Jumatatu, 13 Novemba 2017

NJIA SABA ZA KUKUSAIDIA KUIACHA DHAMBI INAYOKUSUMBUA.

BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu. Karibu tujifunze Neno la MUNGU aliye hai.
Dhambi ni kosa la kwenda kinyume na utaratibu wa MUNGU.
Dhambi ni uasi kwa MUNGU.
Dhambi ni kulikataa kusudi la MUNGU.
Dhambi ni matendo maovu yote atendayo mwanadamu mbele za MUNGU.

Warumi 6:12 '' Basi, dhambi isitawale ndani ya miili yenu ipatikanayo na mauti, hata mkazitii tamaa zake;''mKama kuna kitu cha kwanza ambacho mwanadamu anatakiwa kushughulika nacho basi ni kuacha dhambi ili kuishi maisha matakatifu.

Kwanini tunajifunza njia hizi saba za kukusaidia kuacha dhambi?

Ni kwa sababu hakuna siri kwa MUNGU.Mithali 15:3 ''Macho ya BWANA yako kila mahali; Yakimchunguza mbaya na mwema.'' Kwa MUNGU matendo yetu yote yako wazi mbele zake.
Na kama mtu asipoacha dhambi na asipotubu maana yake matendo yake yataendelea kukaa, na siku ya mwisho kama matendo yake yalivyokuwa angali alipokuwa duniani ndivyo atakavyolipwa siku ya mwisho.Obadia 1:15 ''Kwa maana hiyo siku ya BWANA i karibu juu ya mataifa yote; kama ulivyotenda, ndivyo utakavyotendwa; malipo yako yatakurudia juu ya kichwa chako mwenyewe.''
Waliotenda mema katika KRISTO wataupata uzima wa milele na waliotenda mabaya wote watapokelewa na ziwa la moto. Ni muhimu sana kuacha dhambi. Ni Muhimu sana kutafuta njia za kuiacha hiyo dhambi inayokusumbua. 1Timotheo 1:15 ''Ni neno la kuaminiwa, tena lastahili kukubalika kabisa, ya kwamba KRISTO YESU alikuja ulimwenguni awaokoe wenye dhambi; ambao wa kwanza wao ni mimi.'' Kumbuka kuwa ukimpokea YESU na ukatubu kwake hakika dhambi zako zote zitafuta na MUNGU hatazikumbuka tena. Lakini usipotubu na kuokoka hakika uovu wako utadumu hadi siku unaondoka duniani maana hukutubu na kuacha uovu huo. Kuna watu hudhani kwamba hawawezi kuacha dhambi lakini ukweli ni kwamba huo ni uongo tu wa shetani kuhakikisha mwanadamu huyo haendi uzima wa milele. Kama kuna dhambi inakutesa na hujui jinsi ya kuiacha nakuomba jifunze ujumbe huu na uuhamishie katika matendo utashinda.

NJIA SABA ZA KUKUSAIDIA KUIACHA DHAMBI INAYOKUSUMBUA.

1. Kumtii MUNGU kupitia Neno lake Biblia.
Yakobo 4:7-10 '' Basi mtiini MUNGU. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia. Mkaribieni MUNGU,naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili. Huzunikeni na kuomboleza na kulia. Kucheka kwenu na kugeuzwe kuwa kuomboleza, na furaha yenu kuwa hamu. Jidhilini mbele za BWANA, naye atawakuza. ''
·        Njia muhimu za kumtii MUNGU ni kumpinga shetani.
·        Ni kujitenga na kila jambo la kishetani.
·        Kumtii MUNGU ni kumwabudu katika Roho na kweli.
Kama kuna dhambi inakutesa ni kwa sababu tu hujaamua kumtii MUNGU. Kumtii MUNGU ni kuiacha dhambi hiyo kwa nguvu kisha kuhamishia nguvu zako kwa MUNGU. Ndugu anza kuanzia leo kumtii MUNGU na Neno lake utashinda.

