wanitwalie sadaka; kila mtu ambaye moyo wake wampa kupenda mtatwaa kwake sadaka yangu. Sadaka utakayopokea mikononi mwao ni hii; dhahabu, na fedha, na shaba"

Mfano kwa mganga wa kienyeji huwa wanatoa hela ili kusoma uchumi wako na kuunganisha nyota yako na madhabahu ya huyo mganga. Ndio maana hutaka hata kama ni sarafu ili ikae kwenye ungo wake ambayo ndiyo madhabahu yake. 

Kwa upande wa sadaka ya damu, hutumika kwa agano(covenant) kwa ajili ya kuwa moja ya viumbe watiifu wa huo ulimwengu kutoka22:20 Mtu atakayemchinjia sadaka mungu ye yote, isipokuwa ni yeye Bwana peke yake, na angamizwe kabisa. pia  kutoka29:36 Kila siku utamtoa ng'ombe wa sadaka ya dhambi kwa ajili ya upatanisho; nawe utaisafisha hiyo madhabahu, hapo utakapofanya upatanisho kwa ajili ya hiyo madhabahu; nawe utaitia mafuta, ili kuitakasa.

Kinachotokea pindi mtu akiweka maagano inamaana anaweka uhai tofauti ulio ndani ya huyo kiumbe ili damu yake inapodai au kulia kwenye mahabahu, ilie kwa kutaja jina lako. Kwa hiyo jina lako litabaki pale linatamkwa na huo uhai wa kwenye hiyo damu. kama vile kuhusu damu ya Habili Mungu alivyosema "Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi" na tena kuhusu Damu ya Yesu akasema "Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya Habili"  (mwanzo 4:9-10, ebr `12:24)

Huo uhai  utaendelea kulia kwaajili yako mpaka huo uhai utakapokoma kuwa ndani ya hiyo damu. Damu  inaweza kuwa ya mnyama au ndege inategemea na ukubwa wa agano. Kadiri agano linavyokuwa kubwa ndivyo ukubwa wa kitu cha kumwaga damu unavyohitajika. Mfano;mtu aliyetoa damu ya kondoo ni tofauti aliyetoa damu ya kuku hata ikiwa ni kwenye madhabahu moja. Na damu ya mwisho kwa kuwa na thamani kubwa ni damu ya mwanadamu kwa maana yenyewe ina-uungu ndani yake lakini huwa haina nguvu ya kuwa sawa na MUNGU mwenyewe kwasababu ya dhambi. (ndiyo maana ilibidi Yesu azaliwe akiwa ametengwa mbali za dhambi tulizolirithi kwa adamu, ili awe kwetu dhabihu yenye Nguvu, isiyo na mawaa/dosari)

Kwa hiyo ukiwa kwenye madhabahu yako uliyochagua kwaajili ya kumwabudia mungu wako angalia ni nini unataka kutoa kwenye huo ulimwengu je sadaka inatakiwa au haitakiwi na kama inatakiwa ni kubwa kiasi na kwa uzito upi??

.
Wiki ijayo tutaangalie moja kati ya zile zilizosalia MUNGU muumba mbingu na nchi akubariki sana
Mwandishi: MICHAEL BASA 0765 279 698,+255 789 799 199

Jumapili, 12 Juni 2016

NGUVU ILIYOMO KWENYE MAOMBI( UTANGULIZI)