2. Kuishi maisha matakatifu.
1 Petro 1:15 '' bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote;'' Mtakatifu kinyume chake ni mtenda dhambi. Kama unataka kushinda dhambi basi acha dhambi na kuanza kutenda mema, huo ndio utakatifu. Anza tu kuipenda mbingu kwa kuamua kuishi maisha matakatifu. Jitenge na kila vishawishi vilivyokufanya uingie dhambini. Jitenge na marafiki wabaya wote. Acha tabia zako zote ambazo ni za dhambi. Acha ulevi, uzinzi, uongo na kila dhambi. Amua tu kumpendeza MUNGU kwa kuanza kuishi maisha matakatifu kila siku. Kama ukiamua hakika utaona nguvu ya MUNGU ya kukusaidia kuishi maisha matakatifu. Kumbuka huwezi kuishi maisha matakatifu kama uko mbali na MUNGU, uko mbali na Neno la MUNGU, Uko mbali na watakatifu wengine ambao watakusaidia kusonga mbele vyema, ndio maana ni muhimu sana wewe ukaokoka na kuanza kuwa mhudhuliaji wa vipindi kanisani ili ukue kiroho na ukikua kiroho itakuwa rahisi sana kwako kushinda dhambi.

3. Kuokoka.
Yohana 3:16-21 ''Kwa maana jinsi hii MUNGU aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana MUNGU hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa MUNGU. Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu. Maana kila mtu atendaye mabaya huichukia nuru, wala haji kwenye nuru, matendo yake yasije yakakemewa. Bali yeye aitendaye kweli huja kwenye nuru, ili matendo yake yaonekane wazi ya kuwa yametendwa katika MUNGU. '' Kuokoka ni jambo la muhimu sana kama unataka kuzishinda dhambi. Kuokoka ndio mwanzo wa mwanadamu kumwabudu MUNGU katika Roho na kweli. Kuokoka ni kumpokea BWANA YESU kama Mwokozi wako. Hakuja jambo zuri na muhimu kwa kila mwanadamu kama kumpokea YESU na kuanza kuishi maisha matakatifu. Kama unataka kuishinda hiyo dhambi nakuomba okoka na uwe mhudhiliaji wa ibada, huko kanisani utapata maarifa sahihi ya kukusaidia kushinda dhambi na mambo ya ulimwengu.

4. Kujitenga na dhambi.
Warumi 6:23 '' Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.'' Biblia iko wazi sana ikisema kwamba dhambi ina matokeo mabaya sana. Dhambi ina mshahara na huo mshahara unaitwa mauti yaani kutengwa na MUNGU. Na mauti hiyo kama Mwanadamu huyo hatatubu maana yake mauti hiyo ya dhambi itazaa jehanamu. Kama unataka kushinda dhambi hakikisha unajitenga na kila dhambi. Kila kisababishi cha dhambi hakikisha unakaa mbali nacho. Kama ni wanadamu ndio hukushawishi kuingia dhambini nakuomba leo amua kuwa karibu na YESU mwenye uzima wako. tii Neno la MUNGU utashinda. Kama unaweza kuacha kula chakula fulani ulichokatazwa kula na daktari, basi mimi naamini kabisa kwa njia kama hiyo hiyo unaweza kuamua kuacha dhambi zote, maana ukitenda dhambi kuna madhara kama ambavyo ukila chakula kile ulichokatazwa na daktari. Ndugu, amua tu kutoka moyoni mwako kuacha dhambi zote na utabarikiwa rohoni na mwilini.

5. Kuutumia muda wako wote vizuri na kwa malengo mema.
Waefeso 5:15-17 ''Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima; mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu. Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya BWANA.'' Biblia inakushauri kuukomboa wakati maana nyakati hizi ni nyakati za maovu mengi. Muda ambao unautumia disko ungeutumia kwa MUNGU ungeziepuka dhambi. Muda ambao unautumia kuzini ungeutumia katika maombi ungeepuka dhambi. Dhambi unaweza ukaishinda kwa kuamua tu kuutumia muda wako vizuri. Kama rafiki yako anakuita ili mkafanye mabaya hakikisha muda huo wewe utumie kwa MUNGU. Hudhuria semina za Neno la MUNGU. Hudhuria mikutano ya injili. Nenda kanisani na utumie muda wako mwingi katika mabo ya MUNGU utashinda
.
6. Kufunga na kuomba.
Mathayo 17:21 ''Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.'' Kazi mojawapo ya maombi ni kuutiisha mwili ili tamaa mbaya zisiinuke. Kazi mojawapo ya maombi ya kufunga ni kuifanya roho yako iutawale mwili na sio mwili kuitawala roho. Kama huwa huwezi kupata muda wa kuomba ni ngumu kushinda ya dunia. Kama huwa huwezi kupata muda wa kufunga na kuomba ni ngumu kushinda dhambi. Nakushauri kuanzia leo uwe na muda wa kuomba na kufunga itakusaidia. Sio yale maombi ya kuombea chakula tu na wewe unajiita muombaji, wala sio yale maombi ya kabla ya kulala unaomba dakika moja na wewe unajiita muombaji bali maombi ya kudumu na ya muda mrefu. Sio yale maombi ya kukariri na wewe ujaiita muombaji, bali ni maombi yanayotoka katika moyo wako kwa imani sio kukariri.
Ø Tafuta ushindi wako katika maombi.
Ø Ita utakatifu kupitia maombi yako.
Ø Ita nguvu za kuishinda dhambi kupitia maombi.
Ø Utiishe mwili wako kupitia maombi na kufunga.
Hakika ukizingatia utashinda.

7. Kuenenda kwa ROHO MTAKATIFU.
Wagalatia 5:16 ''Basi nasema, Enendeni kwa ROHO, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.'' Kazi mojawapo ya ROHO wa MUNGU ndani yetu ni kutusaidia kushinda mambo yote ya ulimwengu. Changamoto ya wanadamu ni jinsi ya kumpata huyo ROHO MTAKATIFU maana yeye hachangamani na uovu, yeye ni mtakatifu na akiingia ndani yako atakusaidia kuishi maisha matakatifu ila kama tu ukimtii. Mambo mengi yanayokuja mbele yako ni mapando ya giza ili kukufanya utende dhambi, lakini akiwapo ROHO wa MUNGU atakusaidia jinsi ya kuepuka dhambi. Unaweza kukuta Binti unaitwa na rafiki yako, yule rafiki yako anakuwa amepanga akupe madawa ya kulevya kisha atembee na wewe, Kama una ROHO wa MUNGU ni lazima tu atakukataza kwenda maana yeye anajua jambo kabla hata halijatokea. ukimtii ROHO wa MUNGU utashinda.

Asante kama unanielewa ndugu yangu.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu. Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha. Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka. Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU. 0714252292.
mabula1986@gmail.com
Ubarikiwe sana kwa kusoma somo hili.

Jumapili, 12 Novemba 2017

MTAZAMO WANGU

Usimkosee Mungu kwa vitu vitatu naam kwa vitu vinne hautakiwi kuikosa mbingu
  1. TUMBO
  2. MAVAZI
  3. UPAKO
  4. NDOA