BASAMINISTRY
Maombi kwa wengi huwa ni kuongea na MUNGU kama ilivyoandikwa wafilipi 4:6 Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. lakini maombi kwa kiingereza huwa yamegawanyika sehemu mbili moja ni prayers naya pili ni requests. Kwa Kiswahili zote zinamaana ya maombi lakini request inaweza kuwa kuomba kwa mwanadam ili kutimiza uhitaji wako bali prayer ni kupeleka uhitaji wako kwa ulimwengu mwingine(ulimwengu wa roho) tofauti na huu unaoishi(ulimwengu wa mwili). Kwenye hili somo tutaongelea maombi ya ulimwengu wa roho ambao umegawanyika sehemu mbili nazo ni ufalme wa giza na ulimwengu wa nuru. Ulimwengu wa giza ndio una waombaji  kama wachawi, waganga wa kienyeji, wapiga ramli, wachanja chale, wezi,waabudu shetani au mizimu, freemason,  wazinzi wengine wenye matendo yasiyompendeza MUNGU. Na  ulimwengu wa nuru unawaombaji wake ambao wameitwa kwa jina la BWANA na wametiwa (kujazwa) roho wake yohana 14: 12 Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba.
 13 Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana.
 14 Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya. Hao wote hufanya maombi ili kufanikiwa katika shughuli zao au mahitaji yao. Ili kupeleka maombi lazima kuwe na madhabahu ambayo huchaguliwa na mtu mwenyewe ili kuongea na kiongoozi wa ulimwengu unaoutumikia. Na kila ulimwengu unamashariti yake ambayo huwa yamepingana na ulimwengu mwingine  waefeso:5 Maana neno hili mnalijua hakika, ya kwamba hakuna mwasherati wala mchafu wala mwenye tamaa, ndiye mwabudu sanamu, aliye na urithi katika ufalme wa Kristo na Mungu.
 6 Mtu asiwadanganye kwa maneno yasiyo na maana; kwa kuwa kwa sababu ya hayo hasira ya Mungu huwajia wana wa uasi.. Ili kuipata nguvu ya kutenda au kuumba kile anachotaka huwa ni kuongea juu madhabahu ili kiongozi wako wa ulimwengu wa roho akusaidie kutimiza kusudi lako. Lakini kaa ukijua kuwa mtu ana asili ya kiMUNGU ndani yake ambayo neno lake ndio huumba zaburi148: 5 Na vilisifu jina la Bwana, Kwa maana aliamuru, vikaumbwa.. Kwa hiyo kuomba huwa ni kutoa maagizo katika ulimwengu wa roho nini unataka kifanyike katika ulimwengu wako wa mwili kwa maana hata MUNGU mwenyewe alifanya hivyo. Kwa hiyo maombi ni siyo kwamba MUNGU ndio anafanya bali huwa ni kutoa maagizo katika ulimwengu wa roho kuwa unataka nini kifanyike kwenye ulimwengu wako unaoishi. Haraka ya kufanyika huambatana na:-
  1. Mwenendo wako katika huo ulimwengu unaopelekamaombi yako.(bofya link)
  2. Muungano wako na huo ulimwengu kwakila siku.(bofya link)
  3. Ushikaji wako wa maagizo ya huoulimwengu.(bofya link)
  4. Sadaka au kafara unayotoa kwenye huo ulimwengu.(bofya link)
  5.  Imani yako juu ya huo ulimwengu(bofya link) 
Watu wengi hatujibiwi maombi yetukwa wakati kwasababu hizo hapo juu tunashindwa kuzifikia katika maisha yetu ya kawaida. Nataka uelewe kuwa hizo sababu hapo juu inatakiwa uviishi au kwa maana nyingine viwe ni utamaduni wa maisha ya kila siku.