1.    Hakuna kitu kizuri kama kula na kunywa mbele za Bwana maana nayo ni karama aisee {mhubiri 3:13 Tena ni karama ya Mungu kila mtu apate kula na kunywa, na kujiburudisha kwa mema katika kazi yake yote.} hata mimi napenda kula na kunywa sana na kufurahia kila chakula na kinywaji changu. Lakini kuna kitu cha kuchunga kila karama ina mipaka yake hata karama ya kulihudumia tumbo inamipaka yake tena mikubwa. Mwanzo 2:16-17{Bwana Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula,walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika}. Umepewa kula na kunywa na kufurahi lakini yakumbuke masharti ya kula na kunywa n siyo kujiendea kama usiye na akili. Huo mwili unaohitaji chakula inatakiwa upate nguvu na afya siyo kufa ndio maana adam akaewa angalizo mappema kabisaa. Naamini katika biblia sheria ya kwanza ilihusu chakula kwa mwanadam na ndio agizo la kwanza kabisaa. Kuna watu wanahisi kila kitu ni chakula na kunywa tu huku afya zao au uzima ndani yao unatetereka kila siku na magonjwa ya ajabu ajabu yanaongezeka. Wataalam wa afya wanadai kuwa ulaji mbaya umefanya magonjwa yasoyoambukiza kuongezeka. 
                   Kwenye angalizo la kwanza lilikuwa ni kula chakula ulichoewa mwenyewe na ambacho unauwezo wa kuamua ule nini na nini usile?. Basi tumbo hutamani kila kitu kwa mda wote bali roho hutafuta ibada kwa kila jambo hapa nasemea mtu aliyempokea KRISTO nasivinginevyo. Kuna watu siyo Amani ya KRISTO ndani yao bali ni mazoea yao ndio huamua ndani yao. Ni kweli andiko lasema wazi kuleni vyote kwaajili ya dhamiri lakini kumbuka siyo kila chakula chafaa kuliwa na mwandam na si kila kinywaji cha chafaa kwa afya yako anza sasa kula na kunywa kwaajili ya roho yako mwenyewe na kwaajili ya uzima wako ndani ya KRISTO. Kula kwaajili ya kufurahia hii karama lakini uwe na KIASI katika kula kwako na kunywa kwako. Kuna watu wamejaa ubatili kwaajili ua kula tu na kunywa. Nawaonya mapema isafisheni mikono yenu na muzitakase nia zenu ili roho zimrudie YEYE aliye juu na yote na juu ya vyote ni Bwana wa vyote pia na ndie aliye mmiliki wa vyote Mungu wa enzi na miliki zote. Kwamaana wokovu wafaa sana kwake yeye aliye nao na Roho wa ahadi afaa kwa vyote na yote pia. Kuna watu walimfuta Yesu kwasababu tu walikula mikate waksahau kuwa hawajanywa maji ya uzima, je wewe tumbo lako limeokoka na vyakula vya laana na makao ya kuzimu yako nje ya viuongo vyako. Mkate usikutoe kwa Yesu kwamaana 1wakolintho 6:13 Vyakula ni kwa tumbo, na tumbo ni kwa vyakula; lakini Mungu atavitowesha vyote viwili, tumbo na vyakula. Lakini mwili si kwa zinaa, bali ni kwa Bwana, naye Bwana ni kwa mwili. 
       Utapata hasara kama uliwekeza kwa tumbo kwamaana hakuna kitakachobaki kwako siku ya hukumu lakini wewe basi jifariji kwa hii yohana 6:51 Mimi ndimi chakula chenye uzima kilichoshuka kutoka mbinguni; mtu akila chakula hiki, ataishi milele. Na chakula nitakachotoa mimi ni mwili wangu, kwa ajili ya uzima wa ulimwengu. Hakikisha tumbo lako limejaa hiki chakula kila siku za Maisha yako 
           Mandishi MICHAEL BASA 0765279698

Alhamisi, 9 Novemba 2017

CHURCH GIRLS AND CHURCH BOYS

Siku moja nilikuwa engineering pale SUA najisomea mara akapita msichana mmoja kavaa tisheti imeandikwa church girl. Nilishangaa kwa mda kisha nikajiuliza huyu ni nani? mbona mavazi yake na mwonekano wake hayana hilo neno?. Nikagundua kuwa ni mkristo mmojawapo katika makanisa ya kikristo. Kwa mtazamo wa nje linaonekana ni neno zuri lakini kwa mtazamo wa ndani halina maana yoyote. Subiri nikuambie kitu mwana wa mungu aliye hai. Kinachotakiwa kumtangaza kristo ni matendo  yako siyo maandishi ya kwenye nguo. Kristo aliyekufa msalabani na kwakufuata maagizo yake huwa hakuna mwana kanisa fulaani kwamaana kwake sisi kwa umoja wetu ni mwili mmoja. Hautakiwi hata mara moja kuwa church girl wala church boy. Kwa maana hilo ni mojawapo la tendo la mwilini kwamaana kanisa ni hali ya kupatanishwa kwa mwili na siyo roho. Soma biblia tena uone kama kuna sehem yoyote ambayo yesu anaongelea kujazwa mwili. Bali roho yako ndio inayopaswa kukaa kwa YESU na ukijazwa ROHO kamwe hauwezi kuwa wa mwilini tena bali utakuwa mtu wa kuishinda dhambi. Tazama church boys na church girls wengi. Utaona maisha yao ya kiroho ni machanga kwa maana upendo wao hauko kwa kristo bali kwa jengo na jina la dhehebu analotumika. Lakini kristo ambaye kwa pendo lake ndio tunapaswa kuliishi na kulitangaza ni uzima wa milele tu. Na uzima wa milele ndio huu wakujue wewe Mungu mmoja wa kweli na wapekee na Yesu kristo uliyemtuma. Kuna wengine wameenda mbali zaidi kwa kuanzisha mijadala kuhusu dhehebu Fulani ni bora kuliko dhehebu Fulani. Sikiliza nikuambie huo siyo upendo wa kristo kwa maana vipimo vya ubora vipo katika maarifa ya kujua Mungu anataka nini kwa mda huo juu yako. Soma tena biblia uone kama pendo la kristo ndilo hilo unalotangaza wewe kwenye mijadala yako. Yesu alikufa msalabani kwaajili ya watu wote na siyo baadhi ya watu tu. Hakuna ubora wa dhehebu ndani ya KRISTO mwenyewe bali kuna ubora wa mtu atendaye mema ndani ya KRISTO. Kwahiyo hayo majengo yanayowachanganya mpaka mkaanza kujifunza historia ya dhehebu lenu ili ukitembea ujisifu kwa wengine ni upuuzi na kujilisha upepo. Soma neno ujazwe Roho mtakatifu uone kama utabaki mtu wa kuwaza chini ya viwango vya kiroho kiasi hicho. Unamkuta mtu  kajiandika I LOVE JESUS lakini maisha yako hayaakisi hata kidogo hilo neno hata mawazo yako tu hayajui kama kweli kuna YESU ndani yako. Badilika ndugu mpende YESU kwa moyo wako wote, roho yako yote, matendo yako yote, nafsi yako yote na akili zako zote. Ili yeye aliye Bwana wa rehema na neema akutakase mwili wako, nafsi yako na roho yako siku zote za maisha yako. Biblia inasema wazi kabisaa kuwa utatambuliliwa kwa matunda yako mathayo 7:20. wala siyo kwa maandishi kwenye mashati yenu wala siyo kwa kuwa church girl and church boy ambao ni ushetani mkubwa ndani ya kanisa.  