 mwandishi: MICHAEL BASA 0765 279 698, +255 789 799 199

Jumapili, 5 Juni 2016

TUJUE KUUWEZA MWILI

Mtu ni roho inayomiliki nafsi. Na mtu huyu akiwekwa ndani ya nyumba ya udongo yaani mwili anakuwa nafsi hai. (mwanzo 2:7). Binadamu nae yupo katika utatu yaani roho, nafsi na mwili. Kama ilivyoandikwa katika 1wathesalonike 5:23 “Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili”(UTATUWA MWANADAM PITIA HAPA)
Yaani kama vile mwili unavyomiliki  "kichwa" vivyo hivyo  roho nayo inamiliki "nafsi".  Kama vile kichwa chako na mwili vyote ni of the physical... vivyohivyo nafsi na roho vyote ni vya kiroho (ndio maana mtu akifa hajisahau yeye ni nani ingawa anaiacha "brain" yake kaburini).. (angalia luka.16:19-31)
Kwahiyo MWILI NI JUMBA LILOTENGENEZWA  KWA UDONGO ili KUTUNZA PUMZI YA UHAI (roho yako). Ndio maana mtu akifa maana yake ni kwamba roho yake inakuwa imeachana na mwili. Hivyo ukiomba mtu afufuke inamaana unairudisha roho yake katika mwili wake. Kama ilivyoandikwa “mwili pasipo roho umekufa (yakobo.2:26)”
Na kwakuwa mtu ni roho na sio mwili. Kinachoitwa “Mwana wa Mungu” sio mwili bali ni roho yako wewe. Na kwasababu roho yako haina asili ya kutenda dhambi imeandikwa “mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu (1yoh 3:9)”
Lakini kumbuka kuwa binadamu anazaliwa akiwa na asili ya dhambi katika roho na mwili wake. Sasa mtu anapookoka mwili wake huchukuliwa na kusulubiwa pamoja na Yesu pale msalabani. Kama ilivyoandikwa “hao walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake(gala.5:24)”.
Sasa pamoja na kwamba mwili unakuwa umesulibiwa lakini asili yake ya dhambi haitolewi katika mwili ila unakuwa umesulubiwa tu pamoja na Yesu pale msalabani. Ndio maana bado miili hii inazeeka na inakufa kwasabu ya ile asili ya dhambi ndani yake iletayo mauti. Imeandikwa “nia ya mwili ni mauti; bali nia ya roho ni uzima na amani. Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii”war8:6-7
 Kwa jinsi hii tunaona kuwa mwili waweza kutenda dhambi na hauwezi kutii sheria kwani bado unayo asili ya dhambi.  Na kwa muda huohuo roho yako haitaki kutenda dhambi kwani haiwezi kutenda dhambi kwasababu haina asili ya dhambi. Kama ilivyoandikwa “mwili hutamani ukishindana na roho, na roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka (gal.5:17)” na tena imeandikwa “Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho.(1pet.2:11)
Kwa hiyo tamaa za mwili na matendo ya kimwili yako tofauti na  ya roho yako ndani yako
JE MATENDO YA MWILI NI YAPI SASA?
WAGALATIA 5:
19 Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi,
 20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,
 21 husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.
Na kwa upande wa roho ni
WAGALATIA 5:

Na matendo/tunda la roho ni lipi?
22 Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,
 23 upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.

JE KUNA UHUSIANO WOWOTE KATI YA MWILI NA KUMTUMIKIA MUNGU????
NDIYO UPO
1WAKORINTHO 6:19; Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe
Kwa hiyo mwili ni hekalu la ROHO mtakatifu tuliyepewa na MUNGU lkn matendo ya mwili hayapo katika kumpendeza MUNGU
WARUMI 8:7.
8 Wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu.
Kumbe ili kumpendeza  MUNGU inabidi mtu asiiufuate mwili je njia zipi za kutoufuta mwili
KUMKIRI YESU
WAGALATIA 5; 24
WARUMI 8:10 Na Kristo akiwa ndani yenu, mwili wenu umekufa kwa sababu ya dhambi; bali roho yenu i hai, kwa sababu ya haki.

KUISHI KWA KUIFUATA roho/ROHO
WARUMI 8: 6 Kwa kuwa nia ya mwili ni mauti; bali nia ya roho ni uzima na amani.
9 Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake.
WAGALATIA 5;25 Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho.
KUTOUFUATA MWILI
WARUMI 8:5 Kwa maana wale waufuatao mwili huyafikiri mambo ya mwili; bali wale waifuatao roho huyafikiri mambo ya roho.
1PETRO1: 24 Maana, Mwili wote ni kama majani, Na fahari yake yote ni kama ua la majani. Majani hukauka na ua lake huanguka;
2PETRO2: 9 basi, Bwana ajua kuwaokoa watauwa na majaribu, na kuwaweka wasio haki katika hali ya adhabu hata siku ya hukumu; 10 na hasa wale waufuatao mwili katika tamaa ya mambo machafu. na kudharau mamlaka.
KUJUA DHUMUNI LA MUNGU JUU YA MWANADAM
1WATHESALONIKE4: 3 Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati;
1WAKORINTHO 6: 20 maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu.
KUJUA KUUWEZA MWILI
1WATHESALONIKE 4: 4 kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima; 5 si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua Mungu.

Mwandishi;  Michael BASA              0765 279 698, +255 789 799 199

Mhariri;       IBRAHIM J. NZUNDA  0754 210 627
Inaendeshwa na Blogger.