Jumatatu, 6 Novemba 2017

NDANI YA DINI YANGU----5


MATENDO YAKE HUMTANGAZA KRISTO{kusoma utangulizi bofya hapa}

"Usiangalie matendo yangu bali sikia nasema nini kwako au fuata ninachosema" moja ya hoja maarufu sana kwa wakristo wengi wasiojua kwanini wanamfuata KRISTO. Ni kweli Mungu huichunguza mioyo kama biblia inavyosema kwenye mstari wa 1 Samuel 16:7…Bwana haangalii kama binadamu aangaliavyo; maana wanadamu huitazama sura ya nje, bali Bwana huutazama moyo. Subiri nikuambie kitu kimoja ambacho unatakiwa ukielewe kutoka kwangu na si kwamwingine biblia ni kitabu kitakatifu huwa kinachanganya kama usipoweza kufunuliwa kwa Roho mtakatifu. Kuna wachungaji kwa kutojua maana halisi ya neno au msitari huitafasiri vibaya na huenda nawewe ulichukua kwake. 
             Wengine huitafasiri kwaajili ya kuficha udhaifu wao na hao ndio laana imekaa kwao na ndio waalim wa uongo walionenwa ujihadhari nao mapema nakuonya pia. Kuna siku nilikuwa nafundisha nakumbuka nikataka kutoa mfano nikaonya mapema natumia tafsiri isiyo takiwa kuitumia kwenye kila mazingira bali ni kwa mazingira ya mfano huu tu. Sasa kama nisingetoa hiyo kuna watu wangechukua kama ni tafsiri ya kijumla na kuna mazingira ingepingana na wao wenyewe kutumika. Swali la msingi JE NI KWELI MUNGU HUANGALIA MOYO TU? KAMA NDIO KWANINI NIANDIKE MATENDO? KAMA HAPANA JE HUO MSITARI NI WAUONGO?. Nikutoe hofu kwanza kama umeshaanza kuwaza nitajibuje kwenye hayo maswali mawili hapo juu. Kwa msitari huo hauna tatizo kabisaa kama ukiutumia kumuonya mtu ambaye kwa nje ni msafi au unasisitiza usafi ndipo unasema Bwana haangalii nje bali huangalia mioyo na kuvichunguza viuno yeremia 17:10{Mimi, Bwana, nauchunguza moyo, navijaribu viuno, hata kumpa kila mtu kiasi cha njia zake, kiasi cha matunda ya matendo yake}.
         Je unakumbuka kuwa dhambi huanzia ndani ya mtu na siyo nje kama wengi wanavyodhani soma tena mwanzo 4:7{Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde.}jiulize sasa hapo mlango ni upi?. Soma tena ayubu{Job 38:17 Je! Umefunuliwa malango ya mauti, Au umeyaona malango ya kuzimu?}. Uone kitu kingine kipya kabisaa ndipo ujue kuwa biblia haishii hapo wewe unapoona kwa upeo wako wala kwa maandiko ya BASA tu. Pia maandiko siyo ulokole na wala siyo UKRISTO kwamaana UKRISTO ni kuwa ndani ya KRISTO na ULOKOLE ni kumiminwa ndani ya ROHO MTAKATIFU. Ukitaka kuwa MKRISTO kweli jifunze msalabani sana na ukubali na kutii kila andiko kama lilivyo bila kusema mtumishi fulani alisema hivi au vile. Kuna mtu mmoja alifundishwa na watu wawili tofauti mtu wa kwanza alifundisha kutopenda kumpa mkono kila mtu na hakuelezea kwanini na kwa mazingira gani?. Mtu wa pili akafundisha kuwapenda wale wa nje na kuwasalimia kwa kupeana mikono na kama ni jinsia moja unaweza kuwakumbatia kabisaa. Swali likaja kwangu sasa je amfuate nani kwamaana wote ni wachungaji na anawaamini sana na hahisi kama kuna mmoja kasema uongo. Mimi nikacheka kisha nikamfundisha chimbuko la mafundisho yote mawili na kwanini yapo hivyo na kwenye ulimwengu wa roho yanachukuliwaje kisha na yeye afuate lipi?. Lakini nilichogundua kwa huyu mtu hajazama ndani ya Roho mtakatifu vizuri ndio maana hakuelewa ashike lipi sasa?. 
       Ndio maana nasema kwamba matendo yako yote yanatakiwa yamhubiri KRISTO, watu waduniani wanaangalia porn na wewe mkristo unaangalia halafu unataka uione mbingu sahau tu. Mungu siyo wa mzaha kiasi hicho aisee tena pole sana. Watu wanajitesa kwa kufunga na kuomba na kukesha wewe unakula siku 365 kwa mwaka na kulala masaa yote. Kuomba dakika tano nyingi halafu unataka eti ufunuliwe kwenye ulimwengu wa roho sahau tu. Mtu unatembea uchi halafu unataka Yesu aonekane kwako au ajidhihirushe labda utumie pepo aisee. Hakika Mtu ambaye roho yake inamwabudu Mungu kweli au moyo wake unakicho cha Bwana halafu kwa nje anachotoa ni uongo, uasherati, wizi, uuaji, chuki, uchonganishi, ufiraji, kuchora tattoo, huombi, husomi neno, disko umo, sehem za laana hukosi. Wasioamini wanassema kabisaa kama nawewe ukiingia mbinguni basi mimi nitakuwa malaika {mathayo 5:20}halafu unajibu utaona Mungu anaangalia moyo wa mtu haangalii matendo pumbavu kabisaa mwana wa laana wewe. 
       Wewe ndio unafanya injili inakuwa ngumu kwa watu kuipokea na kuitii kwamaana haoni tofauti yako wewe ambaye ni mfuasi wa KRISTO na yeye ambaye bado anaabudu miungu mingine. Basi tuangalie matendo yako kama Mungu anayatazama kama moyo au vyote viwili. Tito 1:16 Wanakiri ya kwamba wanamjua Mungu, bali kwa matendo yao wanamkana; ni wenye machukizo, waasi, wala kwa kila tendo jema hawafai. Huyo siyo mimi bali ni walaka kwa tito ambao mwandishi anaonesha kitu kidogo kwamba kuna matendo ambayo ukiyafanya unakuwa unamkataa Mungu kabisaa. Mkirsto mwenzangu hujui kwamba mdomo wako unaweza kuwa unamkubali Mungu kweli lakini mwili wako unafanya ibada za miungu kila siku. Badilika wewe mkristo mwenzangu hakikisha matendo yako yanatoa kile kilichoko ndani ya moyo wako ambacho Yesu mwenyewe alifundisha. Hatuna kipimo kingine cha utakatifu isipokuwa matunda ya ROHO MTAKATIFU.

Mwandishi: MICHAEL BASA 0765279698/+255789799199

Alhamisi, 2 Novemba 2017

NDANI YA DINI YANGU---4

AMEJAZWA ROHO MTAKATIFU (KUSOMA UTANGULIZI BOFYA HAPA)
      Kuna Rafiki zangu wa dhehebu Fulani Roho kwao ni stori za zama za kale sana kabla ya dunia kuwepo. Huwa nacheka tu kwamaana hadithi za kizee zisizokuwa za dini ndizo zimekuwa sahihi kwao na usahihi wa neno umekuwa ni upotofu kwao. Kuna wengine pia ukiwakuta wanajiita makanisa ya kiroho sikatai maana wao wanajiona hivyo wanategemea viongozi wao kwa kila jambo hata ambalo Mungu anatakiwa kuonekana kwa uwazi kwao wenyewe wanamsubiria mchungaji wao au nabii wao. Sipingi kuwafuata maana hata mimi nina baba zangu wa kiroho lakini hawatakiwi kuchukua nafasi  ya Mungu. Yesu alitoa uhuru kwa kila mtu kujiombea nasiyo kutegemea mtu Fulani. Ndio maana kwa biblia ikasema Bwana anazichunguza nyoyo na huvijaribu viuno. Sasa wewe na huyo kiongozi hamjui kuwa mnamtenda Mungu dhambi. Je mmesahau kuwa amelaaniwa mtu yule amtegemeeaye mwanadam??. Wengine pia kuna roho kiburi na roho uhuru wamewaingia hao hata ukiwahubiria vipi hawaelewi kitu. Tena chunga unaweza kuambulia matusi yanguvu kweli au ukaishiwa kutengwa na kanisa lako. Huwa naukumbuka sana wimbo wa MUNISHI unaitwa “WANAMWABUDU NANI?”. 
      Wengine wamejazwa roho wakajihisi watamuona Mungu wakati biblia imeagiza kujazwa ROHO tena siyo ROHO tu bali awe mtakatifu ambaye anakuja kwako kwa kazi zifuatazo:-
     ➤KUKUFUNDISHA 
     KUKUONYA
     KUKUELEKEZAKUKUJULISHA MAMBO YAJAYO
     ➤KUKUFUMBULIA MAFUMBO MAKUU YA MUNGU
     ➤KUKUPA AMANI
     KUSHUHUDIA PAMOJA NA NAFSI YAKO KUWA WEWE NI MWANA WA MUNGU
     KUKUOMBEA
     KUKUONGOZA
     KUKUPA HUDUMA KWAAJILI YA UFALME
       Unapomkataa Roho mtakatifu inamaana umekataa vyote hivyo. Inakuwa ni ngumu sana kwa wewe kujua mipango ya Mungu juu yako kwa wakati huo. Pia chamaana Zaidi ya hivyo vyote soma nami warumi 8:14{Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu}. Kuwa MKRISTO kwamaana nyingine ni kuwa mwana wa MUNGU kuwa au kuwa chini ya miliki ya Mungu mwenyewe au kuonesha kuwa Mungu yupo katikati ya wanadam. Kuonesha mfano wa watu watakaoingia mbinguni na kustarehe kwa Mungu baba. Mtu hapokei Roho wa Mungu akabaki na matendo au tabia ya asili ya dhambi 1wakorintho 2:14 kwamaana mtu wa matendo ya asili bado amepotea.
        Yohana 14:16-18 {Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele;ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu.Sitawaacha ninyi yatima; naja kwenu}. Roho siyo maamuzi ya dini Fulani tu bali ni agizo la kutobaki yatima kama Yesu mwenyewe alivyoagiza kwa wanafunzi wake. Ukimpata Roho mtakatifu unaanza kukamilishwa sasa katika ukristo wako na siyo dini ile ndio wanajazwa Roho mtakatifu au watu wa jinsi hii ile pekee ndio wanatakiwa kuwa na Roho mtakatifu. Kwamaaana wote waliompokea aliwapa uweza wa kuwa wana wa Mungu hapa haijasema na lazima uwe msabato au mlokole au mkatoliki au lutherani bali ni kule kuwa Mkristo na ukampokea Roho wa Mungu basi wewe umekuwa mwana wake kweli. Kwamaana Roho wa Mungu hakai sehem chafu bali hukaa sehem safi tu. Unaweza anza jiuliza napokea Roho wa Mungu kwasasa hapa nilipo, nakutoa wasiwasi kwamba kumpokea ni rahisi sana fanya yafuatayo:-
○ Jichunguze njia zako je ni kipi ambacho unafanya lakini hakipo sawa kabisaa kibiblia anza kukiacha hicho maana huwezi kujazwa ukiwa bado unatenda dhambi, kama dhehebu lako halizingatii ubatizo wa Roho basi hamia dhehebu jingine ambalo linasisitiza kuacha dhambi na kujazwa Roho mtakatifu. Tubu dhambi zako zote kwa kumaanishan jutia dhambi zako zote ulizotenda wakati bado unahangaika kwenye dhambi na usitamani kurudi huko tena. Elewa kitu kimoja unaweza kumdanganya BASA lakini huwezi kumdaganya Mungu kwamaana yeye huichunguza mioyo ya wote wamwendeao kwa kumtaka YEYE na kama bado unawaza maovu hawezi kukusikia hata kama ukeshe unaomba na kufunga juu. BADILISHA NJIA ZAKO
○ Uwe na njaa ya kujazwa Roho mtakatifu, tamani kuwa na Roho mtakatifu toka moyoni mwako omba kwa Mungu kila siku kuwa naye. Usiache kuomba hata baada ya kujazwa kwasababu kumpata siyo kinga ya YEYE kutoondoka kwako. Kwahiyo omba kila siku aje kwako uzidi kuzama zaidi ndani yake upate mafunuo kupitia Roho mtakatifu. TAMANI KUWA NAYE KILA SIKU
○ Mtumie kila siku ili adhihirike kwa wingi zaidi kwa maana kadri unavyomtumia ndivyo unavyozidi kuimarika kiroho. Kuzama kwako kutakupa kujua zaidi alama na tafsiri za kiroho na pia ndio utaanza kufurahia kumfuata KRISTO. 
         Baada ya kujazwa Roho mtakatifu furahia kuwa ndani yake wala usiruhusu akakuondolea uwepo wake ndani yako. Kuna watu walipokea na wao wakampoteza na kipimo cha Roho mtakatifu siyo kunena kwa lugha bali ni udhihirisho wake kwako kwa matunda yake tisa ambayo ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; ukiona mtu anayo matunda ya Roho mtakatifu huyo ndio mwana kweli wa Mungu na amejazwa Roho wake kweli. Ukisoma hayo matunda hayajasema dini fulani bali yanamtaka mtu ambaye anataka kuwa mfuasi kweli wa KRISTO awe nayo. Kwamaana huyo msaidizi mwingine ndiye humtengeneza mtu kuwa hivyoo. Tunda la Roho mtakatifu inatakiwa lionekane kwa nje na siyo wewe kujitangaza kama BASA anadharau watu wengine haijalishi nitakuwa dhehebu gani wala kanisa la mchungaji nani na awe na upako kiasi gani?. Lakini bado nitakuwa sina Roho mtakatifu na siku ya mwisho makao yangu ni kwenye ziwa liwakalo moto. Basi ndugu yangu nakusihi kwa upole wake KRISTO YESU hebu tafuta ahadi yake ya Roho uwe na uzima wa milele ndani yako. Barikiwa sana

Mwandishi MICHAEL BASA 0765279698/ +255789799199

Inaendeshwa na Blogger